HERY HERNHO
Member
- Mar 4, 2022
- 70
- 313
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini China ambako pamoja na mengineyo analenga kulishawishi taifa hilo mshirika wa Urusi, kusaidia juhudi za kuleta amani katika mzozo wa Ukraine.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aidha anataraji kuirai China kuacha kuisaidia Urusi kwa silaha. Macron yuko China wakati rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa nchini Poland kwa ziara rasmi ya kikazi kwa mshirika wake huyo ambaye amesaidia pakubwa kuyahamasisha mataifa ya magharibi kumsaidia jirani yake kijeshi na hata kisiasa.
Rais Emmanuel Macron amesema mapema leo akiwa Beijing kwamba taifa hilo lina nafasi kubwa ya kufungua njia ya kupatikana kwa amani nchini Ukraine kutokana na uhusiano wa karibu uliopo kati yake na Urusi, ingawa ameonya kwamba Urusi haipaswi kupewa fursa ya kuwa na majadiliano ya kina na taifa hilo. Amesema hayo katika hotuba yake ya kwanza tangu alipowasili China kwa ajili ya ziara hiyo, alipokutana na raia wa Ufaransa, katika mji mkuu Beijing. Amesema Ufaransa inaweza pia kuwa sehemu ya jukumu hilo la kupatikana kwa amani na utulivu.
"Vita hivi ambavyo nimekuwa nikivieleza mara kwa mara kuwa ni vya kibeberu na kikoloni, vimekiuka misingi mingi ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Hivyo China, haswa kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu na Urusi, ambao umethibitishwa tena katika siku za hivi karibuni, inaweza kuwa na jukumu
Na taarifa kutoka Berlin zinasema kaimu kansela wa Ujerumani Robert Habeck kwa mara nyingine amelikumbusha taifa hilo kujua ukomo wake katika kuisaidia Ukraine, akionya halipaswi kuwa sehemu ya mzozo. Amesema hayo kabla ya kurejea nyumbani akitokea Kyiv alikokuwa kwa ziara ya siku mbili.