MADA FIKIRISHI: Achana na Konde Boy, baharia mkuu kashitukia mchezo wote...

Kisiwa Cha Harishi

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2019
Messages
1,020
Points
2,000

Kisiwa Cha Harishi

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2019
1,020 2,000
Binamu. Kuna mistari yake flani kwenye ngoma ya ‘Bado Nipo Nipo’. Anakuambia: “Alilala na bibi harusi, siku moja kabla ya harusi, bado mnanishauri harusi? Hamuwezi kuwa hamjalewa.” Wakati anatoa hii ngoma, alikuwa baharia mwenzetu. Hivi sasa mchizi kakata kamba kambini. Si baharia tena.

Ilikuwa 2012. Kampeni za jimbo la Arumeru Mashariki, enzi za ‘Dogo Janja’ Nassar. Ilikuwa Jumamosi mida flan ya jioni mitaa ya Sakina pale Arusha. Bar moja maridadi sana. Karibu Dar nzima ilikuwa Arusha. Kila bar baada ya bar unakutana na washikaji wa Kino, Mwenge, Tabata, Sinza na maeneo mengine.

Niko na baharia mwenzangu tukila biere. Yeye alikuwa na ‘pisi’ moja ya hatari. Ilikuwa imeenda hewani kama Irene Uwoya vile. Rangi yake kama ya ukwaju wa Bhakressa lakini yeye muivishe kidogo. Ukweli ni kwamba hakufanana na wanawake waliokuwepo pale bar. Alikuwa wa pekee haswa mwenye upekee wa pekee.

Ugeni wangu ulifanya nikose uwezo wa kukamatia fursa za uzao wa Eva. Nikitegemea hisani ya wenyeji au muujiza kama wa Daudi kwa Goliath. Lakini uwepo wa ile ‘pisi’ ya mshikaji ulinifanya nisiwe mnyonge. Kwa maana uzuri wake ulifubaza wasichana wote pale na kuwaona kama vituko. Labda angekuja aliye na ubora kama wake au zaidi.

Kumtazama ilikuwa burudani kuliko ‘kumkisi’ Hamisa Mobetto. Akinyanyua glasi kupeleka mdomoni, alivutia kuliko tendo la kumvua ‘brauzi’ mkali mwingine yeyote. Meza zote macho yalikuwa kwetu, kisa yeye. Hata madem wenzake walichosha shingo zao kumtazama aendapo ‘toilet’ na kurudi. Acha kabisa.

Ni aina ya warembo ambao huonekana mara moja maishani kwa binadamu wa mlo mmoja kwa siku. Kuna maeneo ngumu kumkuta hata bahati mbaya. Maana kuna warembo hutosikia ana ndugu Mabibo Jeshini, Akachube Road Kijitonyama au Kwa Sokota. Urembo unamtenga na eneo korofi na kumuweka eneo tengefu.

Tayari vyombo vilishampanda kichwani. Wakati wasichana wengi wakikolea kinywaji sura inakosa nuru. Huyu kinywaji kilizidi kumtakasa na kujenga umalaika flan usoni kwake na kuvutia zaidi. Kitendo cha gambe kumfanya ainuke kila wakati kwenda msalani, kilitoa nafasi kwa mshikaji kunisimulia mengi. Noma sana.

Kumbe ni mali ya mtu lakini mshikaji ndiye baharial wake. Na mwenye mali siyo mburula kama huyu baharia. Ni kidume mwenye ukwasi chekwa akiwa na makazi yake Dar. Mke anafanya nini Arusha? Kamfuata baharia wake ambaye ndo huyu niliyekuwa naye bar. Kaagaje kwa mume? Anaenda kusalimia wazazi wake wanaoishi Njiro. Huyu mrembo wazazi wake wapo Arusha. Kwa hiyo ‘akimisi shoo’ za baharia wake anaaga kwa mumewe kuwa anakwenda kuwaona wazazi. Hata kwa mwezi kwenda Arusha mara mbili kwake si kesi. Pesa ipo ya ndege JNIA to Kia. Si Ngorika au Abood. Anaweza kwenda asubuhi akapewa shoo jioni akageuza.

Tajiri huwa ‘bize’ na hesabu kuliko amri ya sita. Choka mbaya ndo wenye ‘stress’ na mke, hujiita mabaharia, mabingwa wa kuzikopa totoz. Nas wanapiga shoo ndefu ili kufidia ‘gepu’ kubwa la kutoa mtonyo. Hapa ni mabaharia wanaonielewa, kwamba wanajituma ili wasiombwe au wapewe pesa.

Si watu wazuri. Matukio yao yamemfikia hadi Baba la Baba pale Ikulu ya Magogoni. Juzi kati kawachana, kuwa wanavizia majimama yenye mtonyo. Ili wasukume mzigo na ndinga zao watambe nazo kitaa. Hapa tofautisheni baharia na marioo. Mabaharia si mabwege kama marioo. Baharia anatafuna mwili na pesa kisha anasepa. Marioo anaweza asipewe chochote zaidi ya kulala bure. Akaishia kuosha vyombo na kutunza watoto. Mabaharia hawana muda wa kuweka kambi eneo moja kama Suma JKT. Kama wafugaji wanasepa na kijiji kusaka malisho na wao kwao popote kambi.

Ndo kama baharia niliyekuwa naye Arusha na yule mbebezi. Anaishi Arusha, lakini totoz ndo inakwea pipa kumfuata baharia wake. Anakwenda na pesa za mumewe anazitafuna na baharia wake. Na zingine anamuachia akiondoka, na baharia anazitumia kwa kutafunia ‘pisi’ zingine za mtaani.
Kwa tabia za mabaharia zilivyo. Naamini hawajasikia neno la Baba la Baba toka Ikulu ya Magogoni. Kama unajijua wewe ni baharia tambua kuwa Mzee anajua nyendo zenu na sifa zenu za kibwege. Baharia mzuri ni yule mchakarikaji siyo unavizia pesa za mke wa mtu. Au za mwanamke mhangaikaji ili wewe ndo upendeze.

Na kwa uzuzu wa mabaharia wengi. Hawajui kuwa kauli ya Rais ni agizo na sheria kwa wakati mmoja na amri kwa upande mmoja. Ina maana polisi akigundua ubaharia wako ni kuvizia majimama yenye fedha ili ule, uvae na utembee lazima atakudaka. Fanyeni kazi hiyo mnayoifanya ni starehe si kazi. Endelea kutanua mabega kama umemwagiwa maji ya baridi mgongoni. Ukijisifu kuwa wewe baharia wakati wana tunajua kuwa wewe ni mtakatishaji fedha za majimama. Lazima wanao tukuchome kibingwa kwa mwela ukatulizwe selo. Mzee anataka tufanye kazi si starehe hizo. Shitukeni mabaharia.

Achana na Konde Boy. Yule si boya kutaka kutemana na WCB. Ana akili zake si kama za mabaharia wetu. Pamoja na kwamba dem wake Sara ana mkwanja mrefu. Lakini hamtegemei ili kuendesha maisha. Kwa tabia za mabaharia wetu Konde Boy, angeshaachana na WCB na muziki wenyewe ili atumie pesa za Sara.

Lakini dogo kakomaa na muziki wake. Na sasa anataka kutemana na WCB ili ule mgao wa kwenda WCB, abaki nao wote. Huyo baharia katumwa pesa mjini. Ila wale wa kutamani fedha na ndinga za majimama mmekwisha. Mzee baba kishatonywa huko kuwa mpo wengi mnaotafuta fedha kwa starehe ya ngono zembe kibaharia. Kuna andiko nilisoma bila kujua aliyeandika. Jamaa ana akili nyingi sana. Siyo vibaya tukaambiana kwa kifupi kupitia andiko hilo. Kwamba ukiwa na miaka 40, waliosoma na wasiosoma wanakuwa sawa. Si ajabu mwenye elimu ndogo, akatengeneza fedha nyingi kuliko mwenye elimu kubwa.

