Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,718
Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.

Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.

Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake

Karibuni sana

Ushauri: Jinsi ya kununua gari iliotumika ndani ya Tanzania


Tahadhari kali kwa nyote mlio na magari binafsi; chunga sana na waambie wengine!

USHAURI: Ununuaji wa magari...

View attachment 225786
 
Wapendwa wana JF
Nimekuwa Napata shida barabarani kutoka kwa washirika wenzangu wa barabara hivyo naomba kukumbusha mambo yafuatayo
Angalizo: MATUMIZI MABAYA YA INDIKETA (KUWASHA WAKATI UMESHA FIKA ENEO LA KUPINDA AU KUTOKUWASHA KABISA) Ni chanzo kikubwa cha ajali za barabarani

1. Washa indiketa unapotaka kutoka barabarani au kuruhusu gari lipite angalau meta 100 kabla ya kutoka. Kuwasha Indiketa wakati umesha fika eneo la kupinda ni makosa makubwa kwani waweza kuleta ajali. Ukiwa huna hakika na mahali pa kuingilia, washa indiketa mapema huku ukibana upande wa kushoto kama unapinda kushoto au kusogea katikati kama unapinda kulia ila hili litategemea pia na upana wa barabara, kama bara nyembamba bana kushoto

2. Ukiona mwenzako ana ovateki, usimfuate/ kuunganisha hadi ujiridhishe kuwa ni salama. Kufuata gari linalo overtake bila wewe mwenyewe kuona mbele husababisha ajali kwani yawezekana yule wa mbele yako amepima akaona atamaliza kuovertake sasa wewe wa nyuma yake ukimfuata shauri yako; AJALI!

3. Kuwasha indiketa sio kibali cha kukuruhusu upite/ kupinda kulia, ila ni ishara kuwa unataka kupinda, hivyo ukishawasha, sharti uangalie nyuma (side mirror) na mbele, kujiridhisha kuwa ni salama kabla ya kupinda.

4. Usikimbize gari mahali ambako huoni umbali mrefu/ kwenye Bonde au Kona, kwani huwezi jua nini unaweza kukutana nacho huko (wanyama, gari imeharibika nk) - Waalimu wa udereva huita kuendesha kwa kupiga ramli (yaani unajiamisha kuwa huko mbele ni salama, wakati hupaoni)

5. Mkiwa mnafuatana (magari mawili) mwenzako akasimama, usipite kabla ya kujua kwa nini amesimama. Yawezekana amesimama ili mtu/mzee/mlemavu avuke au hata kuna kitu cha hatari mbele!

6. Kuendesha chini ya KM 50 kwa saa highway, ni kumalizia watu mafuta kwani sana sana unatumia gia #2. Lakini pia haikuepushii ajali bali ni kuwapa usumbufu watumia barabara wenzako; cha msingi ni kufuata sheria na taratibu za barabarani

7. Kumbuka; kumbiza gari sio chanzo cha msingi cha kuleta ajali; Kinacholeta ajali ni kutokujua sheria au kutozifuata sheria na alama za barabarani zinazokuruhusu wapi ukimbize na wapi uende polepole. Hakikisha unajifunza taratibu/sheria za barabarani NA KUZIFUATA

8. Usiongee na simu lakini pia usipige sana stori au Kusikiliza radio/mahubiri kwenye radio wakati hujazoea kwani ukinogewa unaweza kujisahau na kukwangua/kukwanguliwa

9. Ukiegesha gari/ ukisimamisha gari, hakikisha umetoa gari nje ya barabara na sio unaacha nusu ya gari barabarani; hii ni hatari lakini pia kuwapa usumbufu watumia barabara wengine

10. Ukipaki gari barabarani, hakikisha ni salama kabla ya kufungua Mlango. Hii ni jukumu lako kuangalia usalama wako na uliowapakia hasa kama mlango unafungukia kulia (upande wa barabarani).
Kumbuka kuna bodaboda au hata gari zinazoweza kugonga mtu anayeshuka kwa urahisi

Nawasilisha!!!
 
UMEWAHI KUKAMATWA NA POLISI BARABARANI?

Je, umewahi kukamatwa na polisi wakati ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?
zijue haki na wajibu wako !

Bila kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani kutakuwa na vurugu katika barabara zetu.

Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za Barabara ; iwapo kila mmoja atazifuata sote tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama zaidi.

Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao, isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.

Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati gani anakusimamisha uwapo barabarani.

Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako; kama atakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani ; pia anaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).

Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari ; anaweza kukataa fotokopi ; hata hivyo, unaweza kuamua kupeleka leseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa. Ili kuepuka matatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).

Hati ya usajili:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili; gari lazima liendane na maelezo ya kwenye kibandiko, lakini vitu vidogo kama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).

Leseni ya barabarani, na bima ya gari:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani na kibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).

Kunyang'anywa:
Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.

Mikanda ya kiti ya usalama:
Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) ; unatenda kosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.

Kuendesha baada ya kunywa pombe:
Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi cha pombe kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatia ya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).

