Ahmet
JF-Expert Member
- Oct 15, 2019
- 1,537
- 3,404
Dunia imebadilikia, utandawazi unatukutanisha na watu mbalimbali duniani. Fikra mpya, filosofia na elimu inatujuza mitazamo ya watu mbalimbali katika Historia na hata ulimwengu tulio nao.
Moja kwa moja niende kuelezea kwanini naamini uwepo wa Mungu kwa kutumia hoja za kisayansi zenye kufikirika na hoja za kiroho (kihisia)
HOJA ZA KIULIMWENGU
kwa kuuangalia ulimwengu jinsi ulivyoumbwa basi ni alama tosha ya kuthibisha uwepo wa Mungu.
Sayari, nyota, nebula, Galaksi, mashimo meusi (black holes), miezi, magimba na vyengine vingi.
Nikijaribu kusoma ulimwengu, basi nafsi yangu inaniambia kabisa kuwa Kuna muumba wa vitu vyote hivi. Hivi ni kweli nyota kubwa kubwa Kama Stephenson 2-18, Betelgause, Rigel, Sirius A na nyengine, Nebula kama Carina nebula, Orion nebula, Helix nebula na nyengine nyingi, havina mtengenezaji? Hivi ni kweli vitu vyote hivi vimetokea kwa bahati nasibu?
Ulimwengu ni mkubwa na umeumbwa kwa namna ya kushangaza sana. Mnapo tarehe 11 julai 2022, shirika la utafiti wa anga la Marekani NASA kwa kutumia darubini ya James Webb limeweza kupiga picha za mbali kabisa, wanasayansi wanahuita ukingo wa ulimwengu (edge of the observable universe). Kwakweli picha hizo ni zenye kupendeza sana. Kilichonistaajabisha sana ni kuwa kuna picha imechukuliwa kutoka umbali wa miaka ya mwanga bilioni 4.5 (4.5 billion light years). Umbali huu ni mrefu sana ambao mwanadamu hawezi akapata picha halisi. Lakini kwa tafsiri yenye kueleweka ni kuwa mwanga umesafiri kutoka huko katika ukingo wa ulimwengu hadi hapa duniani kwa miaka bilioni 4.5 iliyopita na hizo galaksi tunazoziona kwenye picha basi tunaziona jinsi nilivyokuwa miaka bilioni 4.5 iliyopita.
Wanasayansi wanathibitisha ya kuwa ulimwengu wenyekuonekana ni sehemu ndogo tu ya ulimwengu mzima, ni nukta tu ya ulimwengu mzima. Wapo wanaothibitisha ya kuwa Kuna ulimwengu zaidi ya mmoja (multiverse). Hivi kwa uumbaji huu ni kweli hakuna mwenye nguvu zisizo za kawaida ambae ndio katengeneza vyote hivyo?
Uwingi wa nyota, galaksi, nebula na vyengine vingi. Uwingi tu wa vitu hivyo unastaajabisha sana. Hizi vyota tumaziona ni nyota chache tu kati ya nyota nyingi katika galaksi yetu yaani milky way. Inakadiliwa kuwa Kuna nyota bilioni 100 hadi 400 katika galaksi yetu yaani milky way. Ni nyota nyingi ambazo kama ungeweza kuziangalia kutoka katika umbali fulani basi ungepata picha halisi. Sasa hii ni galaksi moja na wanasayansi wanakadiria pia kuwa kuna takribani galaksi bilioni 100 hadi 200 katika ulimwengu unaoonekana. Na huu ulimwengu wenyekuonekana ni sehemu tu ya ulimwengu mzima, je Kuna vitu vingapi katika ulimwengu usiooneka?
Mifumo ya kiulimwengu yenye kutulinda wanadamu. Nikiangalia jinsi tabaka la ozoni (ozone layer) inavyotulinda kutokana na mionzi ya UV, mzunguko wa jua na dunia, mwezi na sayari nyengine ambapo Kama vitaenda tofauti basi maisha ya mwanadamu yatakuwa hatarini. Ukitafakari mfumo wa uzungukaji wa maji (water cycle) unaweza ukapata taswira ya kivipi maisha yetu yanategemea huruma ya Mungu. Dunia ingeweza hata kuhama kutoka katika obiti yake. Lakini kuna mlizi wetu ambae halali, anaetupenda.
Kuna magimba makubwa yanayodondoka kila siku, kila saa na dakika, Lakini Mungu kaweka utaratibu wake, magimba hayo huyayuka kabla ya kutufikia binadamu katika uso wa dunia. Ni njia ya Mungu kutulinda binadamu kwani kuna sayari ngapi huangukiwa na magimba hayo.
SABABU ZA KIROHO (KIHISIA)
Kutambua uwepo wa Mungu ni suala la asili ya mwanadamu na viumbe wengine. Tangu tunazaliwa, tunakuwa na utambuzi wa asili juu ya uwepo wa Mungu. Hakuna mtoto ambae haamini uwepo wa Mungu. Ingawa Mungu haonekani lakini mara zote watoto hutaja neno Mungu. Kiasili kila mtu ana schema ya kutambua uwepo wa Mungu lakini mazingira yanaweza yakambadilisha na kuamini kuwa hakuna Mungu.
Mapenzi ya mzazi kwa mtoto, upendo wa mzazi hasa wa mama ni alama ya uwepo wa Mungu. Ukitafakari kwa kina utagundua kuna alieweka mapenzi haya ambae ni Mungu. Na hii si kwa binadamu tu bali hata kwa wanyama pia. Mzazi yuko tayari kuhatarisha uhai wake ili awalinde watoto wake, ona kuku anavyowalinda vifaranga vyake dhidi ya mwewe, nyoka na wanyama wengine. .
Utofauti wa binadamu na wanyama wengine. Hapa najiuliza kwanini binadamu tunavaa nguo, tunasoma elimu mbalimbali, tuna majumba mazuri, teknolojia, usafiri wa anga na kila kitu kizuri, Kila leo binadamu hubadilika na kugundua vitu vipya, mitindo mipya ya mavazi, nyumba na magari hubadilika pia. Maisha ya viumbe wengine yapo hivyo hivyo miaka nenda, miaka rudi. Si ajabu kabisa kuku kumpanda mama yake, kujamiiana kwao huwa ni sehemu yoyote. Binadamu tunahifadhi hadi kinyesi chetu, lakini wanyama hawana utaratibu huo. Ni jambo gumu kwa binadamu kumla binadamu mwenzake lakini leo ukichinja kuku nyumbani kwako basi mabaki ya nyama hiyo unawatupia kuku wengine. Hivi binadamu kuwa na utambuzi, fikra, akili, uwezo kwa kupanga na kuamua umekuja kwa bahati nasibu au ni Mungu ndio kapanga iwe hivyo?
Mifumo ya mwili na jinsi inavyofanya kazi. Hakika binadamu na wanyama wengine wameumbwa katika namna tata sana. Ona Kuna mfumo wa chakula, mfumo wa hewa, mfumo wa utoaji taka mwili, mfumo wa Neva, mfumo wa mzunguko wa damu na mifumo mingine mingi. Mungu amempa Mwanaamu changamoto ya kuumba hata sisimizi na kamwe hataweza.
NI IPI HASARA YA KUTOAMINI MUNGU?
Mbali na hasara kuu ambayo mtu ataipata siku ya malipo kwa kutoamini kwakwe, pia kuna hasara nyingi ambazo zinaitesa dunia ya leo kutokana na upingaji huu.
Kutoamini Mungu kunaondoa utu, mtu ambae haamini Mungu anaweza akaingia katika matendo ambayo hayatamtofautisha yeye na mnyama. Kama tulivyoona awali kuwa mnyama na binadamu ni tofauti basi mtu ambae haamini uwepo wa Mungu anaweza akakaribiana kimatendo na mnyama.
Mambo yafuatayo yamesababishwa kwa kiasi kikubwa na kuto kuwa na imani ya Mungu
i. Filamu za ngono, matamasha ya kutembea utupu na mfano wa hayo.
Dunia leo inashuhudia kilele cha maovu ya mwanadamu. Kuna maelfu kwa malaki ya waigizaji wa filamu za ngono tena kwa namna tofauti.
ii. Kukua kwa matendo ya ushoga, usagaji na kuwekewa kampeni maalumu ili kukuza vitendo hivyo.
iii. Ujambazi, ukatili, mauwaji na maovu mengine. Jamii ambayo watu wake hawaamini Mungu basi ni rahisi sana kuangukia katika dunia yenye migogoro kuuwana na ukatili wa aina zote.
Ili tuijenge jamii yenye ustawi mzuri, maadili mema, ukuaji uchumi na hatimae maendeleo endelevu basi tusimsahau Mungu wetu.
ELIMU, KAZI NA SALA