Crucifix
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 1,651
- 588
Nimeliita soko la kufikirika Mbezi (Mbezi Luis) kwa sababu nimeona pale panajengwa kituo kikubwa cha daladala lakini nilipoangaza sikuona sehemu ya soko. Pengine mtanishangaa kwa nini stendi iambatane na soko. Ni uzoefu wangu katika vituo vya daladala ninavyotumia kila siku. Pale Ubungo jioni hapatoshi na Mwenge hapapitiki. kila aina ya biashara kwa matumizi ya nyumbani hupatikana pale. Wakati mwingine hadi saa 4 usiku taona taa za mchina, solar na vibatari vikiangaza. Hii inaashiria kuwa, watu wa Dar watafanya shoping yao karibu na vituo vya usafiri. Mara kadhaa napita maeneo ya Karume pale kwenye soko kubwa kwa majengo pengine ni kubwa kuliko hata Kariakoo. Lakini hakuna daladala zenye kusimama pale hivyo hakuna wateja. Saa 12 jioni panakuwa tayari pamechacha. Ninajiuliza sana, hivi watu wa mipango hufuata tu ufundi wa kitabuni bila kuzingatia na hali halisi ya maisha ya watu? Niliwahi kushuhudia pia soko la Makumbusho likiwa tupu kipindi cha nyuma, kwa sababu ya uhaba wa watu. Watu wapo karibu na sehemu za usafiri. Ni katika tafakari hii ninajenga soko la kufikirika pale Mbezi ambalo kama serikali ya jiji haitalijenga, basi wananchi watalijenga bila mpangilio wowote. Penye watu ndipo penye pesa.