MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
1587622539008.png
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Naomba kujua mtoto mchanga inabidi aanze kuongea akiwa na umri gani,kwa kuzingia wale wanaowahji na wanaochelewa.Na je kuna namna unavyoweza kutambua uwezekano wa mtoto kuwa bubu na inaweza kuzulika kwa umri wake mdogo.
nitashukuu
---
Naombeni msaada wana jf.

Mtoto ana miaka mitano sasa hawezi kutamka maneno, hawezi kutafuna chakula.Nimejaribu kumfundisha lakini hafuati kile nachomfundisha au naweza sema hana utulivu wakati wa kumfundisha. Nimejaribu kumpeleka kwa madaktari bingwa wa watoto nao wameshindwa kubaini tatizo zaidi wanasema kiakili yupo fit.

Sasa basi naombeni mawazo ushauri wenu nifanyeje juu ya mtoto huyu kwani nami natamani aongee kama watoto wengine wa umri wake. Na kama unamjua daktari ambae anaweza kumsaidia mtoto huyu naomba msaada wenu. Kina mzizimkavu na wengine nasubiri mawazo yenu.
---
Naombeni msaada wenu wataalam wa afya,

mwanangu wa kiume ana miaka minne sasa but hajaanza kuongea. Napatwa na wasiwasi sana, nyimbo anaimba vizuri japo hatamki maneno yote ya nyimbo sawsawa lakini ukimsemesha hajibu but kuskia anaskia na anaelewa.

Wataalam wamempima hana tatizo lolote la ubongo yaani hata kwa shida yeyote haongei anakushika mkono na kukuonesha anachotaka.

NISAIDIEN JAMAN HIVI INAWEZEKANA AKAONGEA HATA AKIWA NA MIAKA MITANO?

Nimempeleka shule but haijasaidia
---
Habarini za Kazi.

Naombeni msaada wa ushauri hapa. Nina mwanangu ana miaka mitatu na miezi sita na mwaka huu nimemuanzisha shule. Tatizo lake ni kwenye kuwasiliana imekuwa changamoto sana. Anaweza kuimba nyimbo za shule toka asubuhi hadi jioni, anaweza kuhesabu. Kuandika na kusoma 1-20, Anaweza kusoma herufi zote A-Z.

Randomly kuna maneno mengi anatamka shida ni kwamba hawezi kujibu chochote utakachomuuliza labda ukimuambia afanye kitu flani ndo anaweza. Ila ukimwambia aseme neno flani au kitu flani anakuangalia tu. Hapa shida inaweza kuwa nini na suluhisho lake ni nini? Kama kuna mtu ana namba ya mtaalamu naomba anisaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
===
UFAFANUZI NA USHAURI WA WATAALAMU KUHUSU TATIZO HILI
Ni vipi unaweza kumsaidia mtoto wako kujifunza kuongea?

Kadri mwanao anavojifunza maneno mapya katika michezo ndivyo anavyoyabeba na kuyatumia kila siku. Zipo njia za kumsaidia mtoto wako kujifunza kuzungumza:
  • Zungumza kadri uwezavyo na mwanao. Mtazame usoni na uonyeshe kufurahia anapojaribu kuzungumza na wewe.
  • Zingatia zaidi kile ambacho mwanao anajaribu kusema kuliko jinsi anavyotamka matamshi yake. Jitahidi kumfanya mwanao ajisikie huru anapozungumza na wewe.
  • Pindi anaposema kitu sahihi, mpatie ripoti sahihi. Kwa mfano, unaweza kumwambia “ndiyo, ni sahihi, hichi ni kijiko”.
  • Mfanye mwanao kuona unachomaanisha, kwa kuzingatia unachokifanya na unachozungumza. Unaweza kusema “tunatoa viatu” huku ukimvua viatu vyake kisha “tunaondoa soksi” huku ukimvua soksi zake.
  • Pindi unampatia chakula cha mchana mwanao, weka sahani ya chakula mezani kisha mshike mikono na useme “ni muda wa chakula sasa” ataelewa kuwa chakula chake kipo tayari na kitaletwa mezani ikiwa tayari amenusa harufu na kuona maandalizi ya mezani. Anaweza asielewe maana ya “muda wa kula” kama hataona vitendo.
  • Chukua usikivu wake kwa kutaja jina lake na kumtazama machoni kabla ya kuzungumza naye. Hii itamsaidia kuelewa kuwa unazungumza naye.
  • Mpe mwanao nafasi nyingi za kuzungumza katika kipindi chote cha shughuli za kila siku. Kama unamuuliza swali muache kwa sekunde 10 ili apate muda wa kukujibu.
  • Fafanua hali mbalimbali kwa kumtambulisha maneno mengi. Nenda naye matembezi kwenye daladala, mtambulishe vitu anavyoviona na vielezee kwake.
  • Rudia kusema kile ambacho mwanao amejaribu kukuambia, hata kama hajatamka kwa ufasaha. Rudia kwa ufasaha kile alichotamka mtoto wako.
  • Rahisisha mazungumzo yako. Tumia sentensi fupi na zingatia maneno muhimu unapozungumza na mwanao. Hii itamsaidia kuzingatia taarifa muhimu.
  • Zima sauti nyingine zisizohitajika kama vile televisheni na redio. Hii itamsaidia mtoto kukusikiliza kwa umakini unapozungumza naye. Mtoto anapata tabu zaidi kuliko mtu mzima anaposikia kelele.

Nawezaje kumfundisha mtoto kuzungumza kwa kufurahia?
Ni rahisi kupata motisha kwa kufanya kitu unachofurahia. Hivyo utakavyoweza kuzungumza kwa kufurahi na mwanao, hii itamsaidia mtoto kutumia maneno kuweza kujielezea.

Kaa chini sakafu na cheza na mwanao. Muache achague mdoli au mchezo na uzungumze kile anachokifanya. Kwa kujumuika katika michezo na mwanao utampa nafasi nyingi za kumsikia kile anachozungumza kwa mifano sahihi.

Uwe na muda wa kumuigizia mdoli wake anayempenda zaidi kwa vitendo. Mchanganye mdoli wake katika shughuli za kila siku. Mkalishe mdoli wake mezani kwa ajili ya chai na uanze kuzungumza naye kwa kinachofanyika pale.

Angalia vitabu ukiwa na mwanao hata kama hutamsomea hadithi lakini atasikiliza na kujifunza zaidi utakapokuwa unazungumzia picha.

Furahi na mwanao kwa kuimba nyimbo za darasa la awali, kwa kuwa kadri unavyofanya hivyo ndivyo ambavyo mtoto wako atapenda kujiunga.

Cheza na mwanao michezo kwenye simu, hii itamsaidia zaidi kujifunza kuchangia katika mazungumzo.

Jaribu kusikiliza michezo kama vile:
  • Michezo ya kupiga makofi, piga kwa mtiririko maalumu kisha subiri kuona kama mtoto wako naye atafanya hivyo.
  • Chagua picha sahihi ya sanamu za wanyama na utengeneze sauti kwa mnyama mmojawapo kwa mfano “moo” kisha usubiri mwanao achukue sanamu ya ng’ombe kati ya sanamu ulizomuwekea.

USHAURI NA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
Tatizo la watoto kuchelewa kuongea ni la miaka mingi sana lakini miaka ya hivi karibuni limeonekana kuongezeka kwa kasi sana siku hadi siku.

Kuchelewa kuongea ni moja kati ya matatizo ya mawasiliano ambayo huwakuta watoto: tatizo hili hujitokeza pale ambapo watoto hushindwa kuongea kuendana na hatua ya ukuaji walioifikia. Mtoto hushindwa kuongea au kuwaelewa watu wengine wakiongea. Aidha maendeleo ya lugha kwa mtoto husimama au huenda taratibu sana.

AINA ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Zipo aina tatu za tatizo la kuchelewa kuongea kwa watoto. Aina ya kwanza ni ile ambayo mtoto hushindwa kusikiliza nini anaambiwa. Aina ya pili ni ile ambayo mtoto hushindwa kujieleza juu ya ni nini anataka. Aina ya tatu ni ile ambayo mtoto hushindwa kufanya vyote: yaani hushindwa kujielezea na kusikiliza wengine.

Kutokana na uzoefu wangu, aina ya tatu hujitokeza kwa watoto wengi zaidi, watoto wanaoshindwa kujieleza kwa kuongea pia hushindwa kujua nini wanaambiwa na watu wengine.

DALILI ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Mtoto ambaye ana tatizo hili la kuchelewa kuongea mara zote huwa nyuma ya hatua zake za maendeleo na ukuaji. Ili mzazi/mlezi aweze kujua kama mtoto wake ana tatizo hili anaweza kuangalia kama mtoto wake ana dalili zifuatazo:-

Moja, Mtoto kushindwa kupiga kelele zisizo na mpangilio mpaka kufikia miezi 15. Kelele kama “Yaaa Yaaa”, “Daaa Daaa” au “Bluuuuu Bluuuu”

Mbili, Mtoto kushindwa kuongea mpaka kufikia miaka miwili. Kuongea neno moja moja au mawili ambayo yanaweza kumpa mzazi muelekeo juu ya nini mtoto anataka kusema. Kama vile “Mama tamu” “Mama acha” au “Baba Pira”

Tatu, Mtoto kutoweza kuzungumza sentensi fupi mpaka kufikia miaka mitatu. Sentensi kama vile “Naomba maji”, “Nataka kojoa”, “Naomba maziwa”, “Nataka mpira” au “Shikamoo Baba!”

Nne, Mtoto kuwa mzito kufuata maelekezo mpaka kufikia miaka mitatu. Mtoto kutoelewa nini anaambiwa na wenginine. Kwa mfano anaambiwa: “kaa chini” na anashindwa kujua nini anatakiwa kufanya na hata akifanya mara nyingi hufanya kinyume.

Tano, Matamshi ya maneno kuwa mabaya mpaka kufikia miaka mitatu. Kwa mfano, mpaka kufikia miaka mitatu mtoto anatamka neno, Shika-chika, Sasa – chacha au Mkate – Nkate.

Sita, mtoto kushindwa kuweka maneno katika sentensi mpaka kufikia miaka mitatu. Mtoto anaweza akawa anayajua maneno mengi lakini akawa anashindwa kuyaweka maneno katika sentensi moja akielezea kile anachokitaka hivyo huishia kulisema neno moja moja tu. Kwa mfano mtoto huishia kusema: “kula” akimaanisha anataka chakula, au “piga yule” akitaka kusema yule kampiga.

SABABU ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Kutokana na uzoefu na tafiti zangu binafsi nimebaina ya kuwa zipo sababu nyingi za watoto kuwa na tatizo la kushindwa kuongea kwa wakati, kuendana na hatua na maendeleo ya ukuaji wao. Zifuatazo ni baadhi ya sababu:-

Moja, matatizo ya kusikia kwa watoto. Mtoto mwenye matatizo ya kusikia vizuri ni ngumu sana kuweza kuzungumza kwa wakati kama watoto wengine. Ni muhimu mzazi akiona mtoto wake anashindwa kufuata maelekezo na kuitumia lugha vizuri kuendana na umri wake afuatilie kama anaweza kuwa na tatizo lolote la kusikia ili aweze kupata msaada unaotakiwa mapema.

Mbili, Usonjii (Autism). Japo kuwa kuna baadhi ya watoto hawaathiriwi na autism katika maendeleo yao ya lugha lakini, kwa watoto wengi hupelekea kuchelewa kuongea. Angalau 70% ya watoto wenye Usonji huchelewa sana kuongea. Watoto wenye usonji huongea baada ya wataalamu kuwasaidia kujifunza na kutumia lugha kuendana na mahitaji yao. Ni ngumu kwa wao kuweza kujifunza kutumia lugha bila jitihada za wataalamu.

Tatu, mtoto kukosa watu wanaozungumza mara kwa mara karibu yake. Watoto huchukua lugha moja kwa moja kutoka kwa wazungumzaji wengine na ndiyo maana mtoto akiwekwa kwa watu wanaotumia lugha ya kiingereza atazungumza kiingereza, akiwekwa na wazungumzaji wa kiswahili atazungumza kiswahili n.k hivyo kwa mtoto kukosa watu karibu yake ambao huzungumza mara kwa mara humfanya ashindwe kuchukua lugha hali inayoweza kupelekea mtoto kuchelewa kuzungumza.

Nne, Wazazi kutokuwa na maarifa na hatua na maendeleo ya ukuaji wa mtoto. Sababu hii imekuwa ikipuuzwa sana na wataalamu kila wanapoelezea tatizo hili lakini binafsi nafikiri ni moja kati ya sababu kubwa kabisa. Wazazi wengi hawajui nini wafanye ili kuwapitisha watoto wao katika hatua mbalimbali za ukuaji pindi waoneshapo changamoto hali inayoweza kupelekea watoto kukwama katika matatizo bila usaidizi. Watoto wengi hushindwa kuongea mapema kwasababu wazazi wao hawana ufahamu na jinsi lugha kwa mtoto inavyojengeka na nini wafanye endapo kukitokea changamoto.

Tano, Mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake (Njiti). Mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake huweza kuleta matatizo mbalimbali likiwemo na hili la kushindwa kuongea mapema kwa mtoto. Kwani kuna baadhi ya viungo muhimu vya mwili wake vinakuwa havikumalizika kujiunda hivyo huendelea kujiunda taratibu mara baada ya kuzaliwa kwake.

Sita, Kumwacha mtoto atumie vifaa vya kielekroniki kama vile TV na simu kwa muda mrefu. Sababu hii pia haisemwi na wataalamu wengi, lakini nimeona ni moja kati ya sababu kubwa. Mtoto wa kuanzia miezi mpaka miaka mnne endapo ataachwa kwenye TV kwa muda mrefu yaana kwa zaidi ya saa moja kwa siku ni lazima itaingilia maendeleo ya ubongo. Ubongo ndiyo unafanya na kuratibu kila kitu kinachohusiana na maendeleo ya lugha kwa mtoto hivyo kwa maendeleo ya ubongo kuvamiwa na vifaa hivi vya kieletroniki vitu vingi vinavyotegemea maendeleo ya ubongo kuendelea pia husimama. Tutaliongelea hili kwa kina wakati mwingine kwani ni pana sana.

Saba, Mahusiano mabaya kati ya mtoto na mzazi/mlezi. Mtoto kuwa na mahusiano mabaya na mzazi/mlezi wake ni sababu nyingine ya mtoto kuchelewa kuongea. Mzazi/mlezi ambaye haoneshe mapenzi na ukaribu na mtoto wake au ambaye ni mkali kupitiliza kwa mtoto akiwa bado mdogo kabisa anaweza kupelekea mtoto kutotaka kuelezea hisia au mahitaji yake mapema hali inayoweza kupelekea mtoto akachelewa kuongea.

Nane, Familia kutumia lugha zaidi ya moja. Watoto wengi wanaokuwa katika familia inayotumia lugha zaidi ya moja huwa na tatizo la kuchelewa kuongea kwani watoto hulazimika kutumia nguvu ya ziada kutoa tafsiri ya baadhi ya maneno na kufananisha katika lugha zote mbili jambo ambalo huweza kuwachukua muda ukilinganisha na yule anayekua kwenye familia inayotumia lugha moja.

Tisa, Matatizo ya mdomo kama vile uzito wa ulimi. Mtoto mwenye ulimi mzito asipopewa tiba mapema tatizo hili ni lazima litamkuta kwani ulimi ni moja kati ya viungo muhimu sana kwenye uzungumzaji wa mtoto. Yapo mazoezi na jinsi ya kufanya ili mzazi aweze kulimaliza tatizo hili. Nitaligusia siku nyingine nikiwa naelezea juu ya jinsi ya kufanya ili kumaliza tatizo hili kwa watoto.

Kumi, Matatizo ya ubongo. Baadhi ya matatizo ya ubongo kama vile Majeraha kwenye ubongo yanaweza kuathiri misuli ambayo ni muhimu katika maendeleo ya lugha kwa watoto.

Hitimisho, Matatizo mengi ya maendeleo ya lugha na kuzungumza kwa watoto yanatibika kirahisi sana kama mzazi/mlezi atatafuta tiba mapema kabla ya mtoto kufikisha miaka mitano hivyo ni muhimu wazazi/walezi wakatambua mapema kuwa watoto wao wana tatizo hili na kutafuta tiba kutoka kwa wataalamu mapema.

Tuendelee kuwa pamoja nitaandika juu ya jinsi ya kupambana na tatizo hili wakati ujao. Ni rahisi tu, endapo mzazi/mlezi ukijitoa kwa moyo na kushirikiana na wataalamu.
---
Jalibu kutumia google itakusaidia kupata taarifa mbali mbali. kama hii nimeipata "www.emedicinehealth.com"
Age 8-12 Months

By age 8 months, most babies can sit up without support. They also figure out how to roll down to their stomachs and return to a sitting position again. Some babies are in constant motion; they'll arch their necks and look around while on their stomachs and grab at their feet or objects while on their backs. All this activity is preparing them for crawling, which is usually mastered between 7-10 months. Crawling is important for the development of integrated communication between the 2 sides of the brain. Some babies never crawl but rather scoot on their bottoms or move on their stomachs, like an army crawl.

Babies become increasingly more mobile during this stage; now is the time to childproof so baby can explore and discover without the possibility of injury. Baby gates are important to block off stairs or rooms that could be dangerous (such as bathrooms).

After crawling is mastered, babies begin to pull themselves up to a standing position. They then begin to take some steps while holding on to something for support. This will change into cruising around the furniture. As their balance improves, babies may gradually take a few steps without holding on. Many babies' first steps are taken around 12 months, but earlier or later than this is completely normal.

By the end of this stage, babies begin to use the pincer grasp, using the thumb and first or second finger to pick up small objects. As babies learn how to open fingers, they are able to drop and throw things. Babies also more thoroughly investigate objects by shaking them, banging them, and moving them from hand to hand. Babies are interested in objects with moving parts, such as wheels and things that open and close. They also like to poke their fingers through holes.

Babies also show a lot of growth in their language development during this period. They begin to make recognizable syllables like "ma" or "da," which eventually turn into "mama" or "dada." They can also imitate speech sounds they hear others make. By age 12 months, many babies say at least one word (other than mama and dada) clearly. They understand the meaning of no and begin to follow simple commands. Babies communicate nonverbally by pointing, crawling, or gesturing toward desired objects. The can also initiate and play gesture games, such as peek-a-boo and pat-a-cake.

Babies learn object permanence, the concept that an object still exists when taken out of their sight, during this stage. For example, if a toy is hidden under a blanket, babies will pick up the blanket and search for it. Babies also learn that objects have functions besides being just something to chew on or bang with (such as a hair brush or phone).

Separation anxiety and stranger anxiety usually begin during this period and are a normal part of babies' emotional development. Separation anxiety occurs when parents leave a babies' sight, resulting in great distress with fussing and crying. Separation anxiety usually peaks between age 9-18 months and fades before their 2-year birthday. Stranger anxiety is a reaction of distress with an infant encounters a stranger.

By the end of this period, most babies have reached the following milestones:

Motor skills

* Get in and out of a sitting position independently

* Get on hands-and-knees position and crawl

* Pull self up to standing position, walk holding on to furniture, stand without support and, eventually, take a few steps without support and begin to walk

* Use pincer grasp (thumb and first finger)

* Place objects into container and take them out of container

* Begin to do more functional activities, such as hold a spoon or turn pages in a book

Language skills

* Say "mama" and "dada" and use these terms specifically referring to a parent

* Use exclamations such as "oh-oh!"

* Try to imitate words and may say first word

* Use simple gestures, such as shaking head for "no" or waving for "bye-bye"

* Play interactive gesture games, such as pat-a-cake and peek-a-boo

Social/Emotional skills

* Easily find hidden objects

* Use objects correctly such as holding phone up to ear or drinking from a cup

* Shy around strangers

* Cry when mom or dad leaves
---
Mtoto huanza kuongea akiwa na umri wa miezi 12 hadi24, mtoto kuwa bubu huenda sambamba na kuwa kiziwi, kwani ili mtoto aweze kujifunza lugha nilazima awe na uwezo wa kusikia.

Kumtambu kwambua mtoto ambaye ni kiziwi, muweke awebize akicheza kisha mtu mmoja aweza kuja nyuma yake pasipo yeye kumuona na kumwita jina lake kwa sauti tofauti ya chini kati na juu. Akionyesha mwitikio sauti ya chini atakuwa hanatatizo, kati hanatatizo, juu anausikivu hafifu.

Hivyo hunabudi kumpeleka hosipitali kwa vipimo zaidi, na kutambua tatizo la mtoto mapema nikumsaidia mtoto kumtibu au kumpa visaidizi vya kusikia(hearing aids)ambavyo vitamwezesha kujifunza lugha mapema.
---
Ndugu yangu Rutunga mimi sio daktari ila ni baba wa watoto 6. Kati ya hao 6, wawili nimewalea mwenyewe kama single father for 6 good years hivyo uzoefu wangu utakupa mwanga kidogo.

Kuna watoto wanazaliwa wakiwa first learners na Slow learners. Dalili ya kwanza ya first learners anatumia kipindi kifupi tu cha ule usumbufu wa sleepless nights by miezi 3 ya mwanzo anakuwa aneshastabilize na kulala bila kusumbua ukiondoa ukiwa mgonjwa.

Kati ya hao watoto wawili niliowalea nikiwa single father, mmoja ni first learner huyu ni wa kike na mdogo wake ni slow learner huyu ni wa kiume.

First learners watakaa mapema by 3 months, atambaa by 6 months na kutoka meno. Atasimama by 9 months na kutembea kabla ya miezi 12. By miezi 10 anatamka baa... maa ...daa by miezi 11 anatamka kwanza dada then baba halafu mama baada ya Miezi 12.

Huyu slow leaner amechelewa kila kitu miezi 12 bado anatambaa na kuongea ameanza miezi 15-18.

Huyu binti first learner yuko faster na sharp niliwaingiza wote nursery za Montessory yule first learner baada ya mwaka anasoma anaandika na nikamwingiza Standard one at 5 years na akapeak. Huyu slow learner alimaliza mwaka mzima nursery hajui chochote yeye ni kicheza tuu!. Sister Mkuu wa Mountessory ndie aliyenipa hili somo la first learners na slow learners na kunisisitizia nisiwe na wasiwasi ni maumbile tuu!.

Hivyo Rutunga mtoto kuchelewa kuongea, kutembea au kukojoa kitandani ni suala la maumbile tuu ata catch up na kuwa ok.

Watoto hao sasa ni wakubwa, yule slow learner ndie kichwa yule first learner hakuna kitu!. Hivyo kutangulia sio kufika!.

Clinic zetu wanapima tu uzito na kukuambia kuhusu growth, mengine tumia tu wazoefu wa malezi kama hivi!.
---
Mkuu usiwe na wasiwasi ataongea tu muda ukifika--huyo hana tatizo lolote la kiufundi--ni tatizo la kimaumbile tu. Watoto wa kiume huchelewa sana kuongea. Mtoto wangu alianza kuongea akiwa na umri wa miaka 3.5. Mpaka sasa anakaribia miaka 4 lakini bado anaongea kwa kusuasua.

