Macho yanaona mbali lakini ni vigumu kuliona sikio lako! tafakari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Macho yanaona mbali lakini ni vigumu kuliona sikio lako! tafakari!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmh, Jun 25, 2011.

 1. mmh

  mmh JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 852
  Likes Received: 652
  Trophy Points: 180
  Watu wengi wanataka kuona wenzao wakiwajibika kuliko wao kuwajibika, utakuta mtu yeye mvivu balaa na ana matatizo chungu nzima lakini yeye wala hana habari na yeye mwenyewe anaangalia wenzake tu, sijui huyu hafai sijui yuko hivi na kumsababishia mwenzake kero kubwa lool. Halafu wandugu chunga sana watu wavivu na wazembe wanafitina ni balaa. Hayo utayakuta sana maofisini na mitaani.

  Sambamba na hilo utakuta mtu analaumu ooh kiongozi fulani hatimizi wajibu wake ooh ni fisadi ooh sijui nini wakati yeye katika nafasi aliyo nayo japo ndogo haitendei haki ni mwizi ni mtegezi ni mwana majungu ni mbaguzi, hee, tubadirike jama nchi tutaijenga wenyewe tutimize wajibu wetu.
   
Loading...