Nakadori

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,781
20,946
Wapendwa week end inaendaje?
Wanasema kizuri kula na mwenzako....na nomeona niwashirikishe fursa hii adimu hasa kwa wale wanaofika kariakoo na kujikuta wanauziwa bei ghali kuliko hata huku mtaani...

SOMA HAPO UKIPENDA SAWA USIPOPENDA PITA KIMYA

Ngoja nikupe machimbo eh best kizuri kula na mwenzio...Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule mnazi mmoja wengi wanaouza k.koo wanaenda kufata huko,

Viatu navyo vinapatikana huu mtaa wa Narung'ombe na congo pale nenda straight kwenye maduka ya wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini nop unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile visandles wanauza 2500/pc.

Cheni zama mchikichi katikati kuna mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki.

Magauni nayo ingia ndanindani kule congo na aggrey wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc.

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro.

Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau?

Mapazia ya kukata jora Kama unaenda Posta upande wa chuo cha DIT na CBE, Ukishavuka ule ukuta kuna duka la mfanyabiashara ana asili ya india anauza bei nzuri na mara nyingi Jumamos anakua na bei ya SALE kwahyo unaweza kupata majora ya mapazia kwa bei chee na kila design.

NA UKITAKA DAGAA ZA KUKAANGA FRESH KABISA KUTOKA MWANZA YANI KUTOKA ZIWANI STRAIGHT KWA MLAJI UTAZIPATA KWA HUYU HAPA 0654688288

NATUMAIN MTAKUJA NA MACHIMBO MENGINE SEMENI HAPA. copy and paste
 
Wapendwa week end inaendaje?
Wanasema kizuri kula na mwenzako....na nomeona niwashirikishe fursa hii adimu hasa kwa wale wanaofika kariakoo na kujikuta wanauziwa bei ghali kuliko hata huku mtaani...

SOMA HAPO UKIPENDA SAWA USIPOPENDA PITA KIMYA
Asante kwa uzi mzuri, na kwa rim papers bei rahisi napata wapi kkoo hapo. Tunaruhusiwa ku share kwa anaejua please.
 
Shukrani sana

Na vipi zile rasta na ma weaving ambayo yanauzwa kwa bei ya sale?

Nishawahi sikia kuwa huwa wakishusha mzigo mpya ule wa zamani huwa wanautoa na kuuza kwa bei ya sale
 
Wajasiriamali mjeee msijesema hakuna ajira....ajira hizo hapooo
Na machimbo ya( PPE's),
Yaani vitu hivi yako wapi kwa hapo kariakoo mkuu....??

gloves,
helmet,
Overall
Ear plug
Dust mask
Safety glass,
Safety boots
Cutting disc
Drill machine
Welding shield,
Angle grinders
Air compressors
safety harness belt,


Vifaa vya usalama na kazi mahala pa kazi kama Workshops na Mining areas vinauzwa wapi kwa hapo kariakoo mkuu???
 
Na machimbo ya( PPE's),
Yaani vitu hivi yako wapi kwa hapo kariakoo mkuu....??

gloves,
helmet,
Overall
Ear plug
Dust mask
Safety glass,
Safety boots
Cutting disc
Drill machine
Welding shield,
Angle grinders
Air compressors
safety harness belt,


Vifaa vya usalama na kazi mahala pa kazi kama Workshops na Mining areas vinauzwa wapi kwa hapo kariakoo mkuu???
Mimi sijui mitaa so siwezi kukuelekeza uende mtaa gani, ila nikivifuata najua wapi navipata.
 
Back
Top Bottom