Machinjio ya zaidi ya Bilioni 1 jiji Mwanza yageuka nyumba ya popo

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Machinjio ya zaidi ya Bilioni 1 jiji Mwanza yageuka nyumba ya popo

Mkurugenzi agoma kununua mashine


Halmashauri ya jiji la Mwanza imeshindwa kununua mashine za kuchinjia mifugo tangu mwaka 2018

Machinjio hiyo iliyojengwa kwa gharama ya Tsh. Bilioni moja kwa sasa imegeuka kuwa nyumba ya popo.

Taratibu za kuanza kujengwa machinjio hiyo zilianza mwaka 2016 enzi za Mkurugenzi Adam Mgoyi ambaye kwa sasa ni mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Machinjio hiyo iliokamilika katika baadhi ya maeneo kwa sasa imeshindwa kuanza kufanya kazi kutokana na watendaji wa jiji hilo chini ya Mkurugenzi wake kiomoni Kibamba kushindwa kununua mashine za kuchinjia.

Kushindwa kununuliwa kwa mashine hizo zitakazosaidia kuchinjwa kwa mifugo katika hali ya usalama, kumesababisha machinjio hiyo kugeuka nyumba ya wadudu wakiwamo popo.

Inaelezwa kwa kipindi kirefu viongozi wa ngazi za juu wamekuwa wakitoa maagizo ambayo kwa kipindi kirefu yamekuwa hayatekelezwi.

Miongoni mwa viongozi waliowahi kuagiza machinjio hiyo kukamilishwa kwa wakati ni Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu.

Makamu huyo wa Rais alitoa agizo hilo kwa kiomoni Kibamba, mwaka 2018 akimtaka kuhakikisha machinjio hiyo inawekewa mashine za kuchinjia lakini mpaka leo hii hakuna hatua zilizochukuliwa.

Makamu huyo wa rais alitoa agizo hilo, akiwa mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi.

Kutokana na uzembe uliopo kwa baadhi ya watendaji hao hususani Mkurugenzi Kibamba pamoja na watendaji wake wa idara ya fedha kumekuwa kukisababisha baadhi ya miradi kukwama ikiwemo huo wa machinjio.

Mmoja wa watu watumishi wa jiji hilo (jina linahifadhiwa) anaeleza kwamba kushindwa kukamilishwa kwa machinjio hiyo inatokana na mkurugenzi Kibamba.

Mtumishi huyo anasema kwamba, kwa kipindi kirefu pamoja na maagizo kutolewa amekuwa akishindwa kuchukua hatua.

Anasema kikwazo kikubwa kinachokwamisha kununuliwa kwa mashine za kujinjia mifugo kinasababishwa na Mkurugenzi mwenyewe.

"Unajua pamoja na maagizo ya wakuu wa nchi kutolewa kuhusu kukamilishwa kwa baadhi ya vitu ikiwemo mashine hizo, ukiangalia chanzo ni Mkurugenzi ambaye yeye anaona machinjio kwake sio kipaumbele.

"Pia Mkurugenzi huyu yeye kufanya jambo mpaka maelekezo kutoka juu, mfano mzuri ni wodi ya wanaume pale Hospitali ya Wilaya (Nyamagana) imejengwa mpaka agizo lililotolewa na Rais John Magufuli.

"Bila lile agizo la Rais alilotoa miezi kadhaa iliyopita, hata ile wodi isingejengwa mpaka kuisha, sasa hapo ndipo uangalie uwezo wake ulivyo hawezi kufanya kitu mpaka aelekezwe.

"Ukiangalia hata pale Machinjioni akiona viongozi wanaenda pale ndipo anaanza kutafuta watu wa kufanya usafi ili kuweka mazingira safi.


Katika ripoti ya Mkaguzi mkuu wa hesabu ya 2017/18 inaonesha kuwa jiji Hilo na wahisani wengine walikubaliana kuwa baada ya kukamilika machinjio hiyo jiji litakuwa na wajibu wa kuweka mashine.

Tangu machinjio hiyo ikamilike, 15 agousti mwaka 2018 ilikabidhiwa kwa halmashauri hiyo lakini mpaka Leo haijaanza kutumika kutokana na jiji kushindwa kununua mashine na kusababisha machinjio hayo kugeuka nyumba ya popo na wadudu wengine.


NB: Rais Magufuli tupia jicho lako Mwanza, watendaji wako hawafanyi kazi mpaka uwape maelekezo hii inaonesha uwezo wao wa utendaji wa kazi ni mdogo.
................................
 
Back
Top Bottom