Macho yangu yanaona kama yako? CCM mnaenda kuanguka na anguko lenu ni kubwa sana

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,897
Serikali ya CCM imepoteza dira na mwelekeo inaelekea shimoni inaenda kuanguka na anguko lake ni kubwa sana imepoteza mvuto inawatia hofu Watanzania masikini.

Walianza na hofu ya internet, kwa maana ya Bando watu walichachamaa sana wakabadili gia angani baadaye tena wakaja na suala la Corona na chanjo watu wametishwa sana tena sana baadaye limekuja suala la kufukuza machinga nalo linafukuta.

Hili ni hatari narudia kusema hili ni hatari linaenda kuiangamiza CCM amini nawaambieni ukweli ni kuwa watu wamedevelop resistance they are insensitive yaani hizi colonial mindset za viongozi ni mbaya sana.

Unakuta yeye anahudumiwa kila kitu na Serikali anaanza tena kukimbizana na wafanyabiashara wadogo wadogo wanaotafuta 2000 ya kuwalisha watoto, hivi hali hii ni zaidi ya mfumo wa kinyonyaji.

Serikali iache kuhangaika na hawa watu wadogo wadogo ijiulize kuwa hawa mamilioni ya watu ambao haijawaajili wataenda wapi? yaaani kwa kweli very painful sana kwa Kheri CCM.
 
Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
 
Serikali isiwaguse kabisa wafanyabiashara wadogo wadogo. Waachwe wawe huru kufanya biashara wanavyotaka na vibali wapewe.

Waendelee kupika na kujenga vibanda kandokando ya barabara kwenye maeneo yaliyotengwa kwa dharura na watembea kwa miguu. Kuna wanaolala maeneo hayo, waachwe ni haki yao.

Kuna wanaojisaidia maeneo hayo wasiguswe. Vijana nguvu kazi waendelee kuhama vijijuni waende mijini wakarundikane kariakoo nk waachwe wasiguswe kabisa.

Wafanyabiashara wakubwa wenye maduka wafunge maduka yao na badala yake waendelee kuwatumia ipasavyo wafanyabiashara wadogo wadiogo kuaauzia biashara zao kwa ufanisi mkubwa bila kubugudhiwa sababu hii nchi ni yetu sote
 
Suala la wamachinga si la CCM ni sisi wananchi tunaotaka tuishi kistaarabu tofauti na nzi. Usilete siasa kwenye suala la wamachinga, pia ujue kila mtu anayefanya biashara hamfanyii mtu mwingine zaidi ya yeye kujipatia pesa za kujikimu na familia yake.

Ni ujinga kusema mmachinga anatafuta shilingi 2000 ya kulisha familia yake na wenye maduka hawana shida ya hela.

Naona unajaribu kuingiza udhaifu wa viongozi wetu wanaodhani wamachinga ndiyo wanyonge wengine matajiri hivyo wamachinga wabembelezwe kufuata sheria.

Serikali iwaondoe wamachinga ili kila mtu awe na haki ya kufanya biashara na kutumia barabara bila bughudha.
 
Serikali ya CCM imepoteza dira na mwelekeo inaelekea shimoni inaenda kuanguka na anguko lake ni kubwa sana imepoteza mvuto inawatia hofu Watanzania masikini walianza na hofu ya internet, kwa maana ya Bando watu walichachamaa sana wakabadili gia angani baadaye tena wakaja na suala la Corona na chanjo watu wametishwa sana tena sana baadaye limekuja suala la kufukuza machinga nalo linafukuta hili ni hatari narudia kusema hili ni hatari linaenda kuiangamiza CCM amini nawaambieni ukweli ni kuwa watu wamedevelop resistance they are insensitive yaani hizi colonial mindset za viongozi wapumbavu ni mbaya sana unakuta yy a Anahudumiwa kila kitu na serikali anaanza tena kukimbizana na wafanyabiashara wadogo wadogo wanaotafuta 2000 ya kuwalisha watoto hivi hali hii ni zaidi ya mfumo wa kinyonyaji

Serikali iache kuhangaika na hawa watu wadogo wadogo ijiulize kuwa hawa mamilioni ya watu ambao haijawaajili wataenda wapi? yaaani kwa kweli very painful sana kwa Kheri CCM
Watu kama wewe bado hamjafikiwa tu. Dawa yenu ni ndogo sana.

Utakaposhibishwa hiyo njaa inayokufanya upige kelele hapa hutasikika tena. Kwanza wewe ndiye utakuwa mstari wa mbele kuwananga hao unaojifanya leo hii unawapigania!
 
Serikali isiwaguse kabisa wafanyabiashara wadogo wadogo. Waachwe wawe huru kufanya biashara wanavyotaka na vibali wapewe. Waendelee kupika na kujenga vibanda kandokando ya barabara kwenye maeneo yaliyotengwa kwa dharura na watembea kwa miguu. Kuna wanaolala maeneo hayo, waachwe ni haki yao. Kuna wanaojisaidia maeneo hayo wasiguswe. Vijana nguvu kazi waendelee kuhama vijijuni waende mijini wakarundikane kariakoo nk waachwe wasiguswe kabisa. Wafanyabiashara wakubwa wenye maduka wafunge maduka yao na badala yake waendelee kuwatumia ipasavyo wafanyabiashara wadogo wadiogo kuaauzia biashara zao kwa ufanisi mkubwa bila kubugudhiwa sababu hii nchi ni yetu sote
Hili suala sio la kujibu kwa hasira wala kukurupuka hata kidogo, tukianza kuongelea maisha ya kijijini ambako asilimia tisini ya wakazi vijiji vingi shughuli zao ni kilimo, hali ni mbaya sana.

Aisee labda uwe hujaishi vijijini, kwa wale wasio na rasilimali fedha either kwa kupata kutoka kwenye source nyingine mfano biashara, ajira n.k inayowawezesha kufanya kilimo cha kisasa kwa eneo kubwa, kuwa na maghara/ uthubutu wa kuhifadhi mazao baada ya mavuno na kusubiri mpaka bei ya bidhaa kuwa ya kuridhisha au ikiwezekana kusafirisha mazao mpaka kwenye maeneo yenye masoko mazuri, hakika watu wataendelea kukimbia vijijini na kujazana mjini.

Kijijini sio pazuri kabisa kama huna mtaji, elimu bora ya msingi, pembejeo na vitendea kazi vya kisasa for large scale farming. Tusiongee tu kirahisi, serikali, sekta binafsi wanapaswa kuwekeza zaidi huko ukizingatia mijini kunajiendesha kwenyewe tayari kwa kiwango chake.

Machinga wapo mpaka Paris ufaransa, issue ni wamepangwaje? Serikali ingeweka standards za mmachinga kwa ku-demonstrate catalog ya setup ya mmachinga wa chini, wakati na wajuu. Pia wangewaita kama ambavyo wanaweza fanya kampeni wakajaza wananchi kwenye majukwaa nchi nzima, wakawafundisha namna nzuri za kujipanga, kuwe na siku ya wamachinga ikibidi katika mwaka, maana siku ya wafanyabiashara maarufu kama sabasaba ni kama sio yao, hata hivyo wafanyabiashara wakubwa wanawakataa hawa jamaa kwamba wanawabania riziki. Wengi utawaona siku ya nane nane ambayo sio yao pia.

Tuwasaidie maana nao ni watanzania pia na wana haki zao mbalimbali katika nchi yao. Ni rahisi sana kukosoa ikiwa ofisi yako ni rasmi, mmepewa mpaka usafiri na vitu kama hivyo lazima utawaona wao kama kero.

