Kaisari
JF-Expert Member
- Nov 13, 2012
- 3,636
- 3,042
Katika pitapita zangu mtaani hasa kule Kariakoo, nimeona adha kubwa sana wanayokumbana nayo watembea kwa mguu. Hii hasa ikanisukuma kuandika hapa. Na bado najiuliza sijui nimwandikie barua ya kumshauri. Namba moja atengue kauli.
Ukitazama hawa jamaa zetu wanaopanga bidhaa barabarani kwa kweli imekuwa kero kubwa sana kwa wapitanjia. Maana hata sehemu ya kupita inakosekana kwa inawezekana kukanyaga bidhaa zao ikawa ugomvi.
Sidhani kama tutakuwa tunajenga taifa la wazalishaji naona tunajenga taifa la wachuuzi kwa mtazamo wangu natia shaka kama hawa jamaa wanalipa kodi. Maana sijaona mtu akinunua akapewa receipt.
Zaidi sana naoata shaka kama hapatatokea mzozo na wale jamaa wenye maduka yao ambao wanalipa kodi ya pango, kodi ya mapato, umeme , takataka, nk halafu anatokea watu wanaweka bidhaa hapo nje wanauza hali wakikwamisha wateja kuingia dukani.
Hata kama tunatengeneza ajira nina shaka kama hii ni aina ya ajira tulitarajia. Kwa maana utakuta wengine wamechoka wamelala usingizi na bidhaa zao. Ni mtazamo wangu.
Kama namba moja anapita humu basi alione hili jwa jicho lingine na sio vibaya akitengua kauli. "(Mbona kawaida tuu tuliisha sikia nilishauriwa vibaya)". Tengua tuu kauli ili hali iwe sawia
Na hata kwa wawndesha magari ni shida sana sana kupita na gari. Kwa sisi hatujazoea fujo na makelele tunaacha magari mbali. Huku ukijihami kuchomolewa kilichomo mfukoni. Na simu unazishikilia mkononi kwa nguvu.
Vinginevyo watengeeni barabara zao rasmi wajimwage huko magari yasipite kamwe. Na sisi ambao hatuna shughuli nao basi hatutapita huko mpaka siku nikiwa na shughuli nao.
Kama namba moja hapiti humu basi nyie mlio karibu naye mwambieni yanayotusibu huku.