Kutumia simu ya mkononi wakati unaendesha:
Ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la "kuendesha kwa uzembe" (RTA, s.42, s. 50).

Mwendo kasi:
Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) ; ofisa wa polisi anaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).

Kustahili kuwepo barabarani:
Ofisa WA polisi ana haki ya kukagua Kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri ;unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.

KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA: Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwa ofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezo kwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini ; kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda Na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).

KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIA YOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisi anakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishi kwa Ofisa Msimamizi Mkuu; ambaye atachunguza na kujibu.

Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu;usitoe rushwa na usipokee rushwa.
Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na kuyaweka kwenye gari lako; lakini kumbuka kwamba ni mwongozo tu.
 
Kwa wamiliki wa magari engine oil ni kitu muhimu sana kwa uhai wa gari lako. Bila engine oil au ukitumia engine oil isio sahihi kwa gari lako,unaweza kuliua haraka sana au likwa linakufa taratibu bila wewe kujua,ndio unaona mara kwa mara mara hiki kimekufa mara kile hatimae inakubidi ubadili engine nzima.

Kuna aina mbili za oil[well zinazotumika sana kwa magari]:
1.mono grade eg SAE 40
2.multi grade eg 5W40

Mono Grade:
Hizi huwa zinakuwa na viscocity moja,ikipoa au ikipata moto,zinatumika sana kwa magari ya kawaida hasa toyota,kama ukiona SAE40, SAE 60 ndio hizo

Multi Grade:
Hizi zina grade mbili kulingana na joto la engine eg 5W40, 5W30,10W60 etc. Hizi zinatumiwa sana na european cars. BMW,AUDI,MERCEDES BENZ,VW,RR.DISCOVERY 3/4 etc

mfano 5W30
5 inawakilisha viscocity engine ikiwa baridi kabla haijapata moto, W inawakilisha neno 'weight' wengine wanasema winter.
30 inawakilisha viscocity engine ikishafika optimum operating temperature,ukiangalia gauge yako pale mstari wa temp unapokaa kati ndio operating temperature.

Multi grade huwa zinatumika sana kwa european cars na wameweka hivyo kusudi kwasababu ya baridi,oil inakuwa nzito sana kwahio inabidi iwe nyembamba ili iweze kuzunguka kwenye engine na ubaridi wake mpaka ikipata moto ndio inakuwa nzito inavyotakiwa na kuzunguka kwa urahisi.

Kama unamiliki euro cars nakushauri tafuta specific number kwa ajili ya gari yako. Gari nyingi zinatumia 5W30 au 5W40. Usipotumia oil sahihi utaua vitu vingi taratibu kikubwa turbo kwa gari za diesel. Na asikudanganye mtu kuwa kuna oil ya VW/BENZ/AUDI etc muhimu ni namba ya engine oil specific kwa gari fulani,halafu ndio uchague kampuni nzuri ununue hio oil.

Natumaini kuna wataalam wa lubricants humu wanaweza kuingia deep zaidi na kutupa darasa zaidi.
 
UFAHAMU KWA WENYE MAGARI;
Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne (4) tu toka yatengenezwe (sio toka uyafunge kwenye gari yako).

Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (2603) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne.

Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. kwa mfano 2603 inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au 2699 inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999.

KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE.
Pia kila tairi limeandikwa uwezo wa spidi yake ukikimbiza zaidi ya uwezo wake itapasuka na hizo spidi zimeandikwa kwa herufi kama ifuatavyo
CODE SPIDI
F=============80
G=============90
J==============100
K==============110
L==============120
M==============130
N==============140
P==============150
Q==============160
R==============170
S==============180
T==============190
H==============200
Huandikwa hivi
280/R/70/13/150/S

Tairi.jpg
1423537507090.jpg
1423537539087.jpg
1423537594187.jpg
 
Umefanya vyema mshana jr pia naamini maudhui ya Kiswahili kuhusu magari yapo, tutenge muda kuyapata au kutengeneza....

Haina shida hayo nimepakua mojamoja tukifika kwenye manunuzi bima na ufundi itakuwa kwa kikwetu
 
Last edited by a moderator:
kuna jamaa yangu alikuwa na gari rav4 ina engene ya D4 ilimzingua akaamua kubadili na kuweka engene ya 3S, gari imekataa kukaa silance tatizo linaweza kuwa nini na afanyeje manake hiyo gari hata kuuzika imegoma.
 
leo tulisimamishwa na askari wale wanaokaaga kwenye mataa na kukagua magari ilikuwa ni mitaa ya mjini,alikagua leseni, kisha akahamia kutaka kuonyeshwa risiti ya mzigo tuloubeba, kiukwel hakuwa mzigo useme tumetoka kuununua ,ilikuwa ni vitu vidogo sana vya kwenda kurekebisha mahali palipoharibika tulivyovitoa katika store yetu wenyewe.

Baada ya askari kutuelewesha sana tulimuelewa kuwa chochote unachokitoa labda ubungo kukipeleka labda posta inakubid uwe na risit hata kama unakitoa kwenye store yako mwenyewe.
 
67 Reactions
Reply
Back
Top Bottom