Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
SAKATA la kuondolewa kwa wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga katika mengi nchini, kwa sasa limezua hali ya ukosefu wa amani kwa machinga hao jijini Dar es salaam.
Uamuzi huo umejaribiwa kutekelezwa karibu kila mkoa nchini lakini kwa kiasi kikubwa umekuwa ukijaribiwa sana katika Jiji la Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.
Operesheni ya kuwahamisha na kuwamata wamachinga jijini Dar es Salaam imeongeza kasi ikiwa ni muda mfupi tangu wafanyabiashara hao walipoamriwa kuondoka pembezoni mwa maeneo ya barabara mpya za mwendo kasi, hali ambayo imesababisha msongamano katika eneo moja huku wizi ukipamba moto kutokana na msongamano mkubwa wa watu katika eneo dogo.
Soma zaidi hapa => Machinga: Hatuwezi kuhamia sehemu isiyo na mazingira ya kutengeneza faida | Fikra Pevu