Machimbo mapya ya dhahabu Iringa tayari yashakula watu wawili

LUBEDE

JF-Expert Member
May 7, 2013
4,320
6,677
Kwa mujibu wa taarifa zenye uhakika inasemekana haya machimbo mapya ya dhahabu huko Iringa yashapoteza uhai wa Watanzania wenzetu wawili.

Hivi serikali huwaga haina mfumo au mpangilio maalumu kwa sehemu zenye mikusanyiko ya watu kama hivi?

Zifuatazo ni baadhi ya picha za hayo machimbo mapya ambayo nasikia yamebainika kama wiki tatu zilizopita lakini tayari kuna idadi kubwa ya raia kutoka sehemu mbalimbali nchini, Wasukuma wakiongoza kwa idadi.

IMG-20170516-WA0007.jpg
IMG-20170516-WA0009.jpg
IMG-20170516-WA0007.jpg
IMG-20170516-WA0009.jpg
IMG-20170516-WA0014.jpg
IMG-20170516-WA0015.jpg
IMG-20170517-WA0003.jpg
IMG-20170517-WA0004.jpg
IMG-20170517-WA0007.jpg
IMG-20170516-WA0013.jpg
IMG-20170519-WA00221.jpg
 
Huo uchimbaji wao ni halali?
Ukiangalia hivyo vitendea kazi vinatia shaka!
Yaani kama inayotumika nyembamba kiasi hicho!
Duuuuu
 
Hongera Iringa kwa dhahabu,sasa hpa serikali itoe mafunzo maalum kuzuia majanga haya.
 
Serikali ikiyafungia hayo machimbo najua utakuwa wakwanza kuja hapa kulalamika mkuu
 
Baada ya wiki mbili utasikia hili ni eneo la mwekezaji, yaani hii nchi inachekesha sana
Unaijua PML ndugu, yani unaweza chukua mining licence kwa eneo ambalo sio lako, ila kabla ya kuanza shuguli za uchimbaji ni lazima uwacompasate wenye maeneo yao
 
kwa mujibu wa taarifa zenye uhakika inasemekana haya machimbo mapya ya dhahabu huko iringa yashapoteza uhai wa watanzania wenzetu wawili,hivi serikali huwaga haina mfumo au mpangilio maalumu kwa sehemu zenye mikusanyiko ya watu kama hivi?
zifuatazo ni baadhi ya picha za hayo machimbo mapya ambayo nasikia yamebainika kama wiki tatu zilizopita lakini tayri kuna idadi kubwa ya raia kutoka sehemu mbalimbali nchini,wasukumu wakiongoza kwa idadi.. View attachment 511858 View attachment 511861 View attachment 511858 View attachment 511861 View attachment 511867 View attachment 511868 View attachment 511869 View attachment 511870 View attachment 511871 View attachment 511872 View attachment 511873
Haya machimbo yapo wapi huko iringa
 
Unaijua PML ndugu, yani unaweza chukua mining licence kwa eneo ambalo sio lako, ila kabla ya kuanza shuguli za uchimbaji ni lazima uwacompasate wenye maeneo yao
PML ni Primary Mining License ni kwa ajili ya mzawa tu, ila ML ni mining License kwa wote. Huwezikuchukua ML ikiwa tayari eneo lina PML, labda huyo mtu akuuzie eneo.
 
Baada ya wiki mbili utasikia hili ni eneo la mwekezaji, yaani hii nchi inachekesha sana

Sio kuchekesha, nchi nzima kuna blocks za watu za madini tofautitofauti, kuna Dhahabu, heavy metal, gemstone, coal, natural gas, building materials nk, so nivizuri hata wewe kabla hujaanza kazi yoyote ya Madini, hata kama kuchimba kokoto lazima ujiridhishe kuwa hilo eneo sio la mtu na unatakiwa ufanye process ya vibali

Kwenye ramani ya madini ya Tanzania nzima kuna maelezo ya kila eneo lina madini gani, so hata hapo utakuta ni eneo la mtu na huwa analilipia kila mwaka, hao ni wavamizi tu ndio maana wako hapo na makeshift sherters akija mwenye eneo wana haki ya kutoka

Na hiyo sio Tanzania tu ni Dunia nzima, miezi kadhaa tuliona Watanzania wakifukuzwa nchini Msumbiji kwa sababu ya kwenda kuvuna madini kwenye maeneo ya watu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
PML ni Primary Mining License ni kwa ajili ya mzawa tu, ila ML ni mining License kwa wote. Huwezikuchukua ML ikiwa tayari eneo lina PML, labda huyo mtu akuuzie eneo.
Issue ni kwamba wabongo hatuendi chukua hata hiyo PML, ndio maana mjanja mmoja akigutuka kwamba eneo lina madini na halina license analiombea fasta, kinachofuata ni mgogogor as mwananchi atasema yeye ndie katangulia kwa juhudi zake mwenyewe, wakati mwekezaji ndio ana kibali na madini ya eneo husika.
 
Back
Top Bottom