Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Kwa wamiliki wa magari engine oil ni kitu muhimu sana kwa uhai wa gari lako. Bila engine oil au ukitumia engine oil isio sahihi kwa gari lako,unaweza kuliua haraka sana au likwa linakufa taratibu bila wewe kujua,ndio unaona mara kwa mara mara hiki kimekufa mara kile hatimae inakubidi ubadili engine nzima.

Kuna aina mbili za oil[well zinazotumika sana kwa magari]:
1.mono grade eg SAE 40
2.multi grade eg 5W40

Mono Grade:
Hizi huwa zinakuwa na viscocity moja,ikipoa au ikipata moto,zinatumika sana kwa magari ya kawaida hasa toyota,kama ukiona SAE40, SAE 60 ndio hizo

Multi Grade:
Hizi zina grade mbili kulingana na joto la engine eg 5W40, 5W30,10W60 etc. Hizi zinatumiwa sana na european cars. BMW,AUDI,MERCEDES BENZ,VW,RR.DISCOVERY 3/4 etc

mfano 5W30
5 inawakilisha viscocity engine ikiwa baridi kabla haijapata moto, W inawakilisha neno 'weight' wengine wanasema winter.
30 inawakilisha viscocity engine ikishafika optimum operating temperature,ukiangalia gauge yako pale mstari wa temp unapokaa kati ndio operating temperature.

Multi grade huwa zinatumika sana kwa european cars na wameweka hivyo kusudi kwasababu ya baridi,oil inakuwa nzito sana kwahio inabidi iwe nyembamba ili iweze kuzunguka kwenye engine na ubaridi wake mpaka ikipata moto ndio inakuwa nzito inavyotakiwa na kuzunguka kwa urahisi.

Kama unamiliki euro cars nakushauri tafuta specific number kwa ajili ya gari yako. Gari nyingi zinatumia 5W30 au 5W40. Usipotumia oil sahihi utaua vitu vingi taratibu kikubwa turbo kwa gari za diesel. Na asikudanganye mtu kuwa kuna oil ya VW/BENZ/AUDI etc muhimu ni namba ya engine oil specific kwa gari fulani,halafu ndio uchague kampuni nzuri ununue hio oil.

Natumaini kuna wataalam wa lubricants humu wanaweza kuingia deep zaidi na kutupa darasa zaidi.
Umeongea vizuri lakini naomba nikurekebishe kidogo kwenye matumizi ya monograde oil mfn sae 40 kwa maelezo yako umesema oil hii ni designed kwa magari ya Toyota but ukweli ni kwamba oil hii wengi wenye magari wanaitumia kimakosa. 1 oil hii kama ilivyoandikwa ilitengenezwa mahususi kwa ajili ya matumizi ya nchi ambazo zipo kwenye hali ya joto Kali sana ambapo uzito wake utasaidia engine ya gari kufanya kazi kwa usahihi mkubwa lakini kwa kuitumia oil hii katika magari ya Toyota kwa hapa nchini unakua unaua engine taratibu hii ni kwa maana uzito wake hautwah kujichanganya mapema hasa kipindi cha asbh hadi engine itakapokuwa imepata joto na kumbuka wakati unaiwasha gari yako asbh oil hii haina uwezo wa kusambaa kwa haraka kutokana na uzito ulionao hivyo utasababisha gari yako kutembea bila oil kufanya kazi hadi pale engine inapokua imepata moto so kipind chote hicho unakua unasaga vyuma? Kiufupi na kiushauri zaidi ni kuwa kwa wamiliki wa magari wote unatakiwa kutumia oil kulingana na recommendations ya mtengenezaj na hasa kwa nchi kama Tanzania tunatakiwa kutumia oil ambayo ni multgrade oil eg 5w30 or 10w40 na hizi oil bei yake huwa zimesimama kidog kulinganisha na sae 40 hivyo wengi wa wamiliki wanazitumia sio kwa sababu ni bora kwa magari yao lahasha ni kwa sababu ni rahisi kununulika. Pia ukihitaji ushauri na maswala yote ya oil unaweza kunicheki +255719263074/+255714263074/+255762263074
 
Tairi yenye herufi W (ambayo inawakilisha uwezo wa speed wa tairi) mwisho wa speed ni ngapi?
Tairi iko hivi 215/50/R17 90W
 
Jamani ningependa kujua ni gari gani nzuri zaidi na bei yake hadi inakuwa mkononi kwa Nissani X-trail tu. Ipi bora kununua showroom au kuagiza Japani.
 
Mmh hizi gari zinahitaji handle with care
Sana mkuu, umenena vema
Nlibadilisha oil ya engine na filter halaf fundi akasahau kukaza vzr ile bolt ya kumwagia oil

Nkaanza zangu safar halaf ilikua safar ndefu kinoma wakat natembea ile bolt inafunguka taratibu mpka ikadondoka
oil ikaanza kumwagika taratibu na vile engine ilikua imeshapata moto ilivyokua inamwagikia inaunguzwa nkaanza kuona moshi kwenye mirror

Nkapak pembem kutizama duuuuh oil inamalizikia chin

Nkaita fundi kutoka dar akaja na oil pamoja na filter tukafunga upya baada ya kuachana na fundi mbele huko ikaanza kuleta mauzauza ika nock sitasahau ule usiku kwenye lile pori na mvua ilikua inanyesha na nlikua peke yng kwny gari

Nlibadilisha engine sahv nainjoi nayo maisha haina kokoro ya aina yoyote ile
 
Duu pole sana sana... Hawa mafundi wetu sometimes chenga sana... Kakutia bonge la hasara
 
Habari wakuu. Naomba kuuliza. Gari yangu haijawahi kunisumbua kwa namna yoyote. Lakini sasa kwa Mara ya kwanza imekuwa haiwaki kutokana na betri kuwa low. Naona kama ni jambo la ghafla sana kwa betri iliyokuwa nzima sana. Na hata nikibustiwa ikiwaka na kutembea umbali mrefu bado ukiizima haiwaki hadi wakubust. Je nikibadili maji inaweza kurudia uzima au ndio ninunue mpya tu. Asanteni
 
Badili betri tafadhali

Mimi nina toyota CAMI niliagiza toka Japan mwaka 2011. Binafsi niliipenda kutokana na nafasi kubwa kutoka chini au uvungu. Ulaji wa mafuta pia ni mzuri. Nikiweka full tank lt 40 natoja Dar mpaka Same ndio taa inawaka. Ulaji wake wa mafuta highway unafika lt1/km 13 barabara za mjini lt 1/km 8 hadi 9 kutegemea na uendeshaji. Siri moja juu ya ulaji wa mafuta usiweke chini ya lt 15.
Kumbe kinabugia eeeh kinaenda sawa na Impreza kwa ulaji huo
 
Back
Top Bottom