Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,813
- 4,545
Wabunge nchini Burkina Faso wamepitisha kwa kauli moja muswada utakaowezesha raia wa kupewa silaha ili kupambana na makundi yenye ya waasi.
Muswada huo ambao sasa unasubiri kutiwa saini na Rais unalengo la kupunguza mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wenye uhusiano na makundi ya al-Qaeda na Islamic State.
Kwa mujibu wa wabunge hao, uwezo wa jeshi wa kupambana na wanamgambo hautoshi kutokana na idadi yao kuwa ndogo lakini pia hawana mafunzo ya kutosha.
“Kwasababu ya tishio linaloendelea, watu wameelezea utashi wao wa kushiriki kikamilifu katika kuilinda nchi yao, lakini huu sio ushahidi wa udhaifu wa jeshi,” ilisisitiza taarifa ya Bunge hilo kwa vyombo vya habari.
Awali Wizara ya Mawasiliano ilisema kuwa wengine watakapewa silaha hizo ni pamoja na kikosi cha kujilinda cha Ufaransa kilichokuwapo wakati wa uvamizi wa Ujerumani wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
Wakosoaji wa wamehoji ikiwa hatu mpya itawafanya watu waumie, lakini serikali inasisitiza kuwa watu watakaojitolea kuwa na silaha ni muhimu kwani watasaidia kumaliza kusambaa kwa ghasia.
Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa na baadhi ya wadau wa haki za binadamu kwa madai kuwa ni hatari kwa usalama wa raia.
Kwa muda mrefu Burkina Faso imekubwa na machafuko yanayofanywa na wanamgambo wa kundi la Islamic State.
Chanzo: Mwananchi