Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Watu wanashindwa kuelewa, mteja anapokuwa na ufahamu kidogo, mahusiano ya fundi na mteja ni mazuri na ya kudumu. Uzi huu umetoa fursa hiyo. Nimepata mwanga wa mambo mengi. Wadau, taa ya ABS ya V8 J100 series inawaka. Nini gonjwa?
 
Watu wanashindwa kuelewa, mteja anapokuwa na ufahamu kidogo, mahusiano ya fundi na mteja ni mazuri na ya kudumu. Uzi huu umetoa fursa hiyo. Nimepata mwanga wa mambo mengi. Wadau, taa ya ABS ya V8 J100 series inawaka. Nini gonjwa?

Gonjwa iko kwen hiyo ABS...mosi inawezekana kwamba ni false alarm kuna shoti kwen mfumo wa upelekaji wa taarifa kuroka ABS system hadi kwen computee system ya gari. Pili inawezekana kuna tatizo kiukweli hivyo kwa gari hiyo ningeshauri ufanye diagnosis ili kujua shida ilipo hasa....
 
Sawa sawa mkuu nilijua kati ya ile list nliyompa lazima atapata suluhisho...Naona.. Amina thobias atakuwa ashapata jibu

asante sana nitafuatilia hayo yote kwa maana nimejifunza kua mafundi ukiwaendea kichwa kichwa wanakuliza sana kwenye spea
 
Last edited by a moderator:
Habari zenu wadau.
Nimekuja mbele yenu ili niweze kupata msaada juu ya suala hili.
Historia iko hivi. Kuna gari aina ya toyota pickup niliinunua takriban miez minne iliyopita toka japan. Mara baada ya kununua nikaifanyia maboresho kiasi kwenye body na nikaifanyia service ya kawaida kisha nikaanza safari kuelekea Tabora. Gari hiyo ilichemsha baada ya kutoboka kidogo kwenye rejeta na ikapelekea tutembee nayo kwa kubembeleza na kuongeza maji. Tulivyofika tabora tuliziba rejeta lkn ikawa ukitembea spid inapandusha geji ya temperature. Niliipeleka gereji na tukashauriana tufunge rejeta ingine ambayo ni ya njia 3. Tukafunga lakini tatizo likaendelea. Ilibid kuangalia gasget na cylinder head. Tukakuta gasget ilipata damage na head ilipinda hivyo ilipigwa pasi na kufungwa tena. Cha ajabu gari ikazidi kuchemsha. Baada ya kuipeleka kwa wataalamu wakadai head itakuwa imeharibika zaid baada ya kupigwa pasi. Niliamua kununua head nyingine tukafunga. Pamoja na hayo yote tuliilock fen izunguke muda wote pia tulitoa thermostat lakini badala ya kuchemsha gari imekuwa ikipoteza maji kiasi cha lita moja hadi moja na nusu kwa kilometa 200. Namaanisha maji yanatoka kwenda kwenye tank la reserve na hayarud kiasi kwamba yanapotelea huko. Naomben msaada wa kiutalam tafadhali nini nifanye.
Asanten na karibuni
 
Angalia hayajichanganyi na oil? Kama sivyo jaribu kuangalia sleeves inaweza kuwa sio nzuri.
 
Embu cheki water pump mkuu unaweza kukuta ndio tatizo... alafu rudisha mrejesho hapa.
 
Hiyo gari kutoka Japan halafu muda mfupi ina matatizo hayo... Ulipoinunua ilikuwa grade gani mkuu?

Na he tatizo hilo itakuwa imekuja nalo au?
 
Kununua gari Japan sio guarantee kumbuka zinakuwa used, pia ndo maana nikaelezea historia ya tatizo kwamba rejeta ilitoboka njian ikawa safar, hivyo ili kufikia mahali walipo mafundi ilitulazimu kuiendesha kwa kuongeza maji kila baada ya umbali kadhaa.
 
wana JF wataalamu, Ndugu Mashana Jr
jamani haya mambo ya kuingiza used cars kutoka nchi za nje kweli ni shughuli si ndogo. nitashukuru ndugu ufahamisho zaidi kuhusu haya yafuatayo
1. Ati handling charges ni tofauti na delivery order?? hizi zote bill nimeletewa na clearing agent. Sasa kama sio sawa, delivery order (DO) ni yakuhusu nini? na gharama zake kwa gari dogo ni kiasi gani? Pia handling charges huwa ni kiasi gani kwa gari dogo?
2. Ati storage charges huwa ni kiasi gani kwa siku? na huwaanza lini kutozwa tangu gari lifike bandarini? Lakini si pia huwa kuna grace period, ya bure hiyo huwa ni ya siku ngapi?
3. Ati kuna gharama za ukaguzi wa TBS??? aisee huu umeanza lini na ni gharama kiasi gani.
Shukran!

