Mada vipande: Kilichomponza Kigwangala ni starehe na kula bata, kitakachomponza Simbachawene ni kuvaa viatu over size

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,356
695,156
Ni matukio mfuatano wiki iliyipita na hii.. Matukio yapo kila siku ni kama series ya DAYS OF OUR LIFE... matukio yanayotrend wiki hii ni mahusiano na siasa. Achana na ingizo jipya la Hamida

Kigwangala hajatumbuliwa lakini ni wazi sasa ni swala la muda tuu Kakalia kuti kavu ana kifurushi cha tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi (cheo)

Wizara aliyopewa ni ngumu sana.. Kwakuwa imejaa mirija ya kula. Inahitaji mtu mwerevu, mkomavu na mtulivu sana kuweza kuimudu hii wizara ya utalii. Kuna mambo matatu huwa hayaepukiki kwenye hii wizara ya utalii (ongeza na maliasili) vitu hivyo ni ngono, starehe na rushwa, hivi vimewadondosha wengi. KIGWANGALLA HAPONI

Kalia lia sana mitandaoni kuonesha kuonewa na kutengenezea tuhuma feki majungu na fitina lakini kuna upande hausemi. Yale ya sirini ayafanyayo hata wewe usingejisema.

Wizara sio mtu mmoja, Wizara haiwezi kukosa PRO. Sasa hata kama ni kutangaza utalii kwanini kote uonekane wewe tu? Kuanzia kwenye mabango mpaka kwenye ma swimming pools.

Hivi wewe ndio mnyama na maliasili? Hata kama ni kuhamasisha utalii wa ndani kuna baadhi ya safari angewapa wasaidizi wake. Kuna baadhi ya majukumu angewapa na wengine wanohusika ili nao walau waambulie chochote. Kwenye hili kafeli vibaya sana. Ukila usipige kelele. Ukila na kipofu usimshike mkono.

Simbachawene ni almost anatia huruma. Kama ukiweza kumuuliza kimyakimya na kwa siri kuhusu uteuzi wake mpya atakwambia wazi hajafurahia. Sikumbuki ni wapi alipewa nafasi ya kutumika na akatenda kwa weledi. Mara zote ameishia kuhamishwa na mwishowe kutumbuliwa. Hata hapa kama akiweza kumaliza hii ngwe atamaliza kwa muujiza.

Mojawapo ya wizara zenye changamoto kubwa ni wizara ya mambo ya ndani. Kwa sehemu kubwa wizara hii inahusika na usalama wa nchi pia.

Inahusika na wageni wote pia kutoka mataifa mengine.Inahusika pia na vibali na nyaraka mbalimbali za wageni na wenyeji

Wizara ya Mambo ya Ndani ni wizara nyeti sana na inahitaji mtu mahiri, mwerevu, msomi wa intelijesia, mahusiano, mzalendo na mtoa maamuzi asiyeyumba.

Je, Simbachawene anatosha?

Naamini ndani ya ccm kuna wasomi wengi wazuri wenye uzoefu na weledi ambao wangetosha hii nafasi... Nafasi nyingi za ukuu wa wilaya zinashikiliwa na wanajeshi wa ngazi za juu japo wako kiraia.. Je kuna hatari yoyote kama mmojawao angekasimiwa hii nafasi? Kwa kufuata utaratibu wa nafasi hakiba za ubunge kisha kuteuliwa uwaziri wa nafasi husika?
Inawezekana kabisa simbachawene atakuwepo hapo lakini kwa miongozo

Jr
 
Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
tapatalk_1576482213385.jpeg


dodge
 
Kigwangala anafanya influencer marketing na ndio maana anatumia sana wasanii pia katika kupromote utalii wa ndani.

Kigwangala ndio figure na mwenye influence zaidi hivyo, yeye kuwapo mbele katika kampeni kuna impact kubwa zaidi kuliko angewekwa "just anybody". Hivyo sio matter ya nani ale na nani asile, its a matter of impact kwa investment...

By the way nakubaliana na wewe. Wizara ya utalii inatosha kututoa katika umaskini ila bado haijapatiwa kichwa business minded cha kuivusha ilipo..
 
Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.View attachment 1332677

dodge
Sasa hata kama ni kutangaza utalii kwanini kote uonekane wewe tuu? Kuanzia kwenye mabango mpaka kwenye ma swimming pools.. Hivi wewe ndio mnyama na maliasili?
Huyu jamaa naona akili zake zinataka kufanana na yule mnyiramba aliejiandika kwenye mawe makubwa na madaraja karibu yote nchini kua yeye ndie mfalme wa .

Sent from my DUB-LX1 using Tapatalk
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom