Macho yangu yanaona kama yako? CCM mnaenda kuanguka na anguko lenu ni kubwa sana

Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
Kila mtu anakubaliana na hili except, do they have options kama zako?
Je ungekuwa huna ajira na hali hiyo walioyonayo could you have uttered these words?

Wamachinga ni watanzania kama wewe, kama hawajatafutiwa namna nzuri basi hakuna mwenye haki ya kuwasema vibaya
 
Tangu wafanywe ni mtaji wa kisiasa ndipo kosa kubwa serikali ipofanya.
Ni idadi kubwa ya machinga watafulia kwasababu ya hatua zinazochukuliwa sasa. Inabidi pia serikali iniandae na hili kundi litakalopoteza mitaji yao baada ya hizi hamishahamisha/ bomoabomoa.
 
Unaongelea nchi gani? Huyo mmachinga wa kumpa kiwango atengeneze ni wa hapa! Na akishatengeneza aliweke wapi zaidi ya katikati ya barabara.
Wengi wa hao wamachinga wanalala kwenye mabanda yao.
Bado tu hujanielewa! Kama mtoa mada mmoja alivyochangia humu, Machinga imeyokana na neno la kiingereza “marching guy” kwa maana ya kuwa hakai sehemu moja throughout, sidhani kama watashindwa unda vibaiskeli spesheli na kuzunguka navyo mitaani badala ya kujiposition sehemu moja. Huu ni mfano tu, ni wakati sasa viongozi kituonyesha bongo zao zinafikiria kwa kiasi gani.
 
Wamachinga kukaakatikati ya miji ni kiss, lazima watafutiwe sehemu ili miji iwe safi, na isiwe na foleni
 
Back
Top Bottom