Rais Magufuli na karata ya machinga kuelekea 2020

Webb

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
425
883
Wakuu huu mpango wa kuwathamini Machinga sio wa bahati mbaya.Hii ni karata kubwa kisiasa hasa kwa chama kilichochokwa na wananchi.

Watu wanajiuliza WHY Machinga?

(1) Population ya vijana wengi hasa mijini ni Machinga.

(2)HII NDIO POINT KUU

Watu wanasema Watanzania ni waoga,hasa katika mambo ya kudai haki tena hikihusisha MAANDAMANO.Na huo ndio ukweli

Kwanini watu ni waoga kuandamana kudai haki?.Wengi watakujibu kuwa "Tuache kutafuta ugali wa watoto tukaandamane,wapi".

Apa Tanzania watu wenye uthubutu wa kuandamana na kujitoa kwa 100% kudai haki ni MACHINGA pekee.

Machinga haogopi mabomu wala Segerea kwa sababu tayari kaishakosa haki yake ya kutafuta ridhiki,kwahiyo anajitoa muhanga kwa ajili ya familia yake.

Hii ni tofauti na sekta nyingine,mtu aandamane wakati ana uhakika na mwisho wa mwezi.

Magufuri anaitumia hii kete vizuri ili mwaka 2020 baada ya kujitangazia USHINDI,atawambia Machinga waendelee kuchapa kazi wasisikilize porojo za wapinzani.

Eti waandamane,wakati wameshapewa uhuru wa kufanya biashara,NEVER.

Narudia hakuna mtu wa kuingia road zaidi ya machinga,hata kule Mwanza na Arusha enzi za Slaa Machinga ndio waliokua wanaongoza zile harakati za maandamano.

2020 twende na......
 
Mzee huyu kaona hapa njia pekee ya kuwarubuni machinga ni kuwaambia eti anawapa vitambulisho,

Kwanini visiwe vitambulisho vya kawaida, mfano kama vya kumtambulisha mkazi au aina nyingine mpaka viwe connected na TRA? Kwanini visitolewe na halmashauri au wizara ya viwanda na biashara ila atoe Magufuli kuputia mlango wa TRA?

Kwa sasa kitambulisho mmekipata kwa 20,000 hiyo ni Invitation to treat ,

Hivo mtavilipia mpaka 200,000 ,kwa Muda unaokuja hasa mwakani, na imeshatambulika kuwa huwa una kitambulisho, na kina mama lishe woote mtalipa

Nanukuu "Hakuna kumsumbua machinga au mama lishe mwenye kitambulisho hiki"

Alafu wakashangilia, yaan kwa logic ya kawaida ni kwamba wasiokuwa navyo wasumbuliwe, hivo ipo siku kitauzwa laki 4 lazima awe nacho kuepuka kusumbuliwa na mgambo, haya

Shangilieni
 
Mzee huyu kaona hapa njia pekee ya kuwarubuni machinga ni kuwaambia eti anawapa vitambulisho,

Kwanini visiwe vitambulisho vya kawaida, mfano kama vya kumtambulisha mkazi au aina nyingine mpaka viwe connected na TRA? Kwanini visitolewe na halmashauri au wizara ya viwanda na biashara ila atoe Magufuli kuputia mlango wa TRA?

Kwa sasa kitambulisho mmekipata kwa 20,000 hiyo ni Invitation to treaty ,

Hivo mtavilipia mpaka 200,000 ,kwa Muda unaokuja hasa mwakani, na imeshatambulika kuwa huwa una kitambulisho, na kina mama lishe woote mtalipa

Nanukuu "Hakuna kumsumbua machinga au mama lishe mwenye kitambulisho hiki"

Alafu wakashangilia, yaan kwa logic ya kawaida ni kwamba wasiokuwa navyo wasumbuliwe, hivo ipo siku kitauzwa laki 4 lazima awe nacho kuepuka kusumbuliwa na mgambo, haya

Shangilieni
Invitation to treat! Nimekupa kitambulisho, are there clearer term for an offer to be implicated/implied? are there clear intention to bind? Mimi sijui, ila Wamachinga /wafanyabiashara mama ntilie muwe macho! We are in a lawlessness society!
 
Ungesema wakulima wa korosho nao wapewe ningekuelewa. Na wa mbaazi, miwa, wachimbaji madini, wavuvi, wafugaji wa mbuzi. Lakini pia mafundi wa simu,charahani, mbao, chuma, koroboi, baiskeli, viatu, nywele, kucha, rangi; mpaka ma emu si!
Hao wote ni wajasiliamali.
 
rais wetu wa wanyonge kaja na kodi mpya japo hataki kuipamba kama kodi yeye anaita vitambulisho. kwa hakika hii ni kodi mpya!! tena kodi inayoenda kwa wale anaowaita wanyonge.

hii ni kodi ya kichwa kama iliyokuwepo hapo zaman kwa wazazi wetu. rais wetu anaona wivu raia wake wakipata riziki bila kulipa chochote direct serikalini. anasahau kodi ina njia nyingi sana za kulipwa. kila huduma ninayoipata nalipa kodi inderlect. ila yeye hajaona hilo anaona tunaishi bure katika nchi yetu wenyewe.

kwa wale wanaofurahia hii kodi mpya mtakuja kujuta huko mbele. italeta usumbufu mkubwa sana kwa raia wenye kipato kidogo. mtaji wa kuuza karanga haufiki 20,000 lakn watataka nilipe 20. mtaji wa kuuza maji ni nguvu zako watataka nilipie nguvu zangu.

na tukifurahia wamachinga kuanza kulipa kodi tukidhani sisi haituhusu tunakosea. tujue na sisi anatufikilia namna ya kutukamua

ni huyo mimi muuza karanga hii kodi inanihusu.

ni huyo mimi muuza maji ya kandoro hii kodi inanihusu.

ni huyo mimi mtembeza viatu hii kodi inanihusu

ni huyo mimi mama ntilie muuza wali kwenye vumbi kodi hii inanihusu

ni huyo mimi muuza maembe kwa baisker kodi hii inanihusu.

ni huyo mm muuza kahawa kikombe 100 hii kodi inanihusu

aisee rais wa wanyonge ama kweli unaenda kutunyonga!!

haya migambo na polisi ajira hiyo hapo futeni virungu njoon kutukimbiza kwa amri ya rais wa wanyonge
 
Lipeni kodi nyie sisi watu tunakatwa paye, na kodi nyingine kwanini nyie msilipe? Wote sisi si watanzania mlipe kodi tuijenge nchi sote si kuonewa sisi wafanyakazi tu.
 
Hii nchi ina majuha wengi sana. Mijitu inaweza kushangilia hata ujinga bila kujua madhara yake.
 
Naam habari za uhakika ni kuwa wale machinga wanaopiga domo kukosoa, wapinga kila kitu na ambao siyo wazalendo kwa nchi yao wametakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani katu hawatopewa vitambulisho vilivyotolewa kwa ajili yao.

Aidha ili kuwa na uhakika wa kupata kitambulisho hicho basi uwe na kadi ya CCM.

#TeamWanaotumiwaNaMabeberu tutapata tabu sana!

Nasikia huko Mbeya mkuu wa mkoa ndugu Chalamila tayari anayo orodha ambayo hao katu hawatoonja ladha ya vitambulisho vya JPM.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom