Macho ya rohoni huona zaidi ya kuona | Sauti ya rohoni husikika zaidi ya kipaza sauti

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,757
Utabarikiwa na hiki nitakachoandika usiku huu tulivu.
Uono wa macho ya rohoni na usikivu wa sauti ya rohoni.. Hivi ni vitu viwili vyenye nguvu kubwa sana kwenye mustakabali wa maisha yako... Kesho yako...
Kesho yako kazini kwako
Kesho yako kwenye biashara yako
Kesho yako kwenye kipaji, kipawa chako
Kesho yako kwenye usanifu, ubunifu wako
Kesho yako kwenye mahusiano nknk

Chukua muda utulie na kusikiliza sauti rohoni zinasema nini... Ni muhimu sana
Chukua muda utulie uangalie macho ya rohoni yanakuangazia wapi.. Msingi wa mustakabali wa kesho yako huanzia hapo

Maisha ni hatua.. Maisha ni mchakato.. Ziamini ndoto zako kwakuwa ndoto ni uhalisia wetu wa ndani kupitia ufahamu maizi.. Ndoto zinazungumza.. Ndoto zinatuonesha tuendako.. Ndoto hizi hutafsiriwa kupitia macho na sauti za rohoni
Natambua hujanipata vema kuhusu ndoto... Kuhusu sauti za rohoni.. Kuhusu macho ya rohoni.... Nisikilize tena.
Katika hatua za makuzi kila wakati kuna sauti zinakwambia wewe unapaswa kuwa fulani.. Halafu kuna uono unakuonesha vile unavyotakiwa kuwa... Kweli si kweli? Hivi viwili ndio hutengeneza ndoto yako katika tafsiri yake.

Twende na mifano michache upate kunielewa vema.
Wote tunamfahamu vema mwanzilishi wa JamiiForums ndugu yetu Maxence Melo.. Natamani nipate wasaa wa kuhojiana naye.. Nina hakika alijiona akisimama toka kwenye kigoda mpaka kukaa hapo alipo
Wote tunamfahamu mtoto wa Mbagala Diamond Platnamuz... Alipotoka... Alipo sasa na huko aendako.. Anaziishi ndoto zake
Mifano ni miwili tu lakini naamini ni kiwakilishi cha wengi kwenye kuziishi ndoto... Kusikiliza sauti za rohoni na kuangalia kwa macho ya rohoni

Kuna swami moja maarufu watu huulizwa.. Swali husika ndio hubeba uhalisia wa mustakabali wako maishani... UNATAKA KUWA NANI? Jibu la kwanza bila kuwaza ndio huwa sahihi. Kwakuwa kufumba na kufumbua hujiona wewe pale unapotaka kuwa na automatically jibu hukutoka.. Ni kitendo cha split of seconds.

Usijaribu kuwa tofauti ni kile kinachokuambia rohoni mwako.. Usijaribu kuwa tofauti ni kile kinachokupa mwanga wa uono rohoni mwako.. HUTAFANIKIWA.. Kwakuwa unakuwa mpangaji kwenye NAFSI yako mwenyewe

Ujanani kwenye hatua za makuzi ndoto huwa nyingi lakini ukitulia kuna moja hujirudiarudia.. Ifuate hiyo kwakuwa hiyo ndio wewe wa baadae

Usikimbilie kufanikiwa katika hatua za mwanzo za makuzi kabla hujahakikisha ndoto yako.. Wengi wamekwama hapa na kuharibikiwa kabisa
Natambua wazi uko kwenye ajira lakini unajiona kabisa hapo sio kwako.. Unajiona ukiwa kwenye nafasi nyingine kabisa
Natambua uko kwenye biashara lakini unajiona kabisa kuwa unahitaji kukua na kuwa mfanyabiashara mkubwa
Natambua uko kwenye fani lakini kila ukijitazama unajiona kabisa level yako unayostahili ni ya kimataifa

Natambua uko kwenye mahusiano rasmi ama yasiyo rasmi lakini kila ukiangalia mbele unaona giza ama unajiona mkiwa na mwenza wako kwenye maisha fulani ya furaha na mafanikio makubwa.. Kurunzi la rohoni kwenye mahusiano lina nguvu kuliko chochote
Kurunzi la rohoni kwenye mahusiano linaimulika vema kabisa kesho yako.. Hebu liangalie kama linawaka ama unaona giza

Hatua hii ya utambuzi wa kiroho kwenye maisha yako ni muhimu sana sana kuichunga kwakuwa ukifanya kosa tuu.. Umekwisha... Kwakuwa ni katika hatua hii wengi wetu hutaka ndoto zitimie haraka
Kwenye usanii
Kwenye ubunifu
Kwenye vipawa
Kwenye mahusiano
Kwenye ajira
Kwenye biashara
Kwenye siasa
Usijaribu kabisa kulazimisha hapa... Maana yangu ni kwamba usipaniki ukataka kutafuta njia za mkato.. Kama wizi, dili chafu na kubwa kuliko yote USHIRIKINA...

Natambua kuna wakati ndoto hukusukuma kwa nguvu sana utoke hapo ulipo na kukaa kwenye nafasi yako... Hilo halizuiliki... Lakini kamwe usiangukie kwenye mtego wa nguvu za giza
Tamaa ya kutimiza ndoto haraka ni ibilisi anayekusukuma uende uelekeo usio sahihi... Tamaa inakutia upofu wa kuona ATHARI za mbeleni utapokuwa umesimana sasa... Utahubiriwa habari za waliofanikiwa kupitia USHIRIKINA... Usiwasikilize hao ni madalali wa ulozi.. Kama ni mafanikio kwani wao hawayataki? Umeshawahi kujiuliza hili swali? Huko gizani ni utumwani.. Wewe unakuwa mtumwa na mateka wa maagano na makafara na miiko migumu

Unaweza kusema nimechoka mimi ngoja nijilipue.. Lakini majuto yatakuja baadae.. Hakuna kitu kibaya kama viapo na maagano ya damu... Kiwango huongezeka kila hatua... Mwisho wa yote ni anguko kubwa na lenye mateso makubwa na sometimes fedheha na aibu. Si kila umuonaye amefanikiwa ana furaha na amani kama unavyodhani

Ziishi ndoto zako katika njia sahihi.. Katka mstari mnyoofu... Jicho lako na kurunzi la rohoni vikumulikie uelekeo sahihi.. Sauti ya rohoni isibebe mwangi unaotisha bali kila uisikiapo ile loud and clear

Je umekumbuka chumvi yako leo?
Nakuombea ndoto zako zikatimie katika mstari sahihi.. Kumbuka una kipimo chako kwenye maisha yako.. Usilazimishe kuongeza.. Utaharibu chombo...

Alamsiki....!!!
 
Mshana Jr, Leo nilitembelewa na jamaa yangu mmoja, analalamika Kila mti anaoupanda eidha hung'olewa, hukatwa au huchomwa Moto Kama sio kuliwa na wadudu au mifugo.

Kaanza kupanda miti mwaka 1998 Hadi Sasa, lakini hamna mti hata mmoja umekuwa. Alianza kupanda miti kijijini kwao Matembwe Njombe, ikafa, Iringa pia miti ikafa, Moro, Mbeya, Singida, Dar na Sasa kahamishiwa Dodoma, miti bado inakufa. Wengine wakipanda miti jirani na yeye inakuwa.

Je, shida ni Nini?
 
Mshana Jr, Leo nilitembelewa na jamaa yangu mmoja, analalamika Kila mti anaoupanda eidha hung'olewa, hukatwa au huchomwa Moto Kama sio kuliwa na wadudu au mifugo.
Kaanza kupanda miti mwaka 1998 Hadi Sasa, lakini hamna mti hata mmoja umekuwa.
Alianza kupanda miti kijijini kwao Matembwe Njombe, ikafa, Iringa pia miti ikafa, Moro, Mbeya, Singida, Dar na Sasa kahamishiwa Dodoma, miti bado inakufa. Wengine wakipanda miti jirani na yeye inakuwa.
Je shida ni Nini?
Mmh seriously!? maisha yake yakoje?
 
Mmh seriously!? maisha yake yakoje?
Stagnant, alikuja kupata ushauri, ndipo nikamuuliza Kama anafuga, Hali ya mifugo ikoje, akasema alijaribu Mara kadhaa kufuga ng'ombe wa maziwa wanaokopeshwa kwenye vikundi lakini walikufa , mmoja alikula mfuko wa Rambo, mwingine alikufa akizaa akaachana na ufugaji maana ulimwingiza kwenye madeni.
Ndipo akanipa hicho kiss Cha miti kilichonistaajabisha na kuniacha kinywa wazi
 
Stagnant, alikuja kupata ushauri, ndipo nikamuuliza Kama anafuga, Hali ya mifugo ikoje, akasema alijaribu Mara kadhaa kufuga ng'ombe wa maziwa wanaokopeshwa kwenye vikundi lakini walikufa , mmoja alikula mfuko wa Rambo, mwingine alikufa akizaa akaachana na ufugaji maana ulimwingiza kwenye madeni.
Ndipo akanipa hicho kiss Cha miti kilichonistaajabisha na kuniacha kinywa wazi
Mmh... Kuna kasoro kubwa hapo...
 
.
kGvMR2agdTH3hefFYcGpjaZxdEkx1t0YVqdtBAhEHtPzTqmqFpgzziUBAascV6BJWyHEHws_QGcBFnM3odH5mR6j5EAQoP...jpg
 
Ikoje...!?
Niliota nipo kwa gari na mkuu wangu mara ikapata pancha, kisha ikaendelea nipo na wadau wengine katika viunga mfanano na pancha ya gari, pikipiki nayo ikapata pancha, nikajitwisha tairi kwenda kuziba, gafla binti yangu naye katokea mbele yangu, tukaongozana, hapo nikaamka, nikaona isiwe kesi saa nane hii ya usiku ngoja niingie jf, namkuta Mshana Jr keshafanya yake, hapo ni mishale ya saa tisa sasa. Ni hivyo
 
Back
Top Bottom