Kipindi hajaweza kuongea, akiwa na tatizo humshika mtu mkono na kumpeleka kwenye friji kisha kuonyesha anachotaka--maji, soda, juice, etc. Niliogopa nikadhani mwananangu ana tatizo lakini kila nikiangalia matendo namuona yupo intelligent sana.

Mtoto wako ataongea tu usiwe na wasiwasi. kuna mtu nilikutana naye akasema watoto wake wote huchelewa sana kuongea--huongea wakiwa na umri wa miaka 5. ni suala la kawaida. brain development differs from child to child. your child will speak eventually.
---
Pole sana mzazi,

Nashukuru mtoto wangu nilikuwa na spend sana muda kicheza nae na kuongea nae, wakati ana miezi 6 alikuwa anatamka baba. Akaja kupata safari ya kwenda nyumbani Zanzibar na mama yake, baada ya miezi miwili na kitu walipo rudi, ana simamia tena ana miezi 9, lakini alichekelewa kutembea moja kwa moja hadi mwaka na miezi 4, pia akawa mzito wa kuongea,lakini alikuwa na tabia hii kuna siku ana tamka da da da da da, sound ndo hio tu. Na nyengine na na na na na na, hivi sasa hivi ana mwaka na miezi 8 ndio kwanza ana tamka mama, anaongea lakini hatufahamu, tunamuitikia,

Sote ndani ni mama, hajui baba, lakini nipo nacheza nae namsemesha baba, anatamka, bado hajachanganya zaidi ya mama.

Wakati mwengine hunifuata na kinita mama, naitikia kisha anaongea, namuitikia, ananieleza jambo sijui, hii inamfanya awe na confidence.

Mtoto wangu huyu ni mwaka na miezi nane, ana Ndugu yake pia miezi nane,nimefanya hivyo haraka haraka ili apate mwenzie wa kuwa nae, nchi hizi kama ulaya, watoto wako boring sana.

Nafikiri mistake yako wewe hakuwa una spend muda na mtoto katika kumfunza kuongea, or jaribu kuwa na mtoto wako ongea cheza nae, mfundishe kutamka, kawaida mtoto mwaka anaongea, Inategemea mungu alivyo mjaalia.

Mie binafsi nilikuwa nina tatizo na kutamka maneno, hadi nafika umri wa miaka 8. Kwa mfano neno Fadhil, nilikuwa natamka adhidhi, ulimi wangu ulikuwa mzito sana, hata madenda sometimes :D:D
---
Mtoto Wa mdogo wangu alichelewa kuongea, na vile ninavyompenda jamani nikawa nahisi kulia. Siku moja mama yake akanipigia "chu..." Kaongea dah nilifurahi, alianza na neno baba akiwa na umri wa miaka 3.

Ndani ya miezi mi 3 ali develop Maneno mengi zaidi, mama, Dada, bibi etc, ila Maneno mengi alikuwa anayatamka tofauti, eg, ajiwa= majiwa, sasa= Chacha, chikamo= shikamoo, bali= wali, Dage= maharage, danga=Karanga, jaji=Maji, Chule= shule chimu=simu etc
Ndani ya miezi sita alianza kuongea sana mpaka tunashangaa, akawa anaongea kila kitu as if analipiza muda ambao hakuongea.

Mtoto alikuwa mchanganfu kila mtu akawa anatamani ambebe. Ni wa kike lakini anapendwa na jinsia ya kiume mpaka basi, kila mwanaume umsalimia chikamoo baba.😁 nadhani kwakuwa neno la kwanza kutamka lilikuwa baba ndo maana anapendwa na jinsia ya me.

Kuna kipindi alikuja kukaaa na mm, wakaka wa huku wote wakitoka kazini anawapokea getini, wote anawaita baba😀 ananiomba simu awapigie 😁 hawajui majina, ila anajua vyumba vyao, anaita baba wa kule, anawapigia simu, anawambia, " nimewamichii"😀
Wanamletea jawadi😁.

Kwa sasa anaongea utadhani anachoma taarifa ya habari, ana miaka chita, anachoma daracha la kwanja.😀😀😂
 
Naomba kujua mtoto mchanga inabidi aanze kuongea akiwa na umri gani,kwa kuzingia wale wanaowahji na wanaochelewa.Na je kuna namna unavyoweza kutambua uwezekano wa mtoto kuwa bubu na inaweza kuzulika kwa umri wake mdogo.
nitashukuu

Jalibu kutumia google itakusaidia kupata taarifa mbali mbali. kama hii nimeipata "www.emedicinehealth.com"
Age 8-12 Months

By age 8 months, most babies can sit up without support. They also figure out how to roll down to their stomachs and return to a sitting position again. Some babies are in constant motion; they'll arch their necks and look around while on their stomachs and grab at their feet or objects while on their backs. All this activity is preparing them for crawling, which is usually mastered between 7-10 months. Crawling is important for the development of integrated communication between the 2 sides of the brain. Some babies never crawl but rather scoot on their bottoms or move on their stomachs, like an army crawl.

