Maclassmate: Unatumia kigezo kipi kubadilishana namba na Classmate wako?

Habari wakuu,

Nimekuwa nakutana na watu wengi niliosoma nao na kupiga stori kadhaa lakini cha ajabu hakuna anayemuomba mwenzie namba ya simu.(hana nadhani kila mmoja anamwangalia mwenzie kuwa huyu tukibadilishana namba tutaongea nini? hivyo hakuna haja)

Kuna mmoja tulibadilishana , lakini hakuna aliyewahi kumtafuta mwenzie ila njiani tunaonana na kusalimiana kama kawaida.

Je vigezo vipi unatumia vinavyokufanya huyu kuna umuhimu wa kupeana namba na huyu hakuna?
Itakuw wote mnaringa, wote mnajiona bora kuliko mwenzake, wote wanafiki, chukua namba wasiliana nao siyo kipindi cha harusi mnatafutana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama huna hela, huna kazi hun mbele wala nyuma lazima uyachukie makundi ya wasap ya shule ama kuona ulio soma nao ni kero.

pia kama wamekuzidi elimu, yaani unajihisi wewe huna thamani wala si kwamba hamna cha kuongea ila ile kujiona u duni kati yao.

kwangu mimi sikua mtu wa stori na mtu tangu shule, ila makundi ya wasap nipo na tukionana tunazungumza sema napata ugumu kwa wadada walio olewa

ugumu mwingine ni kwa watu wanao jihisi duni (wakijilinganisha) na wenzao
 
Itakuw wote mnaringa, wote mnajiona bora kuliko mwenzake, wote wanafiki, chukua namba wasiliana nao siyo kipindi cha harusi mnatafutana

Sent using Jamii Forums mobile app
Wako na matatizo lukuki hao sie wengine tunao kuanzia primary mpaka mwisho wa masomo!isitoshe kwa wasie wa town tunajuana sana huyu olympio pale kisutu yule forodhani huyu hapa muhimbili halafu mnakutana azania tambaza shaban robert mzizima mkitoka hapo wale wale mnakutana tena high school vyuo mnaachaje kubadilishana namba?
Wale wakuja kytoka nyaminywili ndio wataona tabu maana wakimaliza primary kijijini wanakuja mji huu secondry wanaenda mji mwingine high school kwa bahati ndio mtakutana chuo huyo unadhani atawasiliana na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Primary classmate 7 yrs together, in std Vi &Vii same desk. Tunakaa mtaa mmoja tunakutana almost kila weekend.
Tulikujakutana chuo, lakini hakuna mwenye story tukutanapo zaidi ya salamu za kinafiki. Sasa hivi tunakutana ktk mishemishe njiani bado hakuna mwenyestory....mtu kama huyu hutakiwi kubadilishana naye namba koz hauna mazungumzo naye yyte

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Usipotoa number watasema unaringa, na ukitoa hakuna story. Nionavyo mimi kila mtu ana personalty yake, ila wengi wanapenda kushindana. Mlivyoshindana darasani nani awe wa kwanza wanadhani kwenye maisha nako kuko hivyo. Kila mtu anataka aonekane yuko juu ya mwenziye au awe juu kweli. Lakini faida yake nini? Hushindani na mtu kwenye maisha, bali unashindana na changamoto zilizoko kwenye maisha, na ukizimaliza sasa unaanza kutafuta ziada, ndio sasa tuna tafuta vile vizuri zaidi, maana umeshapata vya kwaida sasa unataka ku show off. lakini kwanini msiwe kama zamani mpigiane simu muulizane mawili matatu na muelezane namna gani mnaweza kusaidiana. Lakini wengi hawataki, sio kwamba hana lakusema lakini unawezakuta anaogopa jamaa atanionaje, nimechoka au mi mjinga sana, hili linafanya mnakosa story.
Nashauri wewe fungua mazungumzo na hao mnaobadirishana number, muulize, muongee labda itamfanya awe free nawe kasha mtaanza kuongea tena. Uki mute naye iki mute, maana ya kubadirishana number inapotea. Kiingereza wanasema "Silent is a relationship killer" sijui kama nimepatia, lakini nadhani nimeeleweweka.
Binafsi nilikuwa mtundu sana, lakini sasa nimekuwa utundu nimeacha. Kuna wanaodhani mimi bado niko kama zamani, na wananiogopa, na kunawengine hiyo ni njia yakukumbushana yazamani, utasikia wewe jamaa ulikuwa mkorofi sana Enzi zile, basi tuna cheka tuanaanza story zingine. Usiogope kukumbushwa ya zamani, yaone ni mapito, na kumbuka wewe unaishi sasa sio zamani. Na labda ulikuwa mjinga darasani, lakini maishani umefanikiwa, usitake ku prove chochote kwa yeyote hayo ni maisha yako na nimajaliwa yako. Na kama ulikuwa unaakili sana lakini sasa maisha yamekupiga pia ona ni challenge kuwaona ulio wazidi grade darasani wamekuzidi kimaisha, ukikubali yote hayo utaongea nakila class mate wako. Aliyesoma sana, ambao hawakusoma kabisa, waliofanikiwa na ambao hawakufanikiwa.
 
Hadi sasa sijaona haja ya namba ya classmate. Ninazo hapa kibao ila tunawasiliana kwa uchache sana tena sana kiasi naweza kusema ni kama hatuwasiliani tu na hata hivyo mnavyowasiliana kuna ugumu sana wa "kuconnect". Uelekeo wa maisha wa kila mmoja umebadilika sana kila mmoja ana changamoto tofauti sana za kimaisha na ikiwa ni wa jinsia tofauti ndio sahau kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inategemea classmate wa level gani na ulisoma wapi... wa secondary ndio haohao mnaendelea nao wengine hadi Uni.. Wengine ndio ma colleague makazini..
Namba unakuwa nazo za wale mnaokutana..Adhawaiz unajaza fonbuku tu
 
Wakaniingiza kwenye group la O Level,nikawa mchangiaji mkubwa. Nikaona ipo haja ya kujua wemzangu mpo wapi na shughuli zenu. Mimi nikaweka details zangu,hakuna aliyeendelea kabisa. Baada ya week nikajitoa
 
Mimi maclassmate wangu wengi wanamiliki Nyumba,Magari na Kazi nzuri na asilimia kubwa wameshadaka Shahada zao za Uzamili.Naogopa kuchukua contact zao ukizingatia enzi hizo nilikuwa nawakimbiza kila paper.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom