Machinga wasilete siasa waondolewe haraka miji yote Tanzania

Nadhani cha kufanya wajiunhe hata 10 ikibidi, wachukue fremu na wafanye bishara rasmi
Fremu leo zimedoda mikoa yote, ina maana Machinga wanashindwa kujiunga hata watatu watatu wakachukua fremu wakaripa Kodi?

Nchi imekuwa ya kipuuzi sana mama ntilie wanashindwa kujiunga wakatengeneza taasisi inayolipa Kodi na wakafanya derivali ya chakula kwenye maofisi mida ya mchana?

Mpaka wakae kila Kona ya mtaa. Ebu tuache ushamba basi

Nashauri Machinga wathibitiwe Kama wanagoma vibanda vyao vyote vichomwe hatuwezi kuwa na taifa la watu wasiolipa Kodi, kufuata Sheria na katiba ya Nchi .

Mbaya zaidi kupoka haki za wengine hii haikubaliki hata kidogo lazima tuwe taifa la mfano.

Na mikoa yote ondoeni Machinga wenye mitaji mikubwa wakapange fremu wauze online bidaa zao wafanye derivali.

Wenye mitaji midogo watengewe viwanja vikubwa viwe Kama minada wafanye uko mbona kila mkoa unayo maeneo?

Makala nakushauri vunja kabisa kila kitu maana wabongo Ni wabishi Sana bila kuwavunjia hawataondoka kwa heri.

Tujenge Nchi tuache kufanya kila kitu siasa. Siasa ndio imetufikisha hapa tulipo.
 
Big NO! Si wewe uliyekuwa mwanafunzi wa university mojawapo nchini uliyesomeshwa na wazazi wako kupitia huo umachinga!
Tz ni taifa pekee katika sayari hii kwa kukamua ng'ombe bila kumlisha vizuri,wekeni mazingira wezeshi kisha watakeni kulipa hiyo kodi.
 
Machinga ni wale wanaozunguka na bidhaa mkononi wale ndio wapewe vitambulisho vya ujasiriamali lakini wale wanaojenga vibanda ni wakwepa kodi tu, wengi wana mitaji mikubwa wanastahili kulipa kodi haiwezekani wenye viduka uchwara na cafe mitaani walipe kodi eti kwa kuwa wamepanga fremu lakini wenye vibanda mabarabarani wao wapewe vitambulisho hiyo siyo haki.
 
Anayestahili kupewa kitambulisho ni mfanyabiashara mdogo yoyote aliye na mtaji wa -4000,000/=. Mengine hayo ni tafsiri yako.
 
Mkuu, hao ndio wanarudi kitaa kutafuta pesa kwa ngeta!
Hivyo tukae mkao wa kutulia, tusubiri yajayo.

Nadhani kungekuwa na smooth transitiin ya maeneo wanayopaswa kufanyia biashara zao, na si kibabe kama ilivyokuwa leo vingunguti.
Wa wao wakae standby kupigwa viberiti na petroli without hesitation huku mtaani..hatutacheka na mwizi.
 
Machinga ni wale wanaozunguka na bidhaa mkononi wale ndio wapewe vitambulisho vya ujasiriamali lakini wale wanaojenga vibanda ni wakwepa kodi tu, wengi wana mitaji mikubwa wanastahili kulipa kodi haiwezekani wenye viduka uchwara na cafe mitaani walipe kodi eti kwa kuwa wamepanga fremu lakini wenye vibanda mabarabarani wao wapewe vitambulisho hiyo siyo haki.
Yaani Samia inabidi akomae watu waondoke huko mabarabarani..kuna mmoja leo nimemsikia anasema amekopa 15m lakini biashara anafanya katikati barabarani kwenye kibanda cha maturubai..kama sio ujuha kuendelea kuwaacha hawa watu ni nini?..
 
Hata hili la kujiunga ili wapate nguvu ya kuchuka fremu na walipe kodi unataka kubisha?
HAIWEZEKANI watu wa kaliba tofauti muungane mkodishe fremu Kariakoo ya 1,000,000 muuze sidiria mwingine madera, haya mawigi nk hamtaelewana chumba kimoja, km mama ntilie tu kuuza chapati mwingine mihogo au maharage mtaa mmoja hawapatani sembuse Machinga
Dawa ni kuwatoa wakatafute mbali na maduka ya wenzao wanauza vifaa vya electronics, au vya umeme huwezi weka Wamachinga
 
Yaani Samia inabidi akomae watu waondoke huko mabarabarani..kuna mmoja leo nimemsikia anasema amekopa 15m lakini biashara anafanya katikati barabarani kwenye kibanda cha maturubai..kama sio ujuha kuendelea kuwaacha hawa watu ni nini?..
Huyo ni mkwepaji Kodi mzuri unawezaje kuchukua mkopo wa million 15 alafu unafanya biashara kwenye kibanda Cha maturubai
 
Vingunguti Scania
Kata Kiwalani Dar es Salaam
Tanzania

WAMACHINGA WAANZA KUTII AMRI, WAPANGWE UPYA

Sasa wapita kwa miguu wanatembea katika maeneo yao bila hatari ya kugongwa na magari. Kuvunjwa kwa vibanda mji unaanza kurudisha sura yake na pia usalama waongezeka. Shukrani ziuwendee uongozi wa mkoa chini ya RC Amos Makala na timu yake kwa uthubutu.

Machinga walia kwa kulaani hatua hiyo, lakini hawajali hali na haki za wakaazi wengine wa jiji hili maarufu la Dar es Salaam.
 
WAMACHINGA WAPANGIWA MFUMO MZURI WA KUWAPANGA, JIJI LIENDELEE KUWA SAFI NA SALAMA

Machinga kuondolewa Dar, Uongozi wa jiji watoa TAMKO la jinsi machinga wajipange ili kuwezesha usalama wa wapita njia pia ukusanyaji taka ktk barabara kuu kuu kufanyika bila vikwazo
 
MACHINGA COMPLEX DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo amekutana na wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex na kusikiliza kero zao, wapate mazingira salama ya shughuli zao na wateja wao huku jiji letu likiendelea kurudisha hadhi yake ya usafi , usalama kwa watu bidhaa na kanuni kufuatwa za jinsi ya kuendesha biashara ndogo a.k.a umachinga, mamantilie, gereji n.k

Back
Top Bottom