Babies become increasingly more mobile during this stage; now is the time to childproof so baby can explore and discover without the possibility of injury. Baby gates are important to block off stairs or rooms that could be dangerous (such as bathrooms).

After crawling is mastered, babies begin to pull themselves up to a standing position. They then begin to take some steps while holding on to something for support. This will change into cruising around the furniture. As their balance improves, babies may gradually take a few steps without holding on. Many babies' first steps are taken around 12 months, but earlier or later than this is completely normal.

By the end of this stage, babies begin to use the pincer grasp, using the thumb and first or second finger to pick up small objects. As babies learn how to open fingers, they are able to drop and throw things. Babies also more thoroughly investigate objects by shaking them, banging them, and moving them from hand to hand. Babies are interested in objects with moving parts, such as wheels and things that open and close. They also like to poke their fingers through holes.

Babies also show a lot of growth in their language development during this period. They begin to make recognizable syllables like "ma" or "da," which eventually turn into "mama" or "dada." They can also imitate speech sounds they hear others make. By age 12 months, many babies say at least one word (other than mama and dada) clearly. They understand the meaning of no and begin to follow simple commands. Babies communicate nonverbally by pointing, crawling, or gesturing toward desired objects. The can also initiate and play gesture games, such as peek-a-boo and pat-a-cake.

Babies learn object permanence, the concept that an object still exists when taken out of their sight, during this stage. For example, if a toy is hidden under a blanket, babies will pick up the blanket and search for it. Babies also learn that objects have functions besides being just something to chew on or bang with (such as a hair brush or phone).

Separation anxiety and stranger anxiety usually begin during this period and are a normal part of babies' emotional development. Separation anxiety occurs when parents leave a babies' sight, resulting in great distress with fussing and crying. Separation anxiety usually peaks between age 9-18 months and fades before their 2-year birthday. Stranger anxiety is a reaction of distress with an infant encounters a stranger.

By the end of this period, most babies have reached the following milestones:

Motor skills

* Get in and out of a sitting position independently

* Get on hands-and-knees position and crawl

* Pull self up to standing position, walk holding on to furniture, stand without support and, eventually, take a few steps without support and begin to walk

* Use pincer grasp (thumb and first finger)

* Place objects into container and take them out of container

* Begin to do more functional activities, such as hold a spoon or turn pages in a book

Language skills

* Say "mama" and "dada" and use these terms specifically referring to a parent

* Use exclamations such as "oh-oh!".

* Try to imitate words and may say first word.

* Use simple gestures, such as shaking head for "no" or waving for "bye-bye".

* Play interactive gesture games, such as pat-a-cake and peek-a-boo

Social/Emotional skills

* Easily find hidden objects.

* Use objects correctly such as holding phone up to ear or drinking from a cup .

* Shy around strangers.

* Cry when mom or dad leaves
 
Mtoto huanza kuongea akiwa na umri wa miezi 12 hadi24, mtoto kuwa bubu huenda sambamba na kuwa kiziwi, kwani ili mtoto aweze kujifunza lugha nilazima awe na uwezo wa kusikia.

Kumtambu kwambua mtoto ambaye ni kiziwi, muweke awebize akicheza kisha mtu mmoja aweza kuja nyuma yake pasipo yeye kumuona na kumwita jina lake kwa sauti tofauti ya chini kati na juu. Akionyesha mwitikio sauti ya chini atakuwa hanatatizo, kati hanatatizo, juu anausikivu hafifu.

Hivyo hunabudi kumpeleka hosipitali kwa vipimo zaidi, na kutambua tatizo la mtoto mapema nikumsaidia mtoto kumtibu au kumpa visaidizi vya kusikia(hearing aids)ambavyo vitamwezesha kujifunza lugha mapema.
 
Hivi kwani watoto hua hawapelekwi kliniki for check ups? Kama wanapelekwa hua hawachunguzi vitu kama kusikia, kuona, kuongea?

Kwa wale tusiokuwa na watoto wa kupeleka Klinik hili swalii litatusaidia kujifunza pia..
Heri ya mwaka mpya Dada..
 
Naomba kujua mtoto mchanga inabidi aanze kuongea akiwa na umri gani,kwa kuzingia wale wanaowahji na wanaochelewa.Na je kuna namna unavyoweza kutambua uwezekano wa mtoto kuwa bubu na inaweza kuzulika kwa umri wake mdogo.
nitashukuu
Ndugu yangu Rutunga mimi sio daktari ila ni baba wa watoto 6. Kati ya hao 6, wawili nimewalea mwenyewe kama single father for 6 good years hivyo uzoefu wangu utakupa mwanga kidogo.

