Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,800
Nilimaliza S/ Msingi miaka km 20 iliyopita. Nilipofauru kuendelea na msomo sikubahatika tena kurudi kwenye kijiji hiki toka nilipomaliza hadi mwaka huu.Nimekuta baadhi ya marafiki zangu(Classmates) wameshakufa.Ilinisikitisha sn.Baada ya kupumzika km siku 1 hv niliweza kuitembelea shule na kukuta waalimu wangu wote wa enzi hizo wamestaafu baadhi wakiwa wametangulia mbele za haki.Nimeingia kwenye madarasa niliyokua nasomea miaka hiyo,nikakumbuka jinsi tulivyokua tukisoma kwa shida, kwa kuchapwa fimbo ziszo na idadi,kuwahi namba saa 12:00 asubuhi tena mm nikiwa time keeper. Nikakumbuka jinsi mtoto wa Mwl. alivyokua akinisaidia kugonga kengele pale ninapochelewa kufika shule kwani nilikua nakaa kilometa 5 kutoka shuleni hivyo kuna wakati nilikua nachelewa kuwahi . Miaka hiyo shule ilikua shule bana asikwambie mtu. Kila mwanafunzi alikua na kiunga chake cha kufanya usafi. Kulikuwa na viranja wakatili sn kuliko hata waalimu. Wao ndo walikua wanasimamia usafi na waliruhusiwa kuchapa wanafunzi wenzao.( Sijui km kishera ilikua sahihi). Kila kiunga kilikuwa kimepangwa vema na umaridadi kwa vipande vya tofali za kuchoma.Kila kiranja alikua ana eneo lake la kusimamia na baada ya usafi alikuwepo Kiranja wa usafi aliyeitwa bwana au bi afya ambaye alikagua maeneo yote na kumpa taarifa Mwl.wa Zamu.Endapo ikitokea eneo(Kiunga) fulani hakijafanyiwa usafi basi kiranja wa eneo hilo aliwajibika kwa kuchapwa fimbo za kutosha. Kiranja wa usafi sifa yake kubwa ilikua ni lazma awe msafi na nadhifu kweli kweli! Vichapo vya fimbo zsizo na idadi ilikua ni kawaida hasa kwa mazwazwa na watukutu.Unakuta mtu anapigwa fimbo 5 za kuchelewa,fimbo 5 za kukosa hesabu,5 Kiingereza na 5 za Kukosa maswali ya Sayansi bado mkaguo wa usafi n.k kwa siku mbaya mwanafunzi aliweza kuchapwa hadi fimbo 20. Wengi waliacha shule, wengi walikimbia makwao na kuamua kua wawindaji n.k. Kumaliza darasa la saba ilikua ni ushujaa. Maisha yalikua zaidi ya kambi ya jeshi. Shuleni tulikua tunalima sn mashamba hasa kipindi cha mitihani karibia na kufunga shule. Kipindi hicho tulikua tunawachukia waalimu akwambie mtu si km leo.Enzi hizo elimu ilikua haijaingiliwa na siasa. Nakumbuka tulifauru wanafunzi 3 tu hapo ni baada ya shule kukaa miaka takribani 5 hivi bila mtu kufauru. Hakukua na kubebwa wala kupanua goli.
Baada ya kukua na kumaliza elimu ya chuo kikuu nmekuja kujua kuwa waalimu hawa pamoja na ukatili wao kuna misingi fulani waliyonijengea na kunisaidia,ambayo sijawezi kuipata popote nilikopita katika maisha yangu ya elimu.Kusema ukweli nawashuru kokote waliko.
Lakini cha kusikitisha nikiwa nimekuja hapa shuleni nmestaajabu sn kukuta shule iko hoi bin taabani. Mazingira ya shule yaliyokua yanapendeza kwa maua sasa hakuna tena. Mazingira ni machafu sn. Madarasa yamechoka hakuna anaejali. Enzi hzo tulikua tuna timu za michezo mbali mbali kuanzia riadha,netball basket,volleyball, handball na football huku mm nikiwa nahodha wa timu.Cha kusikitisha nmekuta uwanja wa mpira wa miguu umeota vichaka na magoli ya chuma yaliyokuwepo wahuni wameiba. Viwanja vingine vya michezo km netball,basket ball, handball volleyball ndo huwezi jua hata km viliwahi kuwepo.Miaka hiyo shule yetu iliweza kutoa washiriki wa michezo mbali mbali hadi ngazi ya mkoa na taifa katika UMITASHUMTA.Mimi nmecheza mpira pamoja na golikipa wa zamani wa Yanga marehemu Isumail Suma ngazi ya mkoa Tabora. Inaskitisha kukuta mambo yameharibika kiasi hiki. Kila kiko vululu vululu. Sjui tunaelekea wapi na elimu ya leo,!!