Machinga Complex, Stendi Ubungo/Mwenge na Soko la kufikirika Mbezi.....

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Nimeliita soko la kufikirika Mbezi (Mbezi Luis) kwa sababu nimeona pale panajengwa kituo kikubwa cha daladala lakini nilipoangaza sikuona sehemu ya soko. Pengine mtanishangaa kwa nini stendi iambatane na soko. Ni uzoefu wangu katika vituo vya daladala ninavyotumia kila siku. Pale Ubungo jioni hapatoshi na Mwenge hapapitiki. kila aina ya biashara kwa matumizi ya nyumbani hupatikana pale. Wakati mwingine hadi saa 4 usiku taona taa za mchina, solar na vibatari vikiangaza. Hii inaashiria kuwa, watu wa Dar watafanya shoping yao karibu na vituo vya usafiri. Mara kadhaa napita maeneo ya Karume pale kwenye soko kubwa kwa majengo pengine ni kubwa kuliko hata Kariakoo. Lakini hakuna daladala zenye kusimama pale hivyo hakuna wateja. Saa 12 jioni panakuwa tayari pamechacha. Ninajiuliza sana, hivi watu wa mipango hufuata tu ufundi wa kitabuni bila kuzingatia na hali halisi ya maisha ya watu? Niliwahi kushuhudia pia soko la Makumbusho likiwa tupu kipindi cha nyuma, kwa sababu ya uhaba wa watu. Watu wapo karibu na sehemu za usafiri. Ni katika tafakari hii ninajenga soko la kufikirika pale Mbezi ambalo kama serikali ya jiji haitalijenga, basi wananchi watalijenga bila mpangilio wowote. Penye watu ndipo penye pesa.
 
mkuu you have a very good idea. yaani ishu ya machinga complex ni aibu tupu.

Wamachinga hawakuhitaji investment kubwa namna ile, walihitaji kitu simple kama soko la samaki 'feri' lakini kwa sehemu nyingi ambazo kuna watu na huduma zinazoshabihiana.
 
Ulaji huo!Wapi papa Meya wa Ilala,Meya wa DSM,papa Mbunge wa Ilala..mmmh hapo ni bolingo na ngai au makilikili?
 
Nimeliita soko la kufikirika Mbezi (Mbezi Luis) kwa sababu nimeona pale panajengwa kituo kikubwa cha daladala lakini nilipoangaza sikuona sehemu ya soko. Pengine mtanishangaa kwa nini stendi iambatane na soko. Ni uzoefu wangu katika vituo vya daladala ninavyotumia kila siku. Pale Ubungo jioni hapatoshi na Mwenge hapapitiki. kila aina ya biashara kwa matumizi ya nyumbani hupatikana pale. Wakati mwingine hadi saa 4 usiku taona taa za mchina, solar na vibatari vikiangaza. Hii inaashiria kuwa, watu wa Dar watafanya shoping yao karibu na vituo vya usafiri. Mara kadhaa napita maeneo ya Karume pale kwenye soko kubwa kwa majengo pengine ni kubwa kuliko hata Kariakoo. Lakini hakuna daladala zenye kusimama pale hivyo hakuna wateja. Saa 12 jioni panakuwa tayari pamechacha. Ninajiuliza sana, hivi watu wa mipango hufuata tu ufundi wa kitabuni bila kuzingatia na hali halisi ya maisha ya watu? Niliwahi kushuhudia pia soko la Makumbusho likiwa tupu kipindi cha nyuma, kwa sababu ya uhaba wa watu. Watu wapo karibu na sehemu za usafiri. Ni katika tafakari hii ninajenga soko la kufikirika pale Mbezi ambalo kama serikali ya jiji haitalijenga, basi wananchi watalijenga bila mpangilio wowote. Penye watu ndipo penye pesa.

mkuu tatizo ya hizi project hazifanyiwi realistic project appraisal, wataalam wapo lakini naona au wanazembea au la utaalam hautoshi
 
Back
Top Bottom