Mada moto: Je, ni sahihi kumlaumu mzazi wako kwa kushindwa kukusaidia au kufanya maendeleo kipindi akiwa ana uwezo?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Inakuwaje wana JF,

Katika pitapita zangu nilikutana na huu mjadala mzito kuhusu vijana wengi kuwalaumu wazazi wao haswa baba wao wazazi kwa kushidwa kuwasaidia kipindi au kufanya maendeleo au kushidwa kuisaidia familia yake kipindi ana uwezo.

Nazungumza haya kwa sababu kuna vijana kama watatu wakizungumza mada hii mmoja alikuwa anamlaumu sana baba yake kipindi anafanya kazi alishidwa kumsaidia kumtafutia kazi wakati akiwa ana uwezo lakini amesaidia watu baki yeye mpka anastaafu watoto wake hakuna aliyeweza kumsaidia.

Kuna mwingine alikuwa anamlaumu sana baba yake mpaka anastaaafu ameshidwa hata kujenga wala kununua kiwanja anadai kipindi ana uwezo pesa alitumia sana kwenye pombe na wanawake na marafiki sasa hivi yeye mtoto ndo kamjengea nyumba ajisitiri kumfichia aibu.

Mwingine anadai mzee wake mpumbavu alikuwa amefungua kampuni yake lakini hakupenda kushirikisha familia yake na alikuwa mkali na hataki kabisa watoto zake mfike kwenye kampuni yake wala hataki mjue nini baba anafanya sasa hivi anadai amefirisika na ile kampuni ameifunga hivyo huwa anamshangaa akilalamika mara hivi mara vile .
 
Nadhani kuna mada kama hii humu, na watu walitaka kupigana ngumi kabisa.... Uzi uunganishweeeeeeeeee.
Maoni yangu lakini, lol.
 
Yeye mwenyewe kashindwa kusaidiwa na serikali ya ccm kupata elimu leo unamlaumu



Swissme
 
Yeye mwenyewe kashindwa kusaidiwa na serikali ya ccm kupata elimu leo unamlaumu



Swissme
Elimu ipi hiyooo kiongozi mwingine unamkuta na maisha mazuli lakini familia yake yupo tofauti na familia yake.
 
Wazee miyeyushoo kwanZa anakua na wivu unapopataa anataka Apatee yeye 2.....mana na mzee wangu mbka kwenye shughulii zangu ananidalalia.
 
Sio kwa jamii ya kaskazini ila naweza kuamini kwa ukanda mwingine wa Tanzania
Hahah ulidanganywa na nani?Nenda kamcheki yule mangi mzee mwenye ma bus ya Dar express anakula maisha na kimada tu Co inaelekea kufa na watoto wake wako Choka mbovu.
 
Back
Top Bottom