Machache ya Kushangaza Kuhusu Nchi ya Argentina

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,153
13,223
1. Ni nchi ya NANE KWA Ukubwa Duniani, Ikiwa ni ya Tatu kwa Uchumi miongoni mwa nchi za Kilatini na ya Pili miongoni mwa nchi za Marekani ya Kusini kutokana na kumiliki asilimia kubwa ya madini ya Fedha ambayo pia ni asili ya jina ARGENTINA (Argentum). Hata hivyo uchumi wa ARGENTINA umeporomoka kwa kasi tangu mwaka 1913 ambapo ilikua ya 10 kwa uchumi duniani hadi nafasi ya 54 kwa sasa kutokana na masaibu ya vita ikiwemo vita maarufu ya 'Falkland'


2. Nchi ya Argentina imegawanyika katika majimbo 23 na kila Jimbo LINA KATIBA YAKE wakiunganishwa na serikali ya Shirikisho chini ya Rais Mauricio Macri kwa sasa

3. Mwaka 2001, Nchi ya Argentina Ilivunja rekodi ya Utawala Duniani baada ya Kuongozwa na Marais 5 Ndani ya SIKU KUMI TU kutokana na mitafaruku ya kisiasa

4. Huko Argentina Kila chama kinajitanabaisha kwa AINA YA BIA Mojawapo inayouzwa nchini humo na wafuasi wa chama hujuana kwa aina ya BIA wanayokunywa kwenye BAA@@@
argentina.jpg


5. Huenda Mnakumbuka Diego Amando Maradona ambaye alikua mwanandinga mahiri sana nchini ARGENTINA na Duniani kiasi cha kushwawishi baadhi Raia wa nchi hiyo kuanzisha 'dini ya wafuasi' wa Diego hadi leo -The Iglesia Maradoniana (English: Church of Maradona; literally Maradonian Church )
upload_2016-8-7_0-43-49.jpeg


6. Wargentina wameteseka sana wanapotaka kupata dola ama VISA ya Marekani pindipo wanapotaka kusafiri kwa miaka kadhaa hadi mwaka huu 2016 ambapo ilikua ukitaka kupata dola lazima uandike maombi maalum kueleza unakwenda wapi. lini na kwa nini ili upewe dola

7. Hii ni nchi yenye wataalamu wengi sana duniani wa magonjwa ya akili kutokana pia na kuwa na idadi kubwa ya 'wabwia sembe' (wataalamu 145 kwa kila wakazi 100,000) Huku mji wa Bueno Aires ukiwa na Wilaya nzima ya mateja

8. Kutokana na kubwia sana unga, hii ni nch ya pili duniani kwa wakazi wake kukosa hamu ya kula/APPETITE ikiongozwa na JAPAN ambayo sababu kubwa ni UBIZE

9. Mamlaka ya Nchi imepiga marufuku wazazi katika wa mji alimozaliwa mwanandinga Lionel Messi kuita watoto wao majina ya Mesi ili kuenzi nembo yake Duniani na kuepuka kuwa na Mesi wengi vilaza kisoka
i


10. Yasemekana ukichimba shimo kuuubwa sana ukiwa China Utaibukia Argentina ama Chile....
11 Mwaka 1977, Argentina ilipeleka mama mjamzito huko Antarctica katika jitihada za kuhodhi sehemu ya eneo hilo na mama huyu kufanikiwa kuzaa kiumbe wa kwanza hapo na hivyo kuifanya sehemu hiyo kuwa miliki ya ARGENTINA

12. Licha ya Mwanamapinduzi wa Cuba Che Guevara kuzaliwa Argentina, Papa Francis pia ni zao la nchi hiyo ambapo kabla ya Upapa sasa alikua akitumika kama baunsa wa mlangoni kwenye Baa moja Jijini Buenos Aires wakati akiwa kijana sana na aliwahi kuzungumzia hilo yeye mwenyewe

40 Facts about Argentina ←FACTSlides→
 
najiuliza kama papa alikuwa baumsa katika baa,je kale kasheria ka kutozini kabla ya kuwa mtawa alikizingatia?' au i ipoje wajuzi wa mambo? kwani inasemekana ili uwe mtawa wa kikatoliki au madarka hata ya upadri ,mtu lazima uwe bikra ati.!!!
 
Mtoa mada ana hoja lakini hakujipanga au ameelemewa na hisia kuliko utashi. Hasa hapo namba 6. Ishu ni viza siyo dola pia namba 12. Picha hiyo haina uhalisia. Huo ni mlango wa kanisa siyo Club pia Papa alifanya kazi hiyo akiwa kijana sana hata hajawa padre.
 
Back
Top Bottom