Machafuko yanayotokea Libya na yaliyotokea Egipy mafundisho kwa viongozi wetu Tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machafuko yanayotokea Libya na yaliyotokea Egipy mafundisho kwa viongozi wetu Tz

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by silver25, Feb 25, 2011.

 1. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu Watanzania wenzangu, (munaopenda maendeleo ya nchi na musiopenda pia)
  Leo ninacho cha kushare na nyinyi kuhusu mwenendo mzima wa nchi yetu ya Amani na upendo, nimeamua kushare hivi kwasababu nimesha ona mbele nini kitatokea na nani atasababisha matokeo hayo, kuna mambo ambayo tuna takiwa tuwe nayo makini wakati tunaenda katika kuzijua haki za msingi kwa kila mwananchi, kwasababu kwa nchi zilizo endelea Matokeo yake tunayaona na nyingine kutokea Mapinduzi ya Aibu kwa Raisi ambaye wananchi walikuwa Wanamuamini kwa asilimia 100%

  Mfano ni Egipy, na Maandamano yanayoendelea huko nchini Libya.
  Haya yote yanatokana na Kutumia fursa ya Kuaminika kwa wananchi wake katika matumizi mabaya ya uongozi bila kujua kwanini wananchi wanamuamini.
  Watanzania baadhi sasa wanajua haki zao za kimsingi na ndio maana limezuka swala la katiba, Watanzania wa sasa ni wepesi kukubali kufanya Movement yeyote ya kimaandamano kama sababu ya Maandamano hayo ni yamsingi. lakini upande wapili ni tofauti, wakati wao wanafanya maandamano ya Halali na Amani wao wanayageuza maandamano hayo ni Range na Uwanja wa mazoezi wa kujifunzia kuattack fujo.

  Nina uhakika Mwalimu Julias Kambarage Nyerere angefunguliwa mbingu siku moja na mungu akayaona haya yanayo tendeka Tanzania angelia na chozi lake tungeliona, Kesi za mafisadi enzi zake hazikuwepo kwasababu yeye alizishughulikia hata kabla hazijafika kwa wananchi wake anaowapenda.
  Mara Mijadala ya kijinga na uchama, haikuwepo enzi zake,,

  Sasa naomba watanzania wenzangu tuweni makini na hali halisi ambayo inakuja hapo mbele, ninauhakika Watanzania wengi wakisha jua haki zao za msingi ni rahisi kuwapahakihizo na umuhimu wake kwa wachache ambao hawajazijua,

  Rai kwa viongozi
  Viongozi tumieni wakati huu kuwapatia haki wanayo stahili wananchi wenun kusije tikea machafuko, (hatujui hatima ya maandamano ya wananchi wa jimbo la segerea, na pingamizi la Mgombea ubunge kupitia chama cha Mapinduzi, kutoka kwa mgombea kupitia tiketi ya chama cha Cadema
  Itafikia hatua Wananchi watatumia nguvu katuka kudai haki zao
   
 2. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila likicho na mwanzo hakikosi mwisho mapinduzi yanakuja TZ nyie subirini Gadafi akipigwa chini nani anafuata
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Viongozi madikteta wa Afrika mwisho wao umefika wajiandae kuondolewa na nguvu ya umma.:rain:
   
 4. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya yote yanakuja Taratibuuu
   
 5. Qulfayaqul

  Qulfayaqul JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 471
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nadhani sasa hii ni athari za kuelimika, kila mmoja sasa anajua haki yake na kila mtu anajua pa kuidai, nafikiri hilo hata kikwete analijua sasa na jinsi umaarufu wake ulivyoshuka anajua lolote linaweza kutokea ameshaanza kuhihofia chadema sasa
   
 6. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi tuliyo kuwa nayo ni kupingana na Hotuba ya Raisi Kikwete inayo sema Wana chadema wanatishia Amani ya Nnchi,, Sasa Kikwete si awachukilie hatua?
   
Loading...