Mada maalumu; Sifa za madereva wa kibongo, ubovu wa miundo mbinu na utata wa matumizi ya njia

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
7,219
2,000
Wapo wanaodanganyika;
Eti kwamba ukiweza kuendesha Gari dar es salaam Tanzania basi utaweza kuendesha gari popote huko duniani (kimataifa).

Ukweli ni kwamba madereva wetu wengi bongo wakiwemo Wa magari ya serikali ni ama wamedumazwa na miundombinu isiyo rafiki! au huko vyuoni hawaelewagi wanachofundishwa au wasimamizi hawana taaluma ya barabarani!

Yapo mambo yanafikilisha kidogo nitasema machache!

A. MATUMIZI YA NJIA
Ukizunguka duniani kote barabara zinazofundishwa ni ama ;

Njia moja, njia mbili, njia nne, sita,nane na hata njia kumi na mbili.
lakini hapa kwetu bongo kuna njia 3 na njia 5
kwa hali ya kawaida matumizi ya njia yameganyika kwa maana nusu zinakwenda na nusu zinarudi ( mfano kama njia ni moja basi itaruhusu njia moja pekee, kama ni njia mbili basi moja itaruhusu kwenda nyingine kurudi,
Na endapo kuna zaidi ya hapo basi kuna tuta/ michoro huwekwa katika kuonesha njia ile inapaswa itumike na nani.
Swali, 1. Aliyeweka utaratibu Wa njia 3 Gongo LA mboto na njia 5 bagamoyo road (moroco-mwenge) alikusudia barabara moja inayobaki itumiwe na nani hususani kwa dereva mgeni?
2. madereva wanaogongana kwenye njia ya ziada wanahukumiwa na sheria gani?
B. ALAMA ZA BARABARANI
Kuanzia mwenge hadi bunju ukitembea utakutana na vibao vinavyozuia kugeuka NO U-TURN,
swali! ni maelekezo gani yaliyowekwa kwa dereva anayetaka ku kurudi(Ku U-turn) kama ataamua kuzingatia alama za barabarani? au ndo akishaingia mwenge sharti akageukie bunju?

Kwa miundombinu ya namna hii ni dereva gani bongo anaweza tia mguu kuendesha Gari barabara za kimataifa? maana wenzetu huko ukiona sehemu kibao kinaonyesha NO basi kuna sehemu kuna sema YES!
au bongo tuna alama zetu pekee?
 

mswangilishi

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
535
1,000
tuanzie sheria zetu zinaruhusu au haziruhusu? yapo mambo mengi tu yamekaa kizembe kama sheria ya zebra.
mimi kwenye zebra huwa sisimami kama hakuna watu, na hata wakiwepo huwa nawapigia honi wavuke haraka.
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
7,219
2,000
tuanzie sheria zetu zinaruhusu au haziruhusu? yapo mambo mengi tu yamekaa kizembe kama sheria ya zebra.
mimi kwenye zebra huwa sisimami kama hakuna watu, na hata wakiwepo huwa nawapigia honi wavuke haraka.
chuoni ulifundishwaje
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom