Mada ya Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa hospitali (by Informer) ndiyo iliyo trend zaidi ktk wiki hii!!

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Nimejaribu kupitia mada zote (wengine huziita "threads") zilizopostiwa wiki hii ktk jukwaa hili, hii ndiyo iliyo trend zaidi kwa kuwa na wasomaji (viewers) wengi zaidi (wanaokaribia 200,000) mpaka sasa ninapoandika hii yangu pamoja na wachangiaji wanaokimbilia idadi ya 3,500 sasa....

Hii ni katika kipindi cha muda usiozidi siku sita jambo ambalo hujitokeza kwa nadra sana unless mada husika ihusu jambo ambalo ni very sensitive sana....

Kusema ukweli Mada (thread) zote kumhusu Magufuli ama makinikia ama chochote wiki hii hazikuwa na soko kabisa kwa kiwango hata cha kupuuzwa tu. Wiki hii, habari ilikuwa Tundu Lissu na ya huyu Informer ndiyo iliyo lead na inaendelea kuongoza mpaka sasa....

Kuna mdau mmoja aliposti mada isomekayo "Hawaamini kuwa kumbe Tundu Lissu ni mtu anayependeka kiasi hiki ". Moja ya uthibitisho wa karibu sana wa kupendwa kwa jamaa huu, mpigania haki huyu, ni huu....

Kwani ukiachilia mbali uwingi wa watu ktk jukwaa hili unaofutilia mjadala unaohusu hali ya Tundu Lissu ukiachilia mbali mada zinazopostiwa, ni wazi kuwa jamaa huyu ni mtu wa watu kwa kiwango cha kuwatisha sana wabaya wake....

Mimi ni muumini wa dini ya kikristo. Miaka takribani 2,000 iliyopita alitokea binadamu mmoja wa ajabu na kipekee sana kwa jina la Yesu Kristo...

Huyu Yesu Kristo alikuwa ni kipenzi cha watu lakini adui mkubwa wa watawala wa kiyahudi na mpaka leo hii vivyo hivyo....

Uadui wake kwa watawala msingi wake ulikuwa yeye ni kukemea na kupinga unafiki na matendo mabaya ya watawala hawa dhidi ya wananchi waliokuwa wanawaongoza....

Ni kwa sababu hii, watawala wa serikali ya wakati huo kwa kutumia kila aina ya njia na mitego walijaribu kushtaki Yesu Kristo kwa mashtaka ya uongo mara kwa mara lakini aliwashinda....

Mbinu hii iliposhindikana, walitumia mbinu ya fedha. Fedha kwa maana ya watawala kuwahonga baadhi ya watu wa karibu na Yesu Kristo ili wamkamate na kisha kumuua wakiamini kuwa ndiyo itakuwa salama yao na hivyo kuendelea na "kushinda kwa kishindo" ktk chaguzi zitakazofanyika na hivyo kuendelea kutawala kwa raha zao...

Yuda Iskariote, mtumishi na mmoja aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo, akanasa ktk tamaa ya hongo ya watawala mafisadi na wauaji na waroho wa madaraka wa kiyahudi. Akahongwa vipande thelasini vya fedha ili mradi atoe siri (amsaliti) Yesu Kristo..

Ikatokea, Yesu kristo akaja akakamatwa, akashitakiwa na kwa kuwa maagizo ya hukumu isiyo haki "yalitoka juu", kesi ikaisha na Yesu Kristo kuhukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Wakati huo adhabu hii ilitekelezwa kwa kusulubiwa msalabani hadharani, akigongomelewa misumari ya nchi nane juu ya msalaba pamoja na mateso mengine kama kutukanwa, kutemewa mate na kuchapwa fimbo hadi alipokufa...

Hili la Tundu Lissu lina mfanano wa kiasi fulani na hili mtetezi wa haki za wanyonge, Yesu Kristo.....

Tundu Lissu ameshtakiwa kwa kesi nyingi sana za uongo ili mradi tu wapate sababu za kumfunga. Lakini zote hizo hahukutwa na hatia....

Njia rahisi na nyepesi ikaonekana kuwa ni kumzimisha kabisa kwa maana kutoa uhai wake. Akamiminiwa risasi karibu 40 na kati ya hizo, 8 zikipenya ktk maungo ya mwili wake....

Mungu ni mkuu na mwema sana, hazikugusa shingo, kifua ama kichwa. Yuko hospitali anauguza majeraha, amekishinda kifo..

Watu wanafuatilia kila habari inayomhusu kwa sbb inaonekana ni muujiza wa kipekee na ajabu kabisa...

Mungu mponye na mrejeshee afya yake Tundu Antipasi Mughwai Lissu, Amen..
 
Back
Top Bottom