Machungu Yetu Leo Kama Taifa na Nimkumbukavyo Mwl Nyerere Jana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machungu Yetu Leo Kama Taifa na Nimkumbukavyo Mwl Nyerere Jana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Jan 20, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MIAKA 20 NAKUMBUKA KAULI TASA YA BABA WA TAIFA JUU YA MHE KIKWETE; "TUMUACHE BADO AKUE KIDOGO"

  Huko nyuma, nilivyokuwa mtoto nilidanganyika sana eti mtu ukianguka basi utakuja kuokota hela sehemu ulikoangukia lakini leo nimegundua pindi utakaporudi tu pale ulipoangukia kwa mapema kidogo sana sana unachoweza kukiokota ni kipande cha ngozi ya mwili wako kilichoanza kuoza tayari.

  Ukweli huu nauona hata sasa katika siasa ya nchi yetu ya Tanzania na kwa masikitiko makubwa sana!! Ila tu kinachonifariji ni hali tulionayo kama taifa iliotekwa na jopo la MAFISADI kwa kila idara ya maisha yetu kweli ni NGUMU SANA KULISEMEA BASI lakini kwa pamoja na uwezo wa Mwenyezi Mungu INAWEZEKANA KABISA KUAGANA NALO MILELE!!!

  Mwanzoni kabisa huko nyuma 2005 nilidanganyika nikidhania atamranda Julius Kambarage Nyerere nikampa kura zote na kuwashawishi wenzangu zaidi ya 50 kufanya hivyo kumbe hovyo kabisa!!

  Hata pale 1995 aliposhindwa na Ndg Benjamin Mkapa mwenzenu nilimkasirika na kusononeka sana lakini kwa kuwa ilikua ni Baba wa taifa Mwalimu Nyerere basi ikabidi nibaki tu kugugumiagugumia bila njia nyingine.

  Baada ya miaka hii zaidi ya 20 NAKUMBUKA MANENO YA Mwl Nyerere na kujikuta nikijitukana kila siku ndani kwangu na wala hasira hazipungui.

  UFISADI niliubariki mwenyewe kwa kura yangu 2005 lakini kwa 2010 nimelazimishwa tu kwa ujanja wa UCHAKACHUAJI - kwanini lakini???

  Si kipindi kirefu nitajitokeza hadharani kwenda kuwaomba radhi wale Watanzania wenzangu niliowashawishi KUFADHILI HUU UFISADI.

  Mzee Mkapa nakuomba sana radhi leo hii; sikuwahi kukupenda kuingia kwako uongozinini kama asingelikua Mwalimu Nyerere.

  Namuomba Mama Maria radhi kwa niaba ya Marehemu Mwalimu Nyerere kwamba kama vijana wadogo sana wa taifa hili ujumbe katika lugha yake ya Ki-Staha zaidi ulikua mzito mno masikioni mwetu ila leo tunaloona ni ule usemi wa 'Majuto ni Mjukuu' Baba wa Taifa.

  Naomba pia radhi watu waliokuona unafaa badala ya Mhe Kikwete!! Masikini kumbe mzee wa watu alikua anajua watoto wake wote na tabia zao ndani ya cha cha mapinduzi. Loooooo!!!!!!!!!!!!!

  Nasema nitawaomba radhi mbele ya hadhara tena bila ya aibu kwa kura zao nilizipotezesha mimi.

  Mwalimu Nyerere kusema "TUMUACHE BADO AKUWE KIDOGO" kumbe mzee wetu alitufunika ujumbe zito ajabu hivi!!!!!!!!!!!!

  Hivi sasa kama taifa ndio tunaelekezwa wapi na kulazimishwa kulipa mafisadi wasiojulika hata kwa mmoja wetu! Kwa ujanja ujanja huu Watanzania tumeshapoteza kwakiwango gani mikononi mwa viongozi wabadhirifu na kutaendelea nao kupoteza hadi lini???

  Jamani kumbe acheni wale wanaovaa mi-bomu wakati mwingine wavae na kuteketeza ukoo wote wa mafisadi na unyama wao wote kwa jamii yatu, ka!! Kumbe usimkemee mvaa bomu kabla haujasikia machungu yako moyoni!!!!

  HOJA YANGU:

  Ndani ya CCM kama bado kumebaki mtu anayefikiria kuwa ni mtetezi wa maslahi ya taifa hili basi MJIUZULU MARA MOJA PINDI TU ITHIBITISHWAPO kwamba kweli Dowans na Mafisadi wengine wanalipwa.

  Mrudi majimboni na kutuuiliza cha kusema katika vikao vyenu na kule bungeni hapo Mwezi Februari. Mbunge yeyote atakayekiuka agizo hili la 'Nguvu ya Umma' asije lalamika baadaye!!

   
 2. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mazuri yanalindwa kwa nguvu zetu zote wananchi na kidogo kutoka kwa viongozi wetu.
  Mabaya yanalindwa kwa nguvu zetu wananchi na nguvu nyingi za Viongozi wetu na Mbwana zao toka kila pembe ya dunia.
  Sisi wananchi tukiacha kuyalinda Mabaya kamwe hayawezi kusimama.
  Viongozi pekee yao hawana ujanja wa kukumbatia mabaya na kutu tweza
  Ni pale tujaapo matamanio yaliyo uzao wa mabaya ndipo tulindapo mabaya kwa nguvu zetu.

