MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Mkuu unaweza kutupa mrejesho baada ya kuwaona wataalamu wa tiba za watoto maendeleo yapoje?
 
Wadau ningependa kujua mtoto hua anaanza kuongea akiwa na umri gan ? Mwanangu n wakike ana umr wa miaka miwili na miez 8 mpk leo bado hajajua kuongea vizur zaidi ya kusema mama, baba, dada, bibi, acha, sitaki. Bas.nilimpeleka kwa docta akamchunguza akasema ulimi wake uko tu vizuri. Msaada wenu na maon yenu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wa mwaka mmoja huanza kuwa na sauti, ataita bila majina lakini utaelewa anaita.

Miaka miwili anaonge neno moja mfano mama, Pipi, mma nk

Miaka 2.5 anaanza kuunganisha maneno kama baba pipi,

Miaka mitatu anaongea sentensi nzima.
 
Mtoto wa mwaka mmoja huanza kuwa na sauti, ataita bila majina lakini utaelewa anaita.

Miaka miwili anaonge neno moja mfano mama, Pipi, mma nk

Miaka 2.5 anaanza kuunganisha maneno kama baba pipi,

Miaka mitatu anaongea sentensi nzima.
Hao ni wa ushuani,ila kwa uswazi mtoto miaka 2 anaimba kanyaga ya mondi na kucheza juu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wa mwaka mmoja huanza kuwa na sauti, ataita bila majina lakini utaelewa anaita.

Miaka miwili anaonge neno moja mfano mama, Pipi, mma nk

Miaka 2.5 anaanza kuunganisha maneno kama baba pipi,

Miaka mitatu anaongea sentensi nzima.
Miaka miwili mtoto anaongea vizuri sana
 
Bora huyo wako, kuna dogo wa best yangu sasa ana miaka 3 na miezi yake anajua baba, mama na maneno machache tu.
Hilo muda mwingine ni tatizo la kiakili lililosababishwa na misukosuko wakati wa kuzaliwa.
Muhimbili wanawafanyisha mazoezi
 
Hii genetical zaidi. ..waulize bibi zake wa pande mbili kama kwel wazazi wake waliwahi au walichelewa kuongea baada ya hapo ndo utajua tatizo liko waapi
 
Tatizo la watoto kuchelewa kuongea ni la miaka mingi sana lakini miaka ya hivi karibuni limeonekana kuongezeka kwa kasi sana siku hadi siku.

Kuchelewa kuongea ni moja kati ya matatizo ya mawasiliano ambayo huwakuta watoto: tatizo hili hujitokeza pale ambapo watoto hushindwa kuongea kuendana na hatua ya ukuaji walioifikia. Mtoto hushindwa kuongea au kuwaelewa watu wengine wakiongea. Aidha maendeleo ya lugha kwa mtoto husimama au huenda taratibu sana.

AINA ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Zipo aina tatu za tatizo la kuchelewa kuongea kwa watoto. Aina ya kwanza ni ile ambayo mtoto hushindwa kusikiliza nini anaambiwa. Aina ya pili ni ile ambayo mtoto hushindwa kujieleza juu ya ni nini anataka. Aina ya tatu ni ile ambayo mtoto hushindwa kufanya vyote: yaani hushindwa kujielezea na kusikiliza wengine.

Kutokana na uzoefu wangu, aina ya tatu hujitokeza kwa watoto wengi zaidi, watoto wanaoshindwa kujieleza kwa kuongea pia hushindwa kujua nini wanaambiwa na watu wengine.

DALILI ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Mtoto ambaye ana tatizo hili la kuchelewa kuongea mara zote huwa nyuma ya hatua zake za maendeleo na ukuaji. Ili mzazi/mlezi aweze kujua kama mtoto wake ana tatizo hili anaweza kuangalia kama mtoto wake ana dalili zifuatazo:-

Moja, Mtoto kushindwa kupiga kelele zisizo na mpangilio mpaka kufikia miezi 15. Kelele kama “Yaaa Yaaa”, “Daaa Daaa” au “Bluuuuu Bluuuu”

Mbili, Mtoto kushindwa kuongea mpaka kufikia miaka miwili. Kuongea neno moja moja au mawili ambayo yanaweza kumpa mzazi muelekeo juu ya nini mtoto anataka kusema. Kama vile “Mama tamu” “Mama acha” au “Baba Pira”

Tatu, Mtoto kutoweza kuzungumza sentensi fupi mpaka kufikia miaka mitatu. Sentensi kama vile “Naomba maji”, “Nataka kojoa”, “Naomba maziwa”, “Nataka mpira” au “Shikamoo Baba!”

Nne, Mtoto kuwa mzito kufuata maelekezo mpaka kufikia miaka mitatu. Mtoto kutoelewa nini anaambiwa na wenginine. Kwa mfano anaambiwa: “kaa chini” na anashindwa kujua nini anatakiwa kufanya na hata akifanya mara nyingi hufanya kinyume.

Tano, Matamshi ya maneno kuwa mabaya mpaka kufikia miaka mitatu. Kwa mfano, mpaka kufikia miaka mitatu mtoto anatamka neno, Shika-chika, Sasa – chacha au Mkate – Nkate.

Sita, mtoto kushindwa kuweka maneno katika sentensi mpaka kufikia miaka mitatu. Mtoto anaweza akawa anayajua maneno mengi lakini akawa anashindwa kuyaweka maneno katika sentensi moja akielezea kile anachokitaka hivyo huishia kulisema neno moja moja tu. Kwa mfano mtoto huishia kusema: “kula” akimaanisha anataka chakula, au “piga yule” akitaka kusema yule kampiga.


SABABU ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Kutokana na uzoefu na tafiti zangu binafsi nimebaina ya kuwa zipo sababu nyingi za watoto kuwa na tatizo la kushindwa kuongea kwa wakati, kuendana na hatua na maendeleo ya ukuaji wao. Zifuatazo ni baadhi ya sababu:-

Moja, matatizo ya kusikia kwa watoto. Mtoto mwenye matatizo ya kusikia vizuri ni ngumu sana kuweza kuzungumza kwa wakati kama watoto wengine. Ni muhimu mzazi akiona mtoto wake anashindwa kufuata maelekezo na kuitumia lugha vizuri kuendana na umri wake afuatilie kama anaweza kuwa na tatizo lolote la kusikia ili aweze kupata msaada unaotakiwa mapema.

Mbili, Usonjii (Autism). Japo kuwa kuna baadhi ya watoto hawaathiriwi na autism katika maendeleo yao ya lugha lakini, kwa watoto wengi hupelekea kuchelewa kuongea. Angalau 70% ya watoto wenye Usonji huchelewa sana kuongea. Watoto wenye usonji huongea baada ya wataalamu kuwasaidia kujifunza na kutumia lugha kuendana na mahitaji yao. Ni ngumu kwa wao kuweza kujifunza kutumia lugha bila jitihada za wataalamu.

Tatu, mtoto kukosa watu wanaozungumza mara kwa mara karibu yake. Watoto huchukua lugha moja kwa moja kutoka kwa wazungumzaji wengine na ndiyo maana mtoto akiwekwa kwa watu wanaotumia lugha ya kiingereza atazungumza kiingereza, akiwekwa na wazungumzaji wa kiswahili atazungumza kiswahili n.k hivyo kwa mtoto kukosa watu karibu yake ambao huzungumza mara kwa mara humfanya ashindwe kuchukua lugha hali inayoweza kupelekea mtoto kuchelewa kuzungumza.

Nne, Wazazi kutokuwa na maarifa na hatua na maendeleo ya ukuaji wa mtoto. Sababu hii imekuwa ikipuuzwa sana na wataalamu kila wanapoelezea tatizo hili lakini binafsi nafikiri ni moja kati ya sababu kubwa kabisa. Wazazi wengi hawajui nini wafanye ili kuwapitisha watoto wao katika hatua mbalimbali za ukuaji pindi waoneshapo changamoto hali inayoweza kupelekea watoto kukwama katika matatizo bila usaidizi. Watoto wengi hushindwa kuongea mapema kwasababu wazazi wao hawana ufahamu na jinsi lugha kwa mtoto inavyojengeka na nini wafanye endapo kukitokea changamoto.

Tano, Mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake (Njiti). Mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake huweza kuleta matatizo mbalimbali likiwemo na hili la kushindwa kuongea mapema kwa mtoto. Kwani kuna baadhi ya viungo muhimu vya mwili wake vinakuwa havikumalizika kujiunda hivyo huendelea kujiunda taratibu mara baada ya kuzaliwa kwake.

Sita, Kumwacha mtoto atumie vifaa vya kielekroniki kama vile TV na simu kwa muda mrefu. Sababu hii pia haisemwi na wataalamu wengi, lakini nimeona ni moja kati ya sababu kubwa. Mtoto wa kuanzia miezi mpaka miaka mnne endapo ataachwa kwenye TV kwa muda mrefu yaana kwa zaidi ya saa moja kwa siku ni lazima itaingilia maendeleo ya ubongo. Ubongo ndiyo unafanya na kuratibu kila kitu kinachohusiana na maendeleo ya lugha kwa mtoto hivyo kwa maendeleo ya ubongo kuvamiwa na vifaa hivi vya kieletroniki vitu vingi vinavyotegemea maendeleo ya ubongo kuendelea pia husimama. Tutaliongelea hili kwa kina wakati mwingine kwani ni pana sana.

Saba, Mahusiano mabaya kati ya mtoto na mzazi/mlezi. Mtoto kuwa na mahusiano mabaya na mzazi/mlezi wake ni sababu nyingine ya mtoto kuchelewa kuongea. Mzazi/mlezi ambaye haoneshe mapenzi na ukaribu na mtoto wake au ambaye ni mkali kupitiliza kwa mtoto akiwa bado mdogo kabisa anaweza kupelekea mtoto kutotaka kuelezea hisia au mahitaji yake mapema hali inayoweza kupelekea mtoto akachelewa kuongea.

Nane, Familia kutumia lugha zaidi ya moja. Watoto wengi wanaokuwa katika familia inayotumia lugha zaidi ya moja huwa na tatizo la kuchelewa kuongea kwani watoto hulazimika kutumia nguvu ya ziada kutoa tafsiri ya baadhi ya maneno na kufananisha katika lugha zote mbili jambo ambalo huweza kuwachukua muda ukilinganisha na yule anayekua kwenye familia inayotumia lugha moja.

Tisa, Matatizo ya mdomo kama vile uzito wa ulimi. Mtoto mwenye ulimi mzito asipopewa tiba mapema tatizo hili ni lazima litamkuta kwani ulimi ni moja kati ya viungo muhimu sana kwenye uzungumzaji wa mtoto. Yapo mazoezi na jinsi ya kufanya ili mzazi aweze kulimaliza tatizo hili. Nitaligusia siku nyingine nikiwa naelezea juu ya jinsi ya kufanya ili kumaliza tatizo hili kwa watoto.

Kumi, Matatizo ya ubongo. Baadhi ya matatizo ya ubongo kama vile Majeraha kwenye ubongo yanaweza kuathiri misuli ambayo ni muhimu katika maendeleo ya lugha kwa watoto.

Hitimisho, Matatizo mengi ya maendeleo ya lugha na kuzungumza kwa watoto yanatibika kirahisi sana kama mzazi/mlezi atatafuta tiba mapema kabla ya mtoto kufikisha miaka mitano hivyo ni muhimu wazazi/walezi wakatambua mapema kuwa watoto wao wana tatizo hili na kutafuta tiba kutoka kwa wataalamu mapema.

Tuendelee kuwa pamoja nitaandika juu ya jinsi ya kupambana na tatizo hili wakati ujao. Ni rahisi tu, endapo mzazi/mlezi ukijitoa kwa moyo na kushirikiana na wataalamu.
 
Back
Top Bottom