Machozi ya mwanamke ni silaha kubwa, Wajinga waamuzi wetu

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Machozi ya mwanamke ni silaha ya kwanza kwake mbele ya mwanamume, Pesa ni silaha ya kwanza kwa mwanamume mbele ya mwanamke. Tatizo la Tanzania watu wenye akili na upeo mkubwa ni waoga na wanafiki wakubwa, Lakini watu wapumbavu na wajinga, ni wasemaji na wanajiamini sana.

Ni rahisi sana kuijua moja lakini ni vigumu sana kuitetea moja hiyo, Dunia haihitaji wanaoijua moja, bali wanaojua kuitetea moja hiyo. Jambo muhimu katika maisha yenye amani na furaha, usiikariri kesho wala usikariri tabia za mpenzi wako wa zamani ukaamini vyotevya fanana.

Kipimo cha ujinga wa Watanzania ni uwezo wa mijadala ya kitaifa ya kijinga na ya manufaa kwa taifa. Mijadala ya kijinga hupata ufuasi mkubwa. Ukitaka kupima ujinga wa Watanzania kwa urahisi sana hasa mitandaoni basi weka link mbili:

Ya kwanza sema "(Diamond na Aliy Kiba wakamatwa na unga )"

Na ya pili sema "(Unga kilo 2200/=, Njaa)". Unadhani itasomwa zaidi ipi?.

Wakati mwingine inaniuma nikikumbuka na kufikiria kuwa mimi ni raia wa taifa ambalo watu wake husahau tukio lolote kila baada ya saa moja tu. Ninasisitiza Magufuli aongeze kubana zaidi, ipo siku wajinga watapevuka.

Duniani hususani Tanzania si mahala pazuri pa watu wema na wenye kuiishi kweli, watu hawa kwao ni peponi. Kuishi na wanadamu duniani kunahitaji maarifa ya duniani. Tanzania bado tunayosafari ndefu, nyota ya matumaini imezimika, wanaotutweza wameinuliwa juu na wananena kwa lugha wakituaminisha Muumba yupo nao.

Bahati Mbaya Tanzania wanauchumi hutumia Siasa kuuchambua (political economy) na kuacha kundi la watu (macro Economy) likitopea katika umasikini. Mwana Uchumi yeyote; Tunaposema Uchumi unakuwa, Tunaangalia Sehemu Kuu Mbili, Uchumi Wa Kiujumla na wa Mtu Mmoja mmoja,

Mungu alishamaliza kila kitu vichwani mwetu, vipawa na akili ni swala la sisi tu wenyewe kuamua namna ya tunavyotaka kuzitumia akili zetu. Kila binadamu ameumbwa na kichaa, tofauti ni kuwa vichaa vya wengi vimelaa, kuna watu hapa twita ukiviamsha vichaa vyao ni balaa.

Tulihimiza kwanba muda wa kusubiria kituoni kupiga kura ni mdogo kuliko muda wa kusubiria mtawala aliyetokana na wewe kutopiga kura atoke madarakani. Maoni yangu Bangi ihalalishwe kama sehemu ya kuheshimu uhuru unaolindwa na katiba ya Tanzania wa kuabudu na imani za watu hasa sisi marastafari ambao bangi ni sakramenti, Huenda kwa miendo ya taifa sasa idadi ya wanaume inapungua sana mjini, na idadi ya wakiume inaongezeka sana huku mauzo ya chips mayai ikipanda na mauzo ya ugali dona ina doda.

Mtu anaekula shingo ya kuku na firigisi ana tofauti gani na kula 'pipe' ?
 
Sijapata muunganiko wa title ya uzi machoz ya mwanamke ni silaha kubwa na content, au umeweka title ya kuvutia watu wasome na wewe?
 
Nimeelewa kuhusu kuhalalisha bangi tu.mengine zero

Mkuu Yericko umetumia Uhuru unaozungumzwa kwenye katiba kama kigezo cha nyinyi marasta kuruhusiwa kutumia sacrament. Je,Uhuru huo hauna mipaka?Je Uhuru huo utumiwe na mashoga kugongewa
 
Yericko ni wewe au kuna mtu kakupostia hii? Umekurupukia wap leo hata sijakuelewa
 
Sijapata muunganiko wa title ya uzi machoz ya mwanamke ni silaha kubwa na content, au umeweka title ya kuvutia watu wasome na wewe?

