Machangudoa ni poa na salama zaidi

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,419
2,270
Imedaiwa kuwa, idadi kubwa ya wanawake wanaotumia kondomu za kike, ni wale wanaofanya biashara ya kuuza miili yao (machangudoa), ambao wengi wameonyesha kuipokea elimu juu ya matumizi ya zana hiyo kwa furaha.

Hayo yamebainishwa na Bi.Janeth Shombe, mtoa huduma kutoka kampuni ya T.MARC ambayo inashughulika na utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya kondomu, usambazaji wa bidhaa hiyo nchini, na huduma nyingine zikiwemo za uzazi wa mpango.

``Unajua idadi kubwa ya wanawake bado hawatumii kondomu za kike ingawa elimu imetolewa kwa wingi...watumiaji wengi wa kondomu za kike ni madada poa (machangudoa), wao tuliwapa elimu na hali inaonyesha wameipokea kwa wingi, `` akasema Bi.Shombe.

Akasema, pamoja na hali hiyo T.MARC bado inaendelea kutoa elimu kwa wanawake kuhusiana na utumiaji wa kondomu hizo ambazo zinamsaidia kujiamini na kujiwekea usalama zaidi kwa afya yao.

Akizungumzia kuhusiana na uhaba wa kondomu za kike katika nyumba za wageni, alisema taarifa hizo zimeshawafikia na akasema tatizo hilo linashughulikiwa.

Hata hivyo Alasiri ilipojaribu kuongea na baadhi ya wanawake kadhaa Jijini kuhusiana na utumiaji wa kondomu za kike, walisema hawazitumii kwa kuwa zinaleta usumbufu wakati wa uvaaji.

Wengine walidai kuwa wanaona aibu kwenda kuzinunua kutoka kwenye maduka ya dawa.

``Mimi sijawahi hata kuiona kondomu ya kike,`` mama mmoja alidai.

Source: Alasiri
 
Aisee kweli kwa kiasi fulani, dadapoa wanaparactice hiyo kitu.watu wengi hudhani ukiwa kwenye relation uko 100% safe, na kwa dadapoas ndio ukimwi na magonjwa mengine ndio nyumbani kwake,kuna experience fulani katika boyfriend-girlfriend relationships, condoms huwa zinatumika ule muda wakati 'HAMJAZOEANA', ya kwanza, ya pili, ya tatu watu wanaanza 'barabara chuma gari chuma',halafu hata kama watu wanatumia condom ni kwa ajili ya kuzuia mimba tu. sio kwa ajili ya magonjwa eeh, maana watu wanaogopa mimba kuliko ukimwi (ingawa kuna 'MIMBA ZISIZOTARAJIWA KIBAO',meaning watu wanakula mjengo bare).got it, ila take care usione wametoa utafiti kwamba hao dadapoa wanatumia condom kwa kiasi kikubwa na hivyo ndio safe to a certain extent, ukaamua kujiachia anga hizo,Undertand it will be at your own risk.people Aids kills, at currently it is as near as your shadow.so stick to the ABC (Abstain,Be faithful, Condomize).
 
Ni kweli kuwa wakinadada machangu wanajilinda sana!! ukiangalia hata takwimu za HIV/AIDS karibu 50% ya waathirika ni watu walio ndani ya NDOA...
 
Ni kweli kuwa wakinadada machangu wanajilinda sana!! ukiangalia hata takwimu za HIV/AIDS karibu 50% ya waathirika ni watu walio ndani ya NDOA...

Mkuu hizi takwimu ni za lini? Tunaomba uziweke zote hapa ili tujue category ipi imeathirika sana na isaidiwe vipi ili isiangamie.

50%!!! Damn......
 
Wengine walidai kuwa wanaona aibu kwenda kuzinunua kutoka kwenye maduka ya dawa.

``Mimi sijawahi hata kuiona kondomu ya kike,`` mama mmoja alidai.[
QUOTE][/QUOTE]

Hiki ndicho kinacho wacost sana wanawake wengi....AIBU ndo maana ukifatilia sana idadi ya walio na VVU ni kubwa sana ya wanawake chanzo ni aibu anaona aibu kwenda dukani kununua apparatus...kazi kweli kweli.
 

Hiki ndicho kinacho wacost sana wanawake wengi....AIBU ndo maana ukifatilia sana idadi ya walio na VVU ni kubwa sana ya wanawake chanzo ni aibu anaona aibu kwenda dukani kununua apparatus...kazi kweli kweli.[/QUOTE]

Sasa apparatus ndio nini?.............si ndio aibu hizo.....hata we mwenyewe hapo kununua huwezi kama kutamka "condom"kwenyewe shida!

Kitu kingine....tusaidiane hapa na tuwe wa kweli....mumeo wa ndoa/mkeo wa ndoa.... kabla hamjaoana,mlipima mkaaminiana,kisha mkaoana....ni lini utaanza kuvaa condom baada ya hapo??????HILI NI TATIZO KUBWA SANA!Cha msingi wana ndoa tuwe waaminifu jamani.
 
Ni kweli kuwa wakinadada machangu wanajilinda sana!! ukiangalia hata takwimu za HIV/AIDS karibu 50% ya waathirika ni watu walio ndani ya NDOA...

Interesting...

Wala sitashangaa kwa sababu ninaelewa ugumu wa matumizi au kukubalika kwa Condom ndani ya ndoa...wanandoa hukumbana na vikwazo vingi ikiwemo na suala zima la kuhofia kuonekana si muaminifu au humwamini mwenzio......Mara nyingi wamama walioko ndani ya ngoa wanapodai matumizi ya mipita ya kiume hukumbana na maswali ya ...."una bwana nje eh? au 'huniamini siku hizi eh?' maswali ambayo huambatana na ugomvi.......but kwa dada poa ni unataka kubali hutaki chapa mwendo, wateja wamejaa kibao ka siti za daladala, ukishuka weye anakalia mwingine!! Kwao inakuwa rahisi kujicontrol!

Kuhusu Condom za Kike mie nadhani wasambazaji wenyewe bado hawajawezaufikia umma mkubwa..ukienda sehemu mbalimbali uliza kinga ya UKIMWI utaambiwa Salama, Rough Rider au Dume....sasa Condom ya kike inaitwa Dume?? Ni wazi wanahitajika kuongeza juhudi kuelimisha! Halafu pia kuna misconception even kwa waelimishaji wenyewe........nakumbuka kuna wakati walikuwa wakielimisha huku wakikazia mfano wa "Hata kama mumeo mlevi, mbishi kutumia kinga ukivaa..Care au Lady Pepeta" hatojua!! Wanasahau kuwa wanaume wanaogoma kutumia kinga si walevi peke yao!! Sasa mmama ambaye mumewe ni mbishi na pia si mlevi hatohamasika!!
 
Back
Top Bottom