Mada ITV: Hali ya Elimu nchini, Nini kifanyike ili kujibu mahitaji ya wakati?

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Kwenu,

Hii ni mada iliyochochewa na kauli ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kwamba kuwe na mjadala kuhusu Elimu ili kuinusuru.

Kati ya walioko mezani ni waalimu Dr. Kalaghe na Prof. Rwaitama.
Prof Rwaitama;
Wakati wa Mwalimu kulikuwa na falsafa iliyoongoza elimu ambayo ni Elimu ya Kujitegemea. Elimu ya msingi ilikuwa lazima na ilitolewa bure, ukiikosa unapata Elimu ya Watu wazima.

Matatizo ya elimu yetu yako katika maeneo matatu,
Mitaala
Ushindani
Usimamizi na kugharimia Elimu.

Kwa sasa hakuna mtaala rasmi. Kila mwalimu anatumia kitabu chake. Mitaala inabadilishwa bila kushirikisha wadau na ikibadilika vitabu havipatikani au havipatikani kwa wakati. Walimu hawapati semina za kuwanoa.
Kila Waziri wa Elimu anafanya mabadiliko ya kimfumo kwa kutoa hiki na kuingiza kile bila sababu za msingi.

Imethibitika kuwa wanafunzi wetu wanaomaliza vyuoni hawana uwezo wa kushindana na wenzao wa nchi jirani au wa nje. Wahitimu hawawezi kujiajiri kwa kuwa wamefundishwa kuajiriwa. Waajiri wanabainisha kuwa vyuo havizalishi wahitimu kulingana na mahitaji ya soko.
Wahitimu wa vyuo hawawezi kujieleza.

Mwalimu ana msururu wa mabosi, kuanzia Mratibu Elimu Kata hadi Mkuu wa Mkoa.Walimu hawakaguliwi, hawapewi stahiki kwa wakati.
Walimu wetu si mahiri. Wanatokana na waliofeli kidato cha nne.
Muda wa ku-train walimu umepunguzwa toka miaka minne hadi miaka mitatu. Hii imepunguza au kuondoa muda wa mazoezi kwa vitendo kwa walimu na hata wakipata muda wa mazoezi hakuna wasimamizi wenye taaluma inayoendana na masomo yanayofanyiwa mazoezi.

Dr.Kahyarara,
Ripoti ya World Bank ilionesha kuwa 20% ya walimu waliopimwa hawakupata 80% ya alama ambayo ndiyo ilikuwa minimum. Vilevile walimu wanatumia nusu tu ya muda unaotakiwa kutumika.

Ili kupambana na changamoto za elimu tunatakiwa kutenga 20% ya bajeti kwenye elimu. Bajeti ya elimu imeshuka hadi 15% mwaka 2017,toka 16% mwaka 2016,toka 17% mwaka 2015.

Toka Serikali itangaze kufuta michango primary na secondary, wazazi wameacha kuchangia chakula. Kufuta michango kumeongeza idadi ya wanaojiunga na shule.

Somo la TEHAMA halifundishiki kwenye mazingira ya shule zetu. Linahitaji vitendo, hakuna umeme wala walimu wenye ujuzi.

Hizi ni baadhi ya dondoo.
Karibuni.
 
Unmeshindwa kuelewa ....

2015. 17%

2016. 16%

2017. 15%

Elimu bure lakini budget inapunguzwa badala iongezwe Mara dufu. Kweli Africa kuendelea Kazi kubwa sana
 
Hoja yako ni nzuri kwa sehemu lakini ngoja nikwambie kitu, binafsi nimefundisha shule za serikali kwa miaka kumi alafu nikaenda kufundisha shule za watu binafsi ambapo nipo mpaka sasa.

Tatizo kubwa si walimu ni mfumo wa elimu ndio tatizo mfano form two akifeli kwenye shule binafsi haruhusiwi kuendelea anapaswa arudia. kwenu mfumo unasema anarudia alafu akifeli tena anatakiwa aendelee.
 
Hoja yako ni nzuri kwa sehemu lakini ngoja nikwambie kitu, binafsi nimefundisha shule za serikali kwa miaka kumi alafu nikaenda kufundisha shule za watu binafsi ambapo nipo mpaka sasa.

Tatizo kubwa si walimu ni mfumo wa elimu ndio tatizo two anarudia. kwenu mfumo unasema anarudia alafu akifeli tena anatakiwa aendelee.
Walimu wakichangia italeta picha halisi. Ahsante mkuu.
 
Elimu itakapojitenga na wanasiasa, hakika yote yatakuwa neema kwa nchi. Kitendo cha kuiweka elimu mikononi mwa wafanyabiashara na ushindani usiyo katika usawa ni tatizo.
 
Ukweli ni kwamba ELIMU BORA NI GHARAMA, na kila mara tumeambiwa, a bure ghali!!!
Hatujawa serious kuwekeza kwenye elimu, hatuwezi kuwa na elimu bora katika mazingira ambayo haki za walimu zinaminywa, wanakaa kazini mpaka miaka 8 anatumikia mshahara alioanza nao kazi!
Yaani mwalimu anamfundisha mwanafunzi, mwanafunzi huyo anafikia hatua ya kusomea ualimu, anaenda kuanza kazi, anamkuta mwalimu wake mwenye miaka 8 au 10 kazini, but anapokea mshahara sawa na mwanfunzi wake!
Na wahusika wako busy hawana hata habari!
Na watanzania tulivyo wazembe na wavivu wa kufikiri, eti unaambiwa wa kwako ansoma bure, lakini anayekwambia mtoto wako asome bure yeye wa kwake anamlipia milioni kadhaa!!
Tafakari!!!
 
Wanasiasa wengi utasikia nilikuwa mwalimu sasa wote wanakimbia na kudharau ila wanachojadili bungeni aibu tu ndio maana BUNGE LIVE NO ila vitu visivyo vya msingi live
 
Kick these shites out of the high office!
IMG_20180316_200112.jpg
 

Attachments

  • IMG_20180316_200112.jpg
    IMG_20180316_200112.jpg
    123.3 KB · Views: 21
Unmeshindwa kuelewa ....

2015. 17%

2016. 16%

2017. 15%

Elimu bure lakini budget inapunguzwa badala iongezwe Mara dufu. Kweli Africa kuendelea Kazi kubwa sana
Niliskia kuna shule ilipokea elf 8 mia 5 kama gawio ...
 
Hili suala halihitaji mjadala,ni political will tu hamna.Ni KUFUMUA tu mfumo wote wa elimu na kuusuka upya.Lakini kwa mwendo huu wa 'kujaribujaribu' ,tutatangatanga nyikani dahari nyingi tu.
 
Back
Top Bottom