Futota,ni shughuli hasa espcly issue ya kodi nyingi gari yako ikifika...japo kwa ufupi...D/O ni paper itakayoruhusu mzigo wako kuwa released kutoka kwa shipper/dealer na kuhakiki kwamba mali imefika salama,...handling charges na d/o ni tofauti kama vinavyojieleza,hata hivyo visikupe tabu agent wako atadeal navyo muhimu ujue exact price ya kila service asije akakupiga! Kuhusu handling charges TPA ndo wanahusika nayo huwa wanatoa cargo service invoice ambayo humo utaona muda wako wa neema I.e grace period 7 days kwa gari yako kukaa kwenye yard za bandari kama gari yako ni suv inarange kati ya usd 150 /250 may be itategemea ni gari gani though! ......handling charges baada ya grace period kuisha muulize agent atakuambia ni ngumu kupata exact figure ya bei hapa but it's probably more than 5,000/_ / day...Gharama za ukaguzi wa tbs zipo ilipaswa uzilipe kwa dealer huko ulikonunulia kama ni Japan tbs wanafanya certification hukohuko na kukagua various issues ikiwemo mileage na road worthiness,likifika huku halijakaguliwa possibility ya gharama kuwa juu ni kubwa ukizingatia madafu cash yetu na penalties za tbs kwa kuimport gari isiyokaguliwa! .....sina uhakika na normal charge za inspection bila shaka haivuki $80 ...japo kwa ufupi ila bei halisi muulize agent,au laah! Tinga tra,tpa upate hakikisho la exact price agents wengine njaa kali hawachelewi kukupiga za uso...nikutakie mafanikio
 
Mkuu tafuta uzi wa Mshana Jr..unahusu magari..pitia hapo kuna watu wanashare experience zao kuhusu matatizo mbalimbali yanayohusu mgari.." mada maalumu ya magari"
 
Hapa nina mashaka na mfumo wa maji,kama umesema sasa hv gari haichemshi ila maji yanapotea inawezekana kabisa mafundi wamebadilisha mfumo wa maji na ukitaka kuhakikisha hilo washa gari kwa muda fulani ukiwa umefungua boneti kwa muda then zima,kama mfumo wa maji wamebadilisha utaona maji yanatokea sehemu ya kupumulia au utasikia kabisa mngurumo wa maji kama yanamezwa vile!
 
Watu wanashindwa kuelewa, mteja anapokuwa na ufahamu kidogo, mahusiano ya fundi na mteja ni mazuri na ya kudumu. Uzi huu umetoa fursa hiyo. Nimepata mwanga wa mambo mengi. Wadau, taa ya ABS ya V8 J100 series inawaka. Nini gonjwa?
Nenda kaangalie miguu (matairi), huenda ndo kuna tatizo, kuna kidude fulan hivi kimefungwa hapo mafundi wanakijua. Chukua fundi makenika afungue tairi then fundi umeme akikague hicho kidude. Ikishindikana ndio upige diagnosis.
-
 
Passo yangu naivutaga mpaka 180 kitu imetulia hata mlio haina ila nikiiwasha asubuhi tu ndio kanatetemeka sana
 
Ndugu Mavado,
TRA nimeshalipia gharama zoote (Import duty, excise duty, vat, vehicle registration, customs and processing fees) pale exam bank.
Haya maswali yangu ni kutokana na madai nayoyapata kutoka kwa huyu clearing agent.... yaani magharama yanazidi hadi nachanganyikiwa. Naomba unijuze at least nipate msingi wa kubishana na huyo clearing agent.
Maji yamefika shingoni karibia kuzama LOL

wana JF wataalamu, Ndugu Mashana Jr
jamani haya mambo ya kuingiza used cars kutoka nchi za nje kweli ni shughuli si ndogo. nitashukuru ndugu ufahamisho zaidi kuhusu haya yafuatayo
1. Ati handling charges ni tofauti na delivery order?? hizi zote bill nimeletewa na clearing agent. Sasa kama sio sawa, delivery order (DO) ni yakuhusu nini? na gharama zake kwa gari dogo ni kiasi gani? Pia handling charges huwa ni kiasi gani kwa gari dogo?
2. Ati storage charges huwa ni kiasi gani kwa siku? na huwaanza lini kutozwa tangu gari lifike bandarini? Lakini si pia huwa kuna grace period, ya bure hiyo huwa ni ya siku ngapi?
3. Ati kuna gharama za ukaguzi wa TBS??? aisee huu umeanza lini na ni gharama kiasi gani.
Shukran!


Ndugu futota, gari Yako ukishalipia Cif, kinachofuata ni tra charges aka tax, then estimation ya kama $800 kwa ajili ya clearing and registration which Kuna chenji inabaki nyingi tuuu. For more help nipigie 0767328063 au whatssap me
 
Back
Top Bottom