Machinga wapangwe kwa utaratibu

kingsila

New Member
Oct 21, 2017
1
4
Machinga Hayati Mh. Rais aliwapenda na kuwapa Uhuru wa kufanya kazi zenu ila mmekuwa kero kwa watumiaji wengine wa mihundombinu.

Tukianza na mifano ya wamachinga waliopo maeneo ya kariakoo,mtaa ya msimbazi,Congo na mitaa mingine ya kariakoo.

Mnatumia Uhuru wenu vibaya inafikia maali mpaka watembea kwa miguu wanapata shida kutembea kwajiri yenu nyie, jaribuni kujitengenezea utaratibu wa kujiongoza na kuheshimu watu wengine wenye matumizi na hiyo miundo mbinu.

Upande mwingine ni waendesha bodaboda nyie pia mmekuwa kero kwenye vituo vya daladala mnafanya magari na watu wanashindwa kutumia kituo kwa amanin, maana mmeweka pikipiki zenu mpaka kwenye sehemu ya kupaki gari.
 
Katika mambo ambayo yalikuwa yakinikera katika majiji ni utaratibu wa hovyo wa hao Machinga

Yaani watembea kwa miguu hukosa hata sehemu ya kukanyaga kisa wapiga kura

Hakuna anaye wazuwiya kufanya biashara lakini wawe kwa mpangilio na maeneo maalumu

Mh Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete pana lile jengo pale Machinga Complex alijitahidi lakini baadhi ya viongozi pia mfano hapo Dar es Salaam Kariakoo waliwaondosha kwa kipindi kifupi mji ulipendeza na mpangilio ukaonekana

Sasa pakaingia utaratibu wa kuzibana macho na akili ili tu ionekane wanahurumiwa sana na wanatetewa wakaruhusiwa kufanya biashara popote kwa kigezo cha wanyonge na kitambulisho cha 20000.

Pale tunapoona mabaya tukubali kukosolewa na kwenye mazuri tusifie si kila kitu ni sahihi kwa sababu tu kimeamuliwa na fulani hapana.
 
Hao wote ni wa kutoa.....!!! Yaani Taifa limekuwa kama la nguruwe mwitu , sio lazima machinga awepo kila chaka , machaka mengine hayawahusu
Ulioona wale watu walioongia Airport kumsindikiza Magufuli... Wale ndio waitoa Serikali madarakani...

Ole wa Serikali itakayokurupuka kuwatoa... Wanakila Sababu ya kuandamana
 
Hawa ni watu wa kuwatoa kwa umakini...wakiandamana wale wanaweza angusha serikali. Maana hawana cha kupoteza wanajijua wao ni maskini... kwa rais mjanja lazima awatoe kisiasa kama hawezi kuwadekeza kama rais aliepita
 
Ulioona wale watu walioongia Airport kumsindikiza Magufuli... Wale ndio waitoa Serikali madarakani...

Ole wa Serikali itakayokurupuka kuwatoa... Wanakila Sababu ya kuandamana
Wapewe notice ya kuondoka hayo maeneo waende maeneo elekezi , hawa watu walikuwa reference ya Maghufuli ya kuwadharau wasomi et wajiajiri .... Maghufuli katengeneza Taifa la hovyo Sana
 
Katika mambo ambayo yalikuwa yakinikera katika majiji ni utaratibu wa hovyo wa hao Machinga

Yaani watembea kwa miguu hukosa hata sehemu ya kukanyaga kisa wapiga kura

Hakuna anaye wazuwiya kufanya biashara lakini wawe kwa mpangilio na maeneo maalumu

Mh Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete pana lile jengo pale Machinga Complex alijitahidi lakini baadhi ya viongozi pia mfano hapo Dar es Salaam Kariakoo waliwaondosha kwa kipindi kifupi mji ulipendeza na mpangilio ukaonekana

Sasa pakaingia utaratibu wa kuzibana macho na akili ili tu ionekane wanahurumiwa sana na wanatetewa wakaruhusiwa kufanya biashara popote kwa kigezo cha wanyonge na kitambulisho cha 20000.

Pale tunapoona mabaya tukubali kukosolewa na kwenye mazuri tusifie si kila kitu ni sahihi kwa sababu tu kimeamuliwa na fulani hapana.
Kwa kweli naamini hakuna nchi isiyo na utaratibu. Hata ktk nyumba binafsi kuna mpangilio. Hawa wapewe maeneo maalumu ili wasizagae kila kona
 
Wapewe notice ya kuondoka hayo maeneo waende maeneo elekezi , hawa watu walikuwa reference ya Maghufuli ya kuwadharau wasomi et wajiajiri .... Maghufuli katengeneza Taifa la hovyo Sana
Kwa hiyo wasomi hawatakiwi kujiajiri

Umenipa cha kutafakari usiku huu
 
Ulioona wale watu walioongia Airport kumsindikiza Magufuli... Wale ndio waitoa Serikali madarakani...

Ole wa Serikali itakayokurupuka kuwatoa... Wanakila Sababu ya kuandamana
mkuu wanabahati kulikua na msiba pale pembeni kuna kambi ya jeshi wangetumwa vijana kuwashugulikia kila mtu angejua njia ya kutokea
 
Back
Top Bottom