Machifu wa Mkoa wa Mbeya walaani mauaji ya John Mwankenja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machifu wa Mkoa wa Mbeya walaani mauaji ya John Mwankenja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, May 26, 2011.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Machifu zaidi ya wanane wamekutana nyumbani kwa Mzee Anyelwisye Mwankenja, baba yake na John Mwankenja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe, aliyeuwawa wiki iliyopita.
  Pamoja na kumpa pole Mzee Mwankenja ,machifu hao wamelaani kitendo hicho cha kinyama na kutoa wito wa aliyehusika na kitendo hicho kujisalimisha kwa vyombo vya dola.
  Mzee Mwakenja vile vile ni chifu wa ukoo wa Mwankenja wa Kiwira

  Update

  Kati ya watuhumiwa, wawili tayari wameshapoteza maisha as of Dec 2012.
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wamanyafu si wakali wa ndumba? Wamroge huyo muuaji shughuli iishe
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,903
  Trophy Points: 280
  ndumbahaifanyi kazi kwenye vitu kama hivi
  ndumba mwana o akisoma au akipata mafanikio ndio inafanya kazi kumuua au wanamfanya awe chizi. si ni kweli wajameni?
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Gwakisa ebu toa utangulizi kidogo mimi binafsi sijui lolote juu ya hilo tukio!
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,426
  Trophy Points: 280
  Hao machifu hawana cha kufanya zaidi ya kumpa pole tu mwenzao, uchawi ungekuwa mwepesi hivyo CCM si wangeshamloga Slaa jinsi anavyowasumbua na kuwanyima usingizi.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu naona hukuwepo wiki iliyopita.
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe ambaye vile vile ni Diwani wa Kiwira na hatimaye kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe , aliuwawa na watu wasiojulikana usiku wa tarehe 19 May 2011.
  Wauaji hawakuchukua kutu chochote pamoja na marehemu kukutwa na hela mfukoni Tshs 300,000/= na bastola yake binafsi.
  Tukio hili kwa mazingira haya inaelekea lilipangwa na kutekelezwa na watu wanaomfahamu fika marehemu.
  Watu wanne wako mikononi mwa polisi wakisaidia uchunguzi wa mauaji hayo.
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana Mkuu, ni kweli sikuwepo wiki hiyo ingawa nilikuwa nachungulia na kutoka bila kukaa nilikuwa na majonzi na hasira sana juu ya swala la Tarime kwa hiyo kila nilipo jaribu kuchangia niliona kama nachangia kwa hasira sana hivyo nilijizua na kukaa pembeni maana sikuona kwanini Polisi wauwe raia na bado wakamate viongozi kiubabe kiasi hicho!

  Nashukuru kwa taarifa ingawa pia naomba kujua hao waliokamatwa ni watu aina gani? na kama ni watu wanaoeleweka, kazi zao, na uhusiano wowote na marehemu na kama kuna tetesi zozote za friction katika Halmashauri yao?
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Asante Mkuu , waliokamatwa siajsikia majina yao lakini ni watu walio kuwa karibu na eneo alilokuwa analoishi marehemu.Kitu cha kusikitisha ni kuwa marehemu hakuwa na historia ya uadui na mtu yeyote mbali ya siasa.
  Wanao hisiwa kuwa wauaji wake ni kutokana na wivu na tofauti za kisiasa.
  Kutokana na taarifa za magazeti J Mwankenja alipendwa sana na madiwani wenzake na hivyo kuchguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa zaidi ya vipindi viwili.
   
 9. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana Gwakisa; Mungu amurehemu ndugu yetu Mwankenja, ni kuchanganyikiwa kwa binadamu wasio nauwezo mbadala katika akili zao ndio uona kama kuuwa ndio jibu la kumshinda mwenzio wakati ni kweli kuwa unapo uwa unajimaliza wewe mwenyewe Duniani na Mbinguni.
   
 10. Edgartz

  Edgartz JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hahahaha mkuu hao wamanyafu ni wenyeji wa mkoa gani? Nilikuwa nawasikia zamani siku hizi naona kama kizazi chao kiliisha!
   
 11. N

  Nguto JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,657
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  RIP John! Mungu atalipiza kifo chako.
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu mimi siamini katika uchawi wala ndumba kwa vile ni kinyume na mapenzi ya Mungu.Lakini kwa jinsi ya wauaji walivyofanya mauaji haya kinyama na kilio kilichotokea pale Wilayani Rungwe na Mkoani Mbeya naamini Mungu atasikia kilio hiki na haki kutendeka.
  Ndugu zangu JF mimi nilikuwepo pale kilioni na majonzi yalikuwa mazito sana na hakuna kiongozi aliyekuwepo ambaye hakuguswa na hatimae kumwaga mchozi kwa tukio lile.
   
 13. 1

  19don JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  RIP john mwankenja
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ridhiwani alikuwepo? Naye si chifu wa wanyambala?

  https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/75716-ridhiwani-kikwete-atawazwa-kuwa-chifu-wa-wanyakyusa-4.html  [​IMG]
   
 15. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
 16. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
 17. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  Kikwete hakutilia maanani kifo cha huyu mzee badala akaenda kwa mganga wake wa majini sheikh yahaya...............
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
 19. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #19
  Dec 12, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kaika mauaji ya maerehemu John Mwankenja kuna watu walioyuhumiwa kuhusika.
  Kuna waliohusika na kupanga na waliohusika kuchagia fedha mpango huo.

  Tayari kwa hivi sasa kuna watu wawili wamekwisha kufa, na inasemekana walihusika moja kwa moja.

  Wa kwanza ni dereva wake Marehemu John Mwankenja, huyu dereva amefia jela alikokuwa rumande hata kabla kesi haijaanza kuikilizwa.

  Wa pli kafariki leo alfajiri na amezikwa jioni hii, hu ni dada wa pale Kiwira na inasemekana alishangilia kupita kiasi mauaji ya John.

  Wanyakyusa pale Tukuyu wanasema kweli Mungu anawalipiza.
   
 20. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Du!
  Hata Waingereza walisema "what goes around, comes around".
  Wanapanga mauaji ya binadamu mwenzao na kushangilia utafikiri walimtengeneza? au kwamba wao hawafi?
  Kweli Mungu si wa kuchezewa!
   
Loading...