Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

IMG-20210219-WA0124.jpg
IMG-20210219-WA0123.jpg
 
Habarini wana jumuiya kubwa ya JamiiForums,

Ni wakati sasa wa kuwa na mada yetu maalum kwa kaliba hii kubwa na pana yenye dhamana adhimu ya kuhakikisha tunasafiri na kufika tuendako salama iwe:
  • Makazini
  • Kwenye starehe
  • Kwenye dharura
  • Kutembeleana nknk
Ni kaliba hii adhimu pia yenye dhamana kubwa ya kufikisha salama mizigo na vifurushi vyetu vyote vya kibiashara, kikazi nknk

Mada hii maalum ni jumuishi ya:
  • Madereva wa magari makubwa na madogo ya mizigo
  • Madereva wa boda to boda
  • Madereva wa magari yote ya abiria
  • Madereva wa viongozi, matajiri na watu maarufu
  • Madereva wa mitambo
  • Madereva bajaj bodaboda wote kwa ujumla wao
  • Na mwisho kabisa madereva wa magari binafsi
Mada hii ni maalum pia ya kusimuliana changamoto mbalimbali za barabarani kuanzia vibali, uendeshaji mbovu, ushirikina, maafisa usalama, mamlaka zenye dhima na usafiri nk.

Kuna ishu ya uzoefu pia ambayo tunaweza kushirikishana hapa ili kupata uzoefu incase likitokea la kutokea ujue jinsi ya kukabiliana nalo

Hakuna mahali hapakosi vituko na vibweka. Kwenye hii kaliba pana ya usafiri vipo vya kutosha. Je, una kituko chochote? Huu ni uwanja wako sasa.

La mwisho lakini ambalo si la mwisho kabisa ni swala zima la kupeana connection. Madereva wazoefu na wazuri ni wengi mno lakini shida inakuja kwenye ajira. Kupitia mada hii nina HAKIKA TUNAWEZA KUPEANA SHAVU LA AJIRA

Ni mada pana na yenye ulingo mpana sana. Kuna mengi ambayo sijaandika hapa. Naomba ushiriki wenu kwa yale niliyosahau.

Dondoo baadhi za uzoefu wangu kwenye udereva
  • Nidhamu barabarani huepusha ajali nyingi
  • Barabarani derava hapaswi kuwa na maamuzi mawili kwa wakati mmoja
  • Muda wote ni dereva anapokuwa kwenye usukani ni lazima macho yake yaone sekunde 15 mbele toka alipo
  • Inapotokea dharura ya pancha si vema kufunga breki ghafla
  • Muhimu muda wote kusoma taa za tahadhari kwenye dashboard
Tutazidi kushirikina mengi kadiri mada itakavyokuwa inaendeleea, na hata kama kuna links za kazi za udereva tutapeana hapa
Nitangulie kuwatakia maandalizi mema ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kwa madereva wenzangu tuna DHIMA kubwa ya kuzivusha salama mwaka huu roho za mamilioni ambazo ni ndugu jamaa marafiki na wanadamu wenzetu.

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Mkuu Mshana Jr kuna hii connection ya madereva ambao wanaweza kufika hapo Soga Kibaha leo au kesho waende fasta. (See the attachment)
Walio karibu wachangamkie fursa hiyo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2021-02-25 at 10.52.01.jpeg
    WhatsApp Image 2021-02-25 at 10.52.01.jpeg
    40.2 KB · Views: 31
 
New force,kitongo iyo
Ilipiga chini ila haijaua,alichomekewa wakati wa ku overtake
 
Mwaka 2010 niliwahi kuwa boda boda "pikpik" kwa mkataba wa mr mmoja hiv mkubwa serkalin upande wa policy!,,, siku moja nikakamatwa beria kwa makosa ya
kutokuwa na lesen,bima na motor vehicle, baada ya kukamatwa nilimjulisha tajil tajil akampa agzo mkuu wa kituo wa eneo husika nililokamatwa ocs,,ocs nae kampigia alie nikamata kampa agzo aniachie mara moja wakat huo nami nasikia akimpa agzo, kuna boda boda hapo namb flani ndio,naomba uiachie mara moja tusike leta balaa aise dk tano muachie hyo mtu fast!, asikal alonikamata kakataa anamjib boss wake afande mie siwez muachia maana kavunja sheria na taratb ko hapana duu!,,nilikaa ka dk 10 hiv boss wang kapiga simu vip wamekuachia?.. hapana mpk saiv boss kapiga tena kwa ocs!,, kama dk 5 hiv ocs kafika beria na usafili wake wa gx100 akawaita maafande wote wakapanga mstali misr ya gwaride ,, akaanza kumuhoji jamaa alie nikamata,,,
ocs,, nimekupa agzo la kuiachia hii pikpik mbona mpk sasa hujaiachia umefanya mpk nimeacha kaz zingne kukufuata ww kwa nn?
afande,,amevunja sheria afande hivyo nilitaka alipe fain afande,,,
ocs,, mi na ww nani kiongoz anaetowa maagzo?...
afande,,, ni ww afande!.
ocs,, nan inchaj wako?..
afande,, ni ww afande!..
ocs,, kwa hyo tuna bishana mi na ww sio una taka tuoneshane ubabe?..
afande,, hapana afande, nisamehe afande nimekosea,,
ocs,, goja nikuonyeshe kidogo ili ujuwe kuwa mm na ww nan mkubwa,,
afande wote,, walikuwa 7 wakapiga salut wakasema msamehe afande hataludia kukiuka maagazo yako afande,,
ocs,, usifikilia kushindana na mm ninapotoa maagzo kwan unajua hiyo pikipik ni ya nan,!?.. anafoka ocs hapo
afande wote,,, salut msamehe afande!..

Wakat huo mie nipo pemben naona kila kitu na kusikia hahahaha ocs akasepa,, jamaa akanilushia funguo kwa hasira na kunifukuza nisonekane pale hahahaha,, kwakuwa ilikuwa njia yang ya nenda lud nilikuwa nalud mara nying nying ko wakiniona tu nakuja!! wana sema yulee muzush mfunguli gat apite,, hahaha mwisho wa siku nikawa rafiki zao sana!,, sikusumbuliwa tena hahahahaha,,enz za jk hizo daa!..
 
Back
Top Bottom