Ndo think tank ya BAVICHA huyo. Kama huyu ndo anategemewa mwenye akili, hao kina Swissme sijui watakuwaje!
 
Nimeelewa kuhusu kuhalalisha bangi tu.mengine zero

Mkuu Yericko umetumia Uhuru unaozungumzwa kwenye katiba kama kigezo cha nyinyi marasta kuruhusiwa kutumia sacrament. Je,Uhuru huo hauna mipaka?Je Uhuru huo utumiwe na mashoga kugongewa
FAIDA 11 ZA KIAFYA ZA MATUMIZI YA BANGI (MARIJUANA).
Katika baadhi ya nchi Duniani, matumizi ya bangi yamehalalishwa kuzingatia utashi wa mamlaka za nchi husika. Uruguy na Marekani (katika majimbo 20) ni mifano ya nchi hizo. Tafiti mbalimbali za kiafya zimefanyika na kupelekea ugunduzi kuwa bangi huweza kutumika kama tiba kwa baadhi ya magonjwa, isipokuwa haipaswi kutumika ovyo kama ilivyo kwa dawa zingine. Zifuatazo ni faida 11 za kiafya za bangi. Kisha tutaeleza na athari hasi za bangi hapo baadae.

1.Inaweza kutumika kukinga na kutibu presha ya jicho (glaucoma), bangi inapunguza presha ya jicho (intraocular pressure) kwa watu wenye presha ya kawaida na hata wale ambao presha ya jicho iko juu( glaucoma).
2. Inaweza kuboresha afya ya mapafu na kupunguza athari za tumbaku katika mapafu. Januari 2012, tafiti zilionesha bangi haiathiri kazi za mapafu badala yake huongeza ufanisi wa mapafu.
3. Huweza kuzuia kifafa. Kemikali aina ya Tetrahydrocannabinol au THC iliyopo katika bangi huambatana na seli za ubongo zinazochochea umeme katika mfumo wa fahamu. Muambatano huo hupunguza msisimko (excitability) wa mfumo w fahamu na kuzuia kutokea kwa kifafa.
4.Kuzuia kuenea kwa baadhi ya kansa, Cannabidiol au CBD ni kemikali iliyopo kwenye bangi ambayo hupunguza kuenea kwa kansa mwilini. Mfano, kansa ya matiti.
5.Inapunguza wasiwasi, maumivu na kichefuchefu, hata hivyo ikitumiwa kwa kiasi kikubwa huweza kuongeza wasiwasi.
6. Hupunguza na kutibu matatizo ya kutetemeka kwa misuli, (Parkinsonism)
7. Bangi huweza kutibu magonjwa ya utumbo (Inflammatory bowel diseases). Mwaka 2010 katika chuo cha Nottingham, tafiti ziligundua kuwa kemikali zilizopo kwenye bangi husaidiana na seli za mwilini kuongeza kinga za mwili na ufanisi wa utumbo.
8. Kupunguza maumivu ya viungo. Bangi hupunguza maumivu, hupunguza miwasho na kuleta usingizi.
9. Huboresha ngozi na kuchangamsha kazi za mwilini, Pia huongeza matumizi ya sukari mwilini.
10. Huongeza uwezo wa kubuni vitu(creativity), uwezo wa kukumbuka na uwezo wa kuzungumza.
11. Huweza kusaidia watu wanaopata matatizo ya mfadhaiko kutokana na kumbukumbu za mambo ya kutisha (post traumatic stress disorder) Mfano, Kwa wahanga wa majanga ya asili na yale yasio ya asili kama vita, moto, tsunami nk. Watu hao hupata kuona upya matukio ya kutisha walioshuhudia zamani na huweza pia kuyaona katika ndoto. Bangi huweza kuwasaidia kuepuka tatizo hilo. Maveterani wa vita ni mfano mzuri kabisa.
ANGALIZO. Matumizi ya kiafya ya bangi yanapaswa kuwa chini ya maelekezo ya mtaalamu/Wataalamu. Kwa kuwa athari zake hutegemea kiasi cha matumizi na hali ya afya ya mtumiaji. Inaaminika kuwa Bangi ina athari chache kulinganisha na pombe.


Dr.Chris Cyrilo.
Asante.
 
Ungeipangilia vizuri ingekuwa riwaya moja nzuri sana
Uzi wako umeufanya kuwa mgumu sana kwa hadhira uliyoilenga
 
Back
Top Bottom