Kuna watoto wanazaliwa wakiwa first learners na Slow learners. Dalili ya kwanza ya first learners anatumia kipindi kifupi tu cha ule usumbufu wa sleepless nights by miezi 3 ya mwanzo anakuwa aneshastabilize na kulala bila kusumbua ukiondoa ukiwa mgonjwa.

Kati ya hao watoto wawili niliowalea nikiwa single father, mmoja ni first learner huyu ni wa kike na mdogo wake ni slow learner huyu ni wa kiume.

First learners watakaa mapema by 3 months, atambaa by 6 months na kutoka meno. Atasimama by 9 months na kutembea kabla ya miezi 12. By miezi 10 anatamka baa... maa ...daa by miezi 11 anatamka kwanza dada then baba halafu mama baada ya Miezi 12.

Huyu slow leaner amechelewa kila kitu miezi 12 bado anatambaa na kuongea ameanza miezi 15-18.

Huyu binti first learner yuko faster na sharp niliwaingiza wote nursery za Montessory yule first learner baada ya mwaka anasoma anaandika na nikamwingiza Standard one at 5 years na akapeak. Huyu slow learner alimaliza mwaka mzima nursery hajui chochote yeye ni kicheza tuu!. Sister Mkuu wa Mountessory ndie aliyenipa hili somo la first learners na slow learners na kunisisitizia nisiwe na wasiwasi ni maumbile tuu!.

Hivyo Rutunga mtoto kuchelewa kuongea, kutembea au kukojoa kitandani ni suala la maumbile tuu ata catch up na kuwa ok.

Watoto hao sasa ni wakubwa, yule slow learner ndie kichwa yule first learner hakuna kitu!. Hivyo kutangulia sio kufika!.

Clinic zetu wanapima tu uzito na kukuambia kuhusu growth, mengine tumia tu wazoefu wa malezi kama hivi!.
 
Hivi kwani watoto hua hawapelekwi kliniki for check ups? Kama wanapelekwa hua hawachunguzi vitu kama kusikia, kuona, kuongea?

unachosema lizzy nisahihi!ila ulemavuma wa kutokusikia kwa mtoto,wazazi au walezi wanawajibika kuhusika na kuwatambua watoto kwani ulemavu huu hutwa.silent disality.na ndipohupelekwa for more checkup.kitengo cha IT ambao ni audiologists.
 
Habari za mchana waungwana mimi nina tatizo nahitaji msaada nina mtoto kafikisha miaka minne na nusu hajatembea wala kuongea sasa sijui ana matatizo gani nahitaji msaada jamani
 
Mimi wa kwangu alichelewa kuongea kwa sababu muda mwingi alikuwa akikaa na dada wa kazi hivyo mtoto na dada hawana cha kuongea.

Pia kutembea alichelewa muda mwingi alikuwa akibebwa mgongoni na hakuwa na tatizo lolote nilichoamua kwa haraka ni kumpeleka shule akakae na watoto wenzake hiyo ndio ilinisaidia.
 
Mimi wa kwangu alichelewa kuongea kwasababu muda mwingi alikuwa aakikaa na dada wa kazi hivyo mtoto na dada hawana cha kuongea. pia kutembea alichelewa muda mwingi alikuwa akibebwa mgongoni. na hakuwa na tatizo lolote nilichoamua kwa haraka ni kumpeleka shule akakae na watoto wenzake hiyo ndio ilinisaidia.

Wa kwake mtoto ni wa 4 and a half years. Hii inabidi awaone wataalam. Maana hata umri wa chekechea tayari.
 
Naombeni msaada wenu wataalam wa afya,

mwanangu wa kiume ana miaka minne sasa but hajaanza kuongea. Napatwa na wasiwasi sana, nyimbo anaimba vizuri japo hatamki maneno yote ya nyimbo sawsawa lakini ukimsemesha hajibu but kuskia anaskia na anaelewa.

Wataalam wamempima hana tatizo lolote la ubongo yaani hata kwa shida yeyote haongei anakushika mkono na kukuonesha anachotaka.

NISAIDIEN JAMAN HIVI INAWEZEKANA AKAONGEA HATA AKIWA NA MIAKA MITANO?

Nimempeleka shule but haijasaidia
 
We subiri siku akianza kuongea utamshangaa! Mimi wangu aliongea na 3 na nusu hivi dah! La msingi mnatumia lugha gani ya mawasiliano home? As sisi tulikuwa tunaa karibu na mama so kichaga kwa sana na tukienda kazini hg kiswahili! N

ikiwa na mother house lugha ka 3 tofauti hasa tunapojifanya hatutaki watu wajue tunaongea nini. Amini dogo sasa ivi anajisemea kama cherahani kiswahili saafi baada ya kumpeleka shule ya kule kwetu?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom