Machali; wanafunzi waliofeli,wakakosa fursa ya kujiendeleza kielimu,watawafuata viongozi masaki.

sangu mnene

Member
Sep 5, 2012
92
35
Akichangia katika mjadala wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi, Mheshimiwa Mkosamali (Mbunge), amewalaumu viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge wa CCM kuwa, baada ya kusomeshwa bure na serikali ya Mwalimu Nyerere, wao
wamegeuka, wameanzisha matabaka, wanapeleka watoto wao shule binafsi maarufu kama 'English Medium', wanawaanzishia watoto wa walalahoi shule za kata zisizo na vitabu, walimu, maabara na madawati.

Kwa uzembe wao wamesababisha watoto wafeli na baadhi yao wanakuwa vibaka na machangudoa. Amedai shule binafsi zinamchukia sana Dr Ndalichako maana amezuia mitihani isivuje,"walizoea kuiba mitihani hawa,sasa Ndalichako kawabana,wanafeli vibaya, wanamtaka aje mwingine atakayekuwa tayari kuuza mitihani kwao". Amewaonya viongozi wa CCM kuwa siku zao zinahesabika."Ole wenu maana vijana mliowanyima elimu wanafahamu mnapoishi, si mnaishi Masaki, watawafuata hukohuko, hapo ndipo kutakapokuwepo kilio cha kusaga meno". Baadhi ya wabunge wamelaumu kauli hiyo ya Mkosamali na kuiita ya kichochezi.

Hivi wana JF;
1.Ninini hasa anachomaanisha Mkosamali? Je, ni kuwa yatawapata kama yaliyowapata mawaziri wa CCM wa Mtwara?
2.Je, viongozi wengi walionufaika na Elimu ya bure ya mwalimu, wanaishi Masaki na maeneo mengine mazuri?
3.Je, matokeo mabovu ya mitihani ya NECTA, yanastahili kubebeshwa viongozi wa Elimu na CCM?
4.Je, chuki ya vijana waliofeli ni kubwa kwa serikali kiasi cha kuwapa onyo viongozi wa CCM wanaoishi maeneo mazuri kama Masaki?
 
Ni kweli,umechanganya mkuu,yule anaitwa Felix Mkosamali,Mbunge mdogo kuliko wote wa kuchaguliwa(kama sio mdogo kuliko wabunge wote,i stand to be corrected)toka chama cha NCCR,jimbo la Muhambwe,mkoani Kigoma na ni mwanasheria kitaaluma.
 
Ni kweli,umechanganya mkuu,yule anaitwa Felix Mkosamali,Mbunge mdogo kuliko wote wa kuchaguliwa(kama sio mdogo kuliko wabunge wote,i stand to be corrected)toka chama cha NCCR,jimbo la Muhambwe,mkoani Kigoma na ni mwanasheria kitaaluma.

A point of correction. Mbunge mdogo kuliko wote ni Nassari, aliyezaliwa mwaka 1986, wakati Mkosamali amezaliwa mwaka 1984
 
mkuu MKOSAMALI AMESEMA UKWELI MTUPU KWANI NANI AJUI KUA WANAKAA MASAKI NA MIKOCHENI B.WATAFUATWA HUKO HUKO.
 
Unajua hata kitendo cha kulaumu vyama vinavyoendesha maandamano miaka hii, siku zijazo kutaisha.. Wananchi wataandamana bila vibali kupinga unyama huu.
 
Muda. Is mrefu watakiona alichokisema Mkosamali. This is a plain truth. Hili jeshi kitoka shule za kata ni kubwa sana. Tena jeshi ambalo ni half-baked. Whatever hao watu wa kada ya juu wana-enjoy wajue ni veey short lived. Wanajidanganya na mipasho na taarab za Komba ambaye hajui ni kwa nini yuko bungeni zaidi ya kulala.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom