Machinga ni yupi?

uncle

JF-Expert Member
Dec 10, 2007
322
184
Machinga ni yupi?

Nimeanza na swali baada ya kuona post ya mdau akielezea athari za kiuchumi baada ya machinga kuondolewa katikati ya jiji na mikoa mengi au hapa miweke sawa kwa lugha ya Rais wetu kuwapanga wamachinga toka sehemu isiyo kuwa rasmi kuwapeleka sehemu rasmi sasa hapo kutokana na hiyo mada ya mdau najiuliza nani haswa mmachinga. Maana anazungumzia kuna wengine walipewa mpaka mikopo na mabenki.

Nazidi kijiuliza kweli sasa huyu ni machinga tena sababu kwa uelewa wangu mdogo nilijua machinga ni wachuuzi wadogo wadogo wanauza vitu kwa kuhamahama kufuatana na fursa au lugha ya kigeni street hawkers sasa hii ya kupatiwa mpaka mikopo tena inaniacha na maswali mengi. Machinga ni yupi?
 
Neno Machinga Lina uhusiano na wamakonde kutoka mkoa wa Mtwara kwani miaka ya 19 kwa wingi wao walihamia mkoa wa Dsm hasa mtaa wa kongo wakijihusiha na biashara ndogo ndogo kama vile kuuza mifuko ya plastiki aka Rambo , walikuwa na umoja na kubebana sana kuanzia kibaruani mpaka kwenye malazi.

Kwenye chumba kimoja walikuwa wanalala mpaka kumi na kwa mama LISHE walikuwa wakienda kikundi wakinunua ukoko na maharage na kudanganya tumbo. Walikuwa hawana mitaji zaidi ya uaminifu kwenye maduka ya jumla.

Baada ya muda wakaanza kuonekana mtaani wakitembea kama enka wakiwa na bidhaa ndogondogo kuanzia sufuria, nguo za Bei rahisi na viatu.

Asili ya wamachinga hawa hawana wajualo kuhusu mikopo, hawa huwa wanahitaji sehemu ya kufanyia biashara
 
Waliojaa na kujaza mabanda road au barabarani no wenye maduka ambao hawataki kulipa kodi..chingaz hawana haha ya kuwa na kibanda road. So wapigwe tu
 
Kwa sisi tuliyozaliwa ocean Road
Wamachinga wanakuja wanaanza
Biashara tulibahatika waona enzi hizo
Mmachinga walikuwa wanauza bidhaa
Zao kwa kutembeza tu,huyo ndiyo
Mmachinga,nmemkumbuka mzee chinganga

Ova
 
Cha ajabu wale tuliowaita machinga waliovunjiwa vibanda wapo kwenye maduka kama masoko ya kisutu na kwingineko hivyo kumbe umachinga ilikuwa plan b yao kukwepa kodi
 
Back
Top Bottom