Machafuko ya Arusha yapo mahakamani yanajadiliwa lakini Dowans mahakamani haijadiliwi

Mlangaja

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
579
218
Nimeshangaa sana kusikia suala la machafuko ya Arusha yanajadiliwa wakati yapo mahakamani. Je tumeambiwa nini kuhusu Dowans? Ni ule msemo wa mkuki kwa nguruwe siyo.
Kweli mimi sielewi tunapelekwa wapi? Kwa nini viongozi wetu wameamua kutusaliti namna hii?
Naomba mnisaidie wana JF.
 
Nimeshangaa sana kusikia suala la machafuko ya Arusha yanajadiliwa wakati yapo mahakamani. Je tumeambiwa nini kuhusu Dowans? Ni ule msemo wa mkuki kwa nguruwe siyo.
Kweli mimi sielewi tunapelekwa wapi? Kwa nini viongozi wetu wameamua kutusaliti namna hii?
Naomba mnisaidie wana JF.
Kweli inabidi Wazri Mkuu na Spika wajibu maana hii ni double standard, kama DOWANS haijadiliwi Bungeni kwa kuwa swala hilo lipo mahakamani iweje maafa ya Arusha yajadiliwe Bungeni?????????????
Waziri Pinda na Spika ANNA tunahitaji majibu????????????
 
Hizi ndizo dalili za ulevi na hasa ulevi wa madaraka, huwezi kuwa thamini unao watawala unasema chote wakati wowote bila ya kutafakari, unawaona kama majuha, watakufanya nini.
 
Sasa je mahakama ikisema kwamba Chadema hawakusababisha machafuko je Waziri mkuu atasema nini? Nadhani ni wakati sasa viongozi wetu wanapaswa kujua kwamba kama kitu ni tete kiachiwe nguzo ya serikali ambayo inashughulikia kitu hicho. Kweli kilichofanyika hapa ni dharau fulani kwa muhimili wa serikali, yaani mahakama. Je legislator imekuwa judiciary? Na kwa nini wanataka kuingilia mihimili ya serikali? Hawajui mipaka yao siyo? Hivi wataendelea kutuongoza namna hii mpaka lini? Hawajifunzi siyo? Watanzania wa sasa si wa miaka ya katikati. Kwani naamini miaka ya hamsini na sitini serikali ilikuwa haifanyi hivi. Huu ni utamaduni uliojengeka siku za hapa katikati tu. Naomba wawe makini.
 
POINT!

Ni "standard practice" duniani kuwa jambo lolote linapokuwa ktk Mahakama ya Sheria huwezi tena kulijadili nje ya mhimili huo. Sasa kama CCM kwao hiyo Mahakama ni kama danguro la sheria.....wanachagua nini na wapi wavunje. Hivyo nadhani ni juu ya Mahakama yenyewe kusimama na kuhesabiwa.

Bila shaka CCM wanaonyesha double-standard yenye kuendana na wasifu na malengo yao.

Asante mtoa mada.
 
Hao ndio CCM... Ni wezi na wanyang'anyi.. Walevi wa madaraka na wenye uchu wa MALI. Hawataki kuona wengine kwa namna yeyote ile wanafanikiwa isipokuwa WAO! Siku zote wako na move ya kudhoofisha chochote kilicho kinyume na wao (km sio kukiua kabisaaaa)!!!
 
ninavomjua PINDA ataanza kulia sasa hivi ..shauri zenu nyie mbaneni tu sasa hivi atamwaga chozi
 
ninavomjua PINDA ataanza kulia sasa hivi ..shauri zenu nyie mbaneni tu sasa hivi atamwaga chozi

Pinda amezoea kuvunja sheria, aliruhusu watu kuuawa wakituhumiwa kuua albino(bila kufikishwa mahakamani) alikomaliwa kidogo bungeni akalia kama mtoto mdogo, akahurumiwa, amerudia kwa kuielekeza mahakama ifanye nini kuhusu kesi inayosikilizwa, mimi nasema wabunge watakaomtetea safari hii watakwenda nae mpanda!!!! Nampigia mbuge wa jimbo langu kumtahadharisha na asipotii nita deal naye mpaka ajute kuijua ccm.
 
we mlangaja ulisikia au uliambiwa kaongea pinda au hujui hata aliyeuliza hilo swali? Kwa tarifa yako aliyeuliza hilo swali ni mbowe! Angekataa kujibu napo ungeongea si unajua tena jf siku hizi udaku tupu
 
we mlangaja ulisikia au uliambiwa kaongea pinda au hujui hata aliyeuliza hilo swali? Kwa tarifa yako aliyeuliza hilo swali ni mbowe! Angekataa kujibu napo ungeongea si unajua tena jf siku hizi udaku tupu

emma eeh! Nawe jiulize kama ukiletewa chakula chooni ungekula? Pinda kategwa swali na Pinda ilibidi kueleza kuwa hawezitolewa jawabu kitu kilicho ndani ya mahakama! Mbona wakati mwingne pinda anakuwa na akili. Bunge la9 aligoma kutolea ufafanuzi Meremeta/nanyumbu kwa kuwa ni mradi wa jeshi! Ukiwa muongo uwe mwepesi wa kukumbuka.
 
Back
Top Bottom