Machozi yanayomwagika kwaajili ya maziwa yaliyomwagika; Lema, tufanye nini?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Viwango vya ukandamizaji wa kisiasa na kijamii vimekua vikubwa zaidi katika awamu hii kuliko awamu yeyote ile katika uongozi wa Tanzania.
Niseme tu, yametosha machozi yaliyomwagika kwaajili ya maziwa yaliyomwagika!

Tunahitaji kufanya jambo!
Tufanye nini?

Wanaosota rumande ni ndugu zetu.
Wanaozunguka mahakamani kila leo ni jamaa zetu.
Walioko jela na waliopotea ni washkaji zetu.
Na waliopigwa risasi pia, wote ni ndugu, ndugu katika mapambano lakini zaidi ndugu katika maendeleo na hatuwezi kuwatupa.
Ukimya wetu ni usaliti kwao na kulalamika kwetu sio heshima stahiki kwa hao waliojitoa sadaka kupigana mstari wa mbele!

Nimesikitika kusoma eti Ndugu yetu Lema hajui tufanye nini?
Lema usifanye chochote, wewe Ongoza!
Tumia karama yako ya kuongoza utuongoze kupaza sauti na kujibu vitendo vyote vya kihuni vinavyofanywa kuinajisi demokrasia yetu.

Lazima maandamano ya kisiasa yawepo, Lazima maandamano ya kijamii yawepo!
Lazima vyama vya wafanyakazi vishiriki kupaza sauti juu ya uhujumu wanaofanyiwa.
Kwanza kabisa lazima watu wapewe ujasiri wa kufungua midomo kabla ya mikono ili baadae wawe na ujasiri wa kutumia mikono.

Haitakuwa kwa maandamano ya siku moja.
Na haitakuja bila sadaka.
Hakuna lelemama kwenye kutafuta haki!
 
Nilifikiri hapo mwisho utaweka jina lako, cheo chako, mahali ulipo na namba zako za simu ili iwe rahisi kukutafuta juu ya huu uchochezi na uchokozi unao uanza
 
Hata alietusaliti na kwenda ikulu ni ndugu yetu tufanye nini na yeye keshasifia utawala!
 
Nilifikiri hapo mwisho utaweka jina lako, cheo chako, mahali ulipo na namba zako za simu ili iwe rahisi kukutafuta juu ya huu uchochezi na uchokozi unao uanza
You are a talented fool
A gifted fool for that matter
 
Hata alietusaliti na kwenda ikulu ni ndugu yetu tufanye nini na yeye keshasifia utawala!

Uzuri Mungu amemuumba binadamu na utashi.Anajua mema na mabaya.Na kwa vile unajua mema na mabaya unajua pia dhuluma kwa utu wa binadamu ni dhambi siku moja utajibu.Yawezekana si leo wala kesho ila utajibu
 
Back
Top Bottom