  Wazee wetu walipigania uhuru, mkoloni alijaribu kuwahonga vyeo na pesa wakataa katakata.
  Leo hii tunadhani Matamanio ya fedha,vyeo na vilemba vya ukoka yanamvuto kuliko uzalendo?!
  Ni mpka tupigane na kuishinda tamaa ndani ya nafsi zetu ndipo tutakapo shinda vita ya tamaa ya maovu.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi ambavyo CCM haionyeshi kutusikiliza wala kushtuka juu ya lolote lile, na wananchi tukizidi kupuuzwa, kukataliwa maelezo ya msingi juu ya kodi zetu zinavyotumika na sasa kuua raia kwa visingizio kede kede, naona huku tupelekwako ni kuangamia kwa taifa letu pamoja na utaifa pia!!!

  Hatua za dharura na za makusudi kukataa kuburuzwa zaidi ndio hivyo haizuiliki tena. Hapo nyuma kidogo tuliwauliza viongozi wetu kujipima kubaki madarakani au kuwajibika mauaji ya Arusha lakini naona wote wameziba masikio kabisa

  Tukawambia wasilipe Dowans sasa kila dalili ni kwamba Dowans inalipwa na kodi zetu tupende tusipende. Tumewaambia CCM waache kabisa tabia ya kutuchezea kamari ya kutupambanisha Wakristo kwa Waislamu kiudini hata kwa mambo ambayo yako wazi kabisa, lakini nani wa kutusikiliza kwa kuwa uchaguzi ulishapita????

  Nasema mpaka hapa hapana tena kusukumwa zaidi!!!!!!
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama kweli wazee wetu wangeamua kufiri kupia mitumbo yao na kufanya maamu ya kitaifa kulingana na mahitaji ya familia zao au dini zao hadi leo hii Watanzania tungekua wapi na umoja wetu wa kitaifa huu tuliouzoea???
   
 5. B

  Bull JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ya leo ni bora kuliko ya wakati wa Nyerere kwa sababu zifuatazo;

  Uchumi unakuwa kuliko wakati wa Nyerere

  Freedom of expression

  Shule na University zimeongezeka

  Budgeti tegemezi wakati wa Nyerere ilikuwa zaidi ya 49%

  Kodi ya vicha

  Biashara ni ulanguzi

  Corrupt leaders hakuwai kushtakiwa au kumpeleka mahakamni yoyote

  Kikundi kidogo cha dini fulani ndio waliokuwa viongozi na kujinufahisha


  na mengineyo......
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ina maana kwamba takwimu zinapoonyesha uchumi unavyokua mfukoni mwake Rostam Aziz, Jakaya Kikwete na Edward Lowassa basi tayari Watanzania wote wanaposhiba na kusaza hawa MAFISADI na sisi huku tayari tumeshiba tu si ndivyo waalimu wako wa Uchumi walivyokufundisha eeehhh??
   
 7. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  @uwezo tunao!mbona hukuwa namba moja kwenye maandamono ya arusha??kama kweli nkmnazi wa upinzani ningetegemea thread zenye breaking news ungekuwa wewe wakwanza kuzitoa wakati tukiangaika kuuliza huko Arusha nini kinaendelea sikuwahi kusikia au kuona thread yenye breaking news!!iweje hapa unahamasisha ujinga??amani ikitoweka hakuna wakuirudisha si upinzani wala cha tawala!!hivyo nibora ukaeleza ulivyo mjua JK Nyerere,na JK Mrisho!mapungufu niyakila mmoja tatizo tulilonalo nikatiba siyo myu binafsi!!Soma katiba utajua kwanini nchi iko hapa tulipo! Mwisho Mod's futeni hii thread kwani ni yakichochezi!!!
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  crap.
   
 9. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [/B]
  Mwalimu Nyerere kusema "TUMUACHE BADO AKUWE KIDOGO" kumbe mzee wetu alitufunika ujumbe zito ajabu hivi!!!!!!!!!!!!

  Hivi sasa kama taifa ndio tunaelekezwa wapi na kulazimishwa kulipa mafisadi wasiojulika hata kwa mmoja wetu! Kwa ujanja ujanja huu Watanzania tumeshapoteza kwakiwango gani mikononi mwa viongozi wabadhirifu na kutaendelea nao kupoteza hadi lini???
  [/COLOR]

  [/QUOTE]

  Ila kula ka ukweli kwa madai ya huyu bwana ukichunguza hayo maneno hapo juu na hali halisi nchini!!!!!!
   
 10. B

  Bull JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nyie ndio wafuasi wachadema mkiongozwa na DJ Mbowe, wanachama walevi kama wewe na Katibu Mkuu Askofu. hamuwezi kamwe kuelewa mafanikio yaliopo tanzania zaidi ya kuhubiri chuki, udini na ukabila

  Kweli ni Takwimu gani za uchumi ambazo Mbowe(DJ), Katibu Slaa (Askofu) watazielewa ? Prof; Lipumba anajua ukweli na hawezi kuongea pumba kama maaskofu !!
   
 11. kitungi

  kitungi Senior Member

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  wewe na huyu View attachment 20958 hamtofautiani ki-mawazo!
   
 12. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MOD kama vile baadhi ya watu wameanza kuondoka kwenye mistari ya taratibu zetu kushiriki mijadala?
   
 13. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taratibu kaka, mbona mwendo kasi hivo.
   
Loading...