Ukifika miaka 50, mrembo na asiye mrembo pia wanaanza kuwa sawa. Ni wakati wa mikunjo usoni, vipara na mvi. Hivi havikwepeki tena. Ukifika miaka 60, aliyekuwa na cheo na asiyenacho wanakuwa sawa tu. Wote wastaafu na wanakuwa washikaji. Kukaa na kupiga stori za kufanana.
Miaka 70, mwenye nyumba ndogo na kubwa. Wote huhitaji nafasi ndogo ya kukaa, kipindi hiki kuhamisha vitu inakuwa taabu. Mwenye ghorofa atapenda kukaa nyumba ya chini. Kwa miaka 80, wenye fedha na wasionazo hawachekani. Hawana pa kwenda kutumia wala kutafuta. Hubaki nyumbani tu.

Ukifika umri wa miaka 90, kulala na kutolala ni sawa tu. Kwa kuwa hata ukiwa macho huna cha kufanya. Baada ya miaka 90, masikini na tajiri, wote wanasubiri kifo tu. Kwa muda huu ulionao fanya mambo kulingana na nafasi na wakati wako. Katika maisha hakuna mtu muhimu kuliko watu wengine.

Kwa sababu ya elimu yako, uzuri wako, nafasi yako kazini, nyumba yako kubwa na nzuri unayoishi, fedha au kipato chako kuwa kikubwa. Basi ulikuwa hujui tu, ila wewe ni wa kawaida sana, hakuna mtu mwenye nafasi kubwa kuliko mwingine. Ni suala la muda tu, hivyo tuishi kwa adabu.

Mabaharia zingatieni haya maandiko. Mafujo yenu yamemgusa mpaka raia namba moko. Siyo jambo dogo ni suala la muda wote tutakuwa sawa. Usishangae leo hii Harmonize kutamani ajitegemee wakati miaka michache nyuma alitamani kushikwa mkono tu na Diamond.
Ni suala la wakati mabaharia.

Credit: Mwananchi
 
Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Messages
11,208
Points
2,000

Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2017
11,208 2,000
hahahaha,kuna movie ya kizungu kajamaa kalikua kabaharia kanaishi huko hollywood kwenye mijengo ya maana na hakana elimu wala kazi,kameanza ubaharia utotoni kalimla mwalimu wake wa primary
 
beckaflavour

New Member
Joined
Sep 26, 2019
Messages
4
Points
45

beckaflavour

New Member
Joined Sep 26, 2019
4 45
Binamu. Kuna mistari yake flani kwenye ngoma ya ‘Bado Nipo Nipo’. Anakuambia: “Alilala na bibi harusi, siku moja kabla ya harusi, bado mnanishauri harusi? Hamuwezi kuwa hamjalewa.” Wakati anatoa hii ngoma, alikuwa baharia mwenzetu. Hivi sasa mchizi kakata kamba kambini. Si baharia tena.
Ilikuwa 2012. Kampeni za jimbo la Arumeru Mashariki, enzi za ‘Dogo Janja’ Nassar. Ilikuwa Jumamosi mida flan ya jioni mitaa ya Sakina pale Arusha. Bar moja maridadi sana. Karibu Dar nzima ilikuwa Arusha. Kila bar baada ya bar unakutana na washikaji wa Kino, Mwenge, Tabata, Sinza na maeneo mengine.
Niko na baharia mwenzangu tukila biere. Yeye alikuwa na ‘pisi’ moja ya hatari. Ilikuwa imeenda hewani kama Irene Uwoya vile. Rangi yake kama ya ukwaju wa Bhakressa lakini yeye muivishe kidogo. Ukweli ni kwamba hakufanana na wanawake waliokuwepo pale bar. Alikuwa wa pekee haswa mwenye upekee wa pekee.
Ugeni wangu ulifanya nikose uwezo wa kukamatia fursa za uzao wa Eva. Nikitegemea hisani ya wenyeji au muujiza kama wa Daudi kwa Goliath. Lakini uwepo wa ile ‘pisi’ ya mshikaji ulinifanya nisiwe mnyonge. Kwa maana uzuri wake ulifubaza wasichana wote pale na kuwaona kama vituko. Labda angekuja aliye na ubora kama wake au zaidi.
Kumtazama ilikuwa burudani kuliko ‘kumkisi’ Hamisa Mobetto. Akinyanyua glasi kupeleka mdomoni, alivutia kuliko tendo la kumvua ‘brauzi’ mkali mwingine yeyote. Meza zote macho yalikuwa kwetu, kisa yeye. Hata madem wenzake walichosha shingo zao kumtazama aendapo ‘toilet’ na kurudi. Acha kabisa.
Ni aina ya warembo ambao huonekana mara moja maishani kwa binadamu wa mlo mmoja kwa siku. Kuna maeneo ngumu kumkuta hata bahati mbaya. Maana kuna warembo hutosikia ana ndugu Mabibo Jeshini, Akachube Road Kijitonyama au Kwa Sokota. Urembo unamtenga na eneo korofi na kumuweka eneo tengefu.
Tayari vyombo vilishampanda kichwani. Wakati wasichana wengi wakikolea kinywaji sura inakosa nuru. Huyu kinywaji kilizidi kumtakasa na kujenga umalaika flan usoni kwake na kuvutia zaidi. Kitendo cha gambe kumfanya ainuke kila wakati kwenda msalani, kilitoa nafasi kwa mshikaji kunisimulia mengi. Noma sana.
Kumbe ni mali ya mtu lakini mshikaji ndiye baharia wake. Na mwenye mali siyo mburula kama huyu baharia. Ni kidume mwenye ukwasi chekwa akiwa na makazi yake Dar. Mke anafanya nini Arusha? Kamfuata baharia wake ambaye ndo huyu niliyekuwa naye bar. Kaagaje kwa mume? Anaenda kusalimia wazazi wake wanaoishi Njiro. Huyu mrembo wazazi wake wapo Arusha. Kwa hiyo ‘akimisi shoo’ za baharia wake anaaga kwa mumewe kuwa anakwenda kuwaona wazazi. Hata kwa mwezi kwenda Arusha mara mbili kwake si kesi. Pesa ipo ya ndege JNIA to Kia. Si Ngorika au Abood. Anaweza kwenda asubuhi akapewa shoo jioni akageuza.
Tajiri huwa ‘bize’ na hesabu kuliko amri ya sita. Choka mbaya ndo wenye ‘stress’ na mke, hujiita mabaharia, mabingwa wa kuzikopa totoz. Na wanapiga shoo ndefu ili kufidia ‘gepu’ kubwa la kutoa mtonyo. Hapa ni mabaharia wanaonielewa, kwamba wanajituma ili wasiombwe au wapewe pesa.
Si watu wazuri. Matukio yao yamemfikia hadi Baba la Baba pale Ikulu ya Magogoni. Juzi kati kawachana, kuwa wanavizia majimama yenye mtonyo. Ili wasukume mzigo na ndinga zao watambe nazo kitaa. Hapa tofautisheni baharia na marioo. Mabaharia si mabwege kama marioo. Baharia anatafuna mwili na pesa kisha anasepa. Marioo anaweza asipewe chochote zaidi ya kulala bure. Akaishia kuosha vyombo na kutunza watoto. Mabaharia hawana muda wa kuweka kambi eneo moja kama Suma JKT. Kama wafugaji wanasepa na kijiji kusaka malisho na wao kwao popote kambi.