By the way, wamachinga ndio wateja wakubwa wa vyoo vya kulipia, hivyo kuziingizia mapato almashauri zetu, wanaojisaidia hovyo mara nyingi ni wapita njia na haswa haswa Mateja, watoto wa mitaani na makuli ambao ndio haswa wanaolala barabarani. Usiuongelee mtaa, ingia mtaani na uijue mitaa hakika hutalaumu sana zaidi ya kutafuta suluhu ya kudumu. Kweli hatupaswi kuishi kama inzi lakini pia hatupaswi fanya wananchi wetu kuwa kama wakimbizi nchini kwao kisa standards zisizoeleweka.

Uchafu wa miji serikali inamchango mkubwa sana, imagine kila mfuko wa mkate, kopo la juice/soda, pampers, mpaka hayo mabaki ya matunda, maganda ya miwa, na kila aina ya uchafu serikali imechukua asilimia yake kwenye kodi, tozo, ushuru au kwa namna nyingine yeyote, wanashindwa vipi kushirikiana na makampuni ya bidhaa husika kuweka miji safi? Hawatujali sisi na afya zetu hao. Bado wanamgambo, sungusungu, skauti, polisi, jeshi n.k ila sasa wao busy na siasa tu January to December. Hatuna viongozi wazuri bado.
 
Serikali ya CCM imepoteza dira na mwelekeo inaelekea shimoni inaenda kuanguka na anguko lake ni kubwa sana imepoteza mvuto inawatia hofu Watanzania masikini walianza na hofu ya internet, kwa maana ya Bando watu walichachamaa sana wakabadili gia angani baadaye tena wakaja na suala la Corona na chanjo watu wametishwa sana tena sana baadaye limekuja suala la kufukuza machinga nalo linafukuta hili ni hatari narudia kusema hili ni hatari linaenda kuiangamiza CCM amini nawaambieni ukweli ni kuwa watu wamedevelop resistance they are insensitive yaani hizi colonial mindset za viongozi wapumbavu ni mbaya sana unakuta yy a Anahudumiwa kila kitu na serikali anaanza tena kukimbizana na wafanyabiashara wadogo wadogo wanaotafuta 2000 ya kuwalisha watoto hivi hali hii ni zaidi ya mfumo wa kinyonyaji

Serikali iache kuhangaika na hawa watu wadogo wadogo ijiulize kuwa hawa mamilioni ya watu ambao haijawaajili wataenda wapi? yaaani kwa kweli very painful sana kwa Kheri CCM
2935090_IMG-20210717-WA0000.jpg
 
Suala la wamachinga si la CCM ni sisi wananchi tunaotaka tuishi kistaarabu tofauti na nzi. Usilete siasa kwenye suala la wamachinga, pia ujue kila mtu anayefanya biashara hamfanyii mtu mwingine zaidi ya yeye kujipatia pesa za kujikimu na familia yake. Ni ujinga kusema mmachinga anatafuta shilingi 2000 ya kulisha familia yake na wenye maduka hawana shida ya hela.
Naona unajaribu kuingiza udhaifu wa viongozi wetu wanaodhani wamachinga ndiyo wanyonge wengine matajiri hivyo wamachinga wabembelezwe kufuata sheria.
Serikali iwaondoe wamachinga ili kila mtu awe na haki ya kufanya biashara na kutumia barabara bila bughudha.
😍👍
 
Hili suala sio la kujibu kwa hasira wala kukurupuka hata kidogo, tukianza kuongelea maisha ya kijijini ambako asilimia tisini ya wakazi vijiji vingi shughuli zao ni kilimo, hali ni mbaya sana.

Aisee labda uwe hujaishi vijijini, kwa wale wasio na rasilimali fedha either kwa kupata kutoka kwenye source nyingine mfano biashara, ajira n.k inayowawezesha kufanya kilimo cha kisasa kwa eneo kubwa, kuwa na maghara/ uthubutu wa kuhifadhi mazao baada ya mavuno na kusubiri mpaka bei ya bidhaa kuwa ya kuridhisha au ikiwezekana kusafirisha mazao mpaka kwenye maeneo yenye masoko mazuri, hakika watu wataendelea kukimbia vijijini na kujazana mjini.

Kijijini sio pazuri kabisa kama huna mtaji, elimu bora ya msingi, pembejeo na vitendea kazi vya kisasa for large scale farming. Tusiongee tu kirahisi, serikali, sekta binafsi wanapaswa kuwekeza zaidi huko ukizingatia mijini kunajiendesha kwenyewe tayari kwa kiwango chake.

Machinga wapo mpaka Paris ufaransa, issue ni wamepangwaje? Serikali ingeweka standards za mmachinga kwa ku-demonstrate catalog ya setup ya mmachinga wa chini, wakati na wajuu. Pia wangewaita kama ambavyo wanaweza fanya kampeni wakajaza wananchi kwenye majukwaa nchi nzima, wakawafundisha namna nzuri za kujipanga, kuwe na siku ya wamachinga ikibidi katika mwaka, maana siku ya wafanyabiashara maarufu kama sabasaba ni kama sio yao, hata hivyo wafanyabiashara wakubwa wanawakataa hawa jamaa kwamba wanawabania riziki. Wengi utawaona siku ya nane nane ambayo sio yao pia.

Tuwasaidie maana nao ni watanzania pia na wana haki zao mbalimbali katika nchi yao. Ni rahisi sana kukosoa ikiwa ofisi yako ni rasmi, mmepewa mpaka usafiri na vitu kama hivyo lazima utawaona wao kama kero.
Hizi fremu nzuri za biashara hatujapewa na serikali, tumejikamua wenyewe. Maduka yetu hayana mali zozote toka serikalini na sisi pia tunaganga njaa na tunazo familia.
 
Hujanielewa, nimesema, wapewe catalog/ setup ( kwa lugha nyepesi naweza kusema muundo) na serikali kwamba hii ndio standard, wao sasa wakatengeneze za kwao, ila ziwe nafuu na zakupendezesha mji.
 
Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
Nini maana kila mtu achape kazi?
 
Serikali ya CCM imepoteza dira na mwelekeo inaelekea shimoni inaenda kuanguka na anguko lake ni kubwa sana imepoteza mvuto inawatia hofu Watanzania masikini walianza na hofu ya internet, kwa maana ya Bando watu walichachamaa sana wakabadili gia angani baadaye tena wakaja na suala la Corona na chanjo watu wametishwa sana tena sana baadaye limekuja suala la kufukuza machinga nalo linafukuta hili ni hatari narudia kusema hili ni hatari linaenda kuiangamiza CCM amini nawaambieni ukweli ni kuwa watu wamedevelop resistance they are insensitive yaani hizi colonial mindset za viongozi wapumbavu ni mbaya sana unakuta yy a Anahudumiwa kila kitu na serikali anaanza tena kukimbizana na wafanyabiashara wadogo wadogo wanaotafuta 2000 ya kuwalisha watoto hivi hali hii ni zaidi ya mfumo wa kinyonyaji

Serikali iache kuhangaika na hawa watu wadogo wadogo ijiulize kuwa hawa mamilioni ya watu ambao haijawaajili wataenda wapi? yaaani kwa kweli very painful sana kwa Kheri CCM
Una muono na akili za kutosha. Kongoree
 
Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
Kokote dunia machinga ni wafanyabiashara wanaotembea, akishakuwa na eneo la kudumu huyo sio machinga bali ni mwekezaji. Siasa zimeharibu nchi hii, barabara zilizojengwa kwa madhumuni ya vyombo vya usafiri zinageuzwa kuwa magulio, haya ni mawazo mafupi sana na siasa za kijinga.
 
Serikali isiwaguse kabisa wafanyabiashara wadogo wadogo. Waachwe wawe huru kufanya biashara wanavyotaka na vibali wapewe. Waendelee kupika na kujenga vibanda kandokando ya barabara kwenye maeneo yaliyotengwa kwa dharura na watembea kwa miguu. Kuna wanaolala maeneo hayo, waachwe ni haki yao. Kuna wanaojisaidia maeneo hayo wasiguswe. Vijana nguvu kazi waendelee kuhama vijijuni waende mijini wakarundikane kariakoo nk waachwe wasiguswe kabisa. Wafanyabiashara wakubwa wenye maduka wafunge maduka yao na badala yake waendelee kuwatumia ipasavyo wafanyabiashara wadogo wadiogo kuaauzia biashara zao kwa ufanisi mkubwa bila kubugudhiwa sababu hii nchi ni yetu sote
Naam,kwa kuwa Ndicho CCM WALICHOKIHUBIRI KWA MIKA 6 YA JPM ,na Hawa wanao waondoa Sasa nao walikuwawanahamasisha warundikane barabarani!
Malipo ya unafiki ni hayo ,kina Mini Hali no Mbaya ,maduka yapo barabarani...Arusha ,Mwanza,Dar na Mbeya ...Jini wamelifuga wenyewe acha liwatese!
 
Kokote dunia machinga ni wafanyabiashara wanaotembea, akishakuwa na eneo la kudumu huyo sio machinga bali ni mwekezaji. Siasa zimeharibu nchi hii, barabara zilizojengwa kwa madhumuni ya vyombo vya usafiri zinageuzwa kuwa magulio, haya ni mawazo mafupi sana na siasa za kijinga.
CCM no janga ...Jiwe aliwahi waambia wakaweke bidhaa hata mlangani kwa Mkuu wa Wilaya!
Tukishasema siku nyingi Wamachinga na Bodaboda no pressure Group ya hatari amabayo CCM wanait3ngeneza bila kijua ...subiri tuone!
 
Nasubiri sana kusikia kwa mtu aliyeko mwanza aniambie kama nje ya lango la Hotel ya kasheku msukuma kuna machinga waliopanga biashara zao hapo!
 
Hili swala la machinga linaathiri sana uchumi wa nchi. Likiachwa kama ilivyo sasa bado ni tatizo kubwa kwani linasaidia sana ukwepaji wa kodi.

Machinga wengi ni madalali wa biashara za wafanyabiashara wakubwa. Kama tunaingalia kesho yetu lazima tuone hili kama tatizo. Lazima maumivu kidogo yawepo kwa kila anaehusika kwenye hili. Cha msingi ni kuhakikisha wakati wa kuwapanga hakuna anaepoteza bidhaa zake.
 
Serikali ya CCM imepoteza dira na mwelekeo inaelekea shimoni inaenda kuanguka na anguko lake ni kubwa sana imepoteza mvuto inawatia hofu Watanzania masikini walianza na hofu ya internet, kwa maana ya Bando watu walichachamaa sana wakabadili gia angani baadaye tena wakaja na suala la Corona na chanjo watu wametishwa sana tena sana baadaye limekuja suala la kufukuza machinga nalo linafukuta hili ni hatari narudia kusema hili ni hatari linaenda kuiangamiza CCM amini nawaambieni ukweli ni kuwa watu wamedevelop resistance they are insensitive yaani hizi colonial mindset za viongozi wapumbavu ni mbaya sana unakuta yy a Anahudumiwa kila kitu na serikali anaanza tena kukimbizana na wafanyabiashara wadogo wadogo wanaotafuta 2000 ya kuwalisha watoto hivi hali hii ni zaidi ya mfumo wa kinyonyaji

Serikali iache kuhangaika na hawa watu wadogo wadogo ijiulize kuwa hawa mamilioni ya watu ambao haijawaajili wataenda wapi? yaaani kwa kweli very painful sana kwa Kheri CCM
Bora wafe kabisa
 
Back
Top Bottom