Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

IMG-20211005-WA0137.jpg
 
TABIA 30 HATARISHI ZA WAENDESHA PIKIPIKI(BODABODA)
Ndugu Msomaji
Leo tumekuletea orodha za waendesha pikipiki ambazo ni hatari kwao au kwa watu wengine barabarani. Tabia hizi kama zisipoisha ajali zitaendelea kutokea. Tabia hizi hazina mkubwa wala mdogo, si askari si raia, hivyo Kila anayeendesha pikipiki aangalie tabia yake ni ipi kisha akate shauri kujirekebisha kwa kuachana nayo.
1. kuovateki kushoto
2. kupita kushoto na kulia mwa gari kwa wakati mmoja
3. kuacha indiketa ikiwaka hata baada ya kukata kona
4. kubeba abiria juu ya mizigo
5. Kupuuza indiketa ya gari lililoko mbele kwa kupinda kwanza kabla ya gari
6. kubeba abiria zaidi ya mmoja (mishkaki)
7. kuendesha kwa kukaa upande (tako moja)
8. kutoa side mirror
9. kudhani honi ndio breki
10. kutokuwa na bima ya chombo
11. kutovaa helmeti
12. kuendesha kwa spidi kubwa barabara za mitaani
13. kupiga muziki kwa sauti kubwa wakati anaendesha
14. kuendesha katika leni ya katikati muda wote
15. kugeuza (u-turn) njia kuu kwa ghafla na bila tahadhari pale akiona abiria
16. kuwa na haraka kila wakati
17. kuchomekea
18. kuendesha huku ameweka tege miguu yake na huku amevaa kandambili
19. kutosimama kwenye zebra
20. kutosimama kwenye taa nyekundu
21. kupita pembeni ya matuta kukwepa matuta
22. kupita kwa kasi kwenye njia maalumu kwa waenda kwa miguu
23. kupita njia zilizozuiwa kuingia (no entry)
24. kuvuka kwenye zebra huku akiendesha pikipiki
25. kuendesha piki piki huku wakiwa na kilevi mwilini
26. kupakia abiria au mizigo juu ya tenki la mafuta
27. mwenda kwa miguuu akimtazama usoni tu atajua ni abiria hivyo atamfuata kwa kasi bila kujali usalama wake
28. kuovateki kwenye mzunguko (round about)
29. kuonesha indiketa anakwenda kushoto kumbe anapinda kulia
30. Daima kuamini kwamba wao wanaonewa hata pale ambapo wao au mmoja wao ndio chanzo cha ajali.

Ewe dereva bodaboda, chukua tahadhari unapoendesha barabarani-mwili sio gari kwamba una spea.

RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote
 
Mkuu Mshana Jr Mshana jr: naomba uziwako wa matumizi ya chumvi ya mawe
 
Back
Top Bottom