Ndo kama baharia niliyekuwa naye Arusha na yule mbebezi. Anaishi Arusha, lakini totoz ndo inakwea pipa kumfuata baharia wake. Anakwenda na pesa za mumewe anazitafuna na baharia wake. Na zingine anamuachia akiondoka, na baharia anazitumia kwa kutafunia ‘pisi’ zingine za mtaani.
Kwa tabia za mabaharia zilivyo. Naamini hawajasikia neno la Baba la Baba toka Ikulu ya Magogoni. Kama unajijua wewe ni baharia tambua kuwa Mzee anajua nyendo zenu na sifa zenu za kibwege. Baharia mzuri ni yule mchakarikaji siyo unavizia pesa za mke wa mtu. Au za mwanamke mhangaikaji ili wewe ndo upendeze.
Na kwa uzuzu wa mabaharia wengi. Hawajui kuwa kauli ya Rais ni agizo na sheria kwa wakati mmoja na amri kwa upande mmoja. Ina maana polisi akigundua ubaharia wako ni kuvizia majimama yenye fedha ili ule, uvae na utembee lazima atakudaka. Fanyeni kazi hiyo mnayoifanya ni starehe si kazi. Endelea kutanua mabega kama umemwagiwa maji ya baridi mgongoni. Ukijisifu kuwa wewe baharia wakati wana tunajua kuwa wewe ni mtakatishaji fedha za majimama. Lazima wanao tukuchome kibingwa kwa mwela ukatulizwe selo. Mzee anataka tufanye kazi si starehe hizo. Shitukeni mabaharia.
Achana na Konde Boy. Yule si boya kutaka kutemana na WCB. Ana akili zake si kama za mabaharia wetu. Pamoja na kwamba dem wake Sara ana mkwanja mrefu. Lakini hamtegemei ili kuendesha maisha. Kwa tabia za mabaharia wetu Konde Boy, angeshaachana na WCB na muziki wenyewe ili atumie pesa za Sara.
Lakini dogo kakomaa na muziki wake. Na sasa anataka kutemana na WCB ili ule mgao wa kwenda WCB, abaki nao wote. Huyo baharia katumwa pesa mjini. Ila wale wa kutamani fedha na ndinga za majimama mmekwisha. Mzee baba kishatonywa huko kuwa mpo wengi mnaotafuta fedha kwa starehe ya ngono zembe kibaharia. Kuna andiko nilisoma bila kujua aliyeandika. Jamaa ana akili nyingi sana. Siyo vibaya tukaambiana kwa kifupi kupitia andiko hilo. Kwamba ukiwa na miaka 40, waliosoma na wasiosoma wanakuwa sawa. Si ajabu mwenye elimu ndogo, akatengeneza fedha nyingi kuliko mwenye elimu kubwa.
Ukifika miaka 50, mrembo na asiye mrembo pia wanaanza kuwa sawa. Ni wakati wa mikunjo usoni, vipara na mvi. Hivi havikwepeki tena. Ukifika miaka 60, aliyekuwa na cheo na asiyenacho wanakuwa sawa tu. Wote wastaafu na wanakuwa washikaji. Kukaa na kupiga stori za kufanana.
Miaka 70, mwenye nyumba ndogo na kubwa. Wote huhitaji nafasi ndogo ya kukaa, kipindi hiki kuhamisha vitu inakuwa taabu. Mwenye ghorofa atapenda kukaa nyumba ya chini. Kwa miaka 80, wenye fedha na wasionazo hawachekani. Hawana pa kwenda kutumia wala kutafuta. Hubaki nyumbani tu.
Ukifika umri wa miaka 90, kulala na kutolala ni sawa tu. Kwa kuwa hata ukiwa macho huna cha kufanya. Baada ya miaka 90, masikini na tajiri, wote wanasubiri kifo tu. Kwa muda huu ulionao fanya mambo kulingana na nafasi na wakati wako. Katika maisha hakuna mtu muhimu kuliko watu wengine.
Kwa sababu ya elimu yako, uzuri wako, nafasi yako kazini, nyumba yako kubwa na nzuri unayoishi, fedha au kipato chako kuwa kikubwa. Basi ulikuwa hujui tu, ila wewe ni wa kawaida sana, hakuna mtu mwenye nafasi kubwa kuliko mwingine. Ni suala la muda tu, hivyo tuishi kwa adabu.
Mabaharia zingatieni haya maandiko. Mafujo yenu yamemgusa mpaka raia namba moko. Siyo jambo dogo ni suala la muda wote tutakuwa sawa. Usishangae leo hii Harmonize kutamani ajitegemee wakati miaka michache nyuma alitamani kushikwa mkono tu na Diamond.
Ni suala la wakati mabaharia.

Credit: Mwananchi
baharia tumekupata
 
secret file

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Messages
965
Points
1,000

secret file

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2019
965 1,000
Aisee tungo tata....
mimi nimedaka hapo kufikia 50yrs
demu/mwanamke mzuri na mbaya wanakuwa sawa......
Kufikia 90 tajiiri na masikini hawachekani...
nimekamata sana hapo
 
Forum statistics

Threads 1,382,576
Members 526,405
Posts 33,831,813
Top