Mabwepande na biashara haramu ya uvamizi wa viwanja

mfyayukulela

Senior Member
May 30, 2017
167
234
Moja kwa moja kwenye mada. Wamiliki wa viwanja vya mradi vilivyopimwa eneo la Mabwe pande, Kinondoni wamekuwa wakisumbuliwa sana na uvamizi uliokubuhu.

Usipoenda ndani ya miezi michache tu wakazi wa kule huvamia kiwanja chako na kuwauzia raia wema wasiojua. Hali hiyo inawaletea usumbufu na hasara wamiliki na pia wanunuzi wanaotapeliwa kila uchwao.

Rai manispaa ya Kinondoni irudishie bikoni zilizoondolewa na wavamizi na kuboresha miundombinu hii itasaidia kupunguza idadi ya wanaotapeliwa.
 
Bila shaka serikali itakuwa mbioni kupata muarobaini wa hao wavamizi wa maeneo ya watu!

Nilimsikia Mkuu wa Wilaya juzi kati akizungumza na wananchi juu ya hayo mambo.
 
Haiwezekani kuendekeza uhuni wa baadhi ya watu kuvamia maeneo ya watu kisha kuwauzia watu kwa utapeli.

Serikali haishindwi na jambo ina mkono mrefu.
 
Wenye maeneo halali wengi wao unakuta walikopa kwa riba wakakatwa marejesho kwa miaka mingi huku wakijinyima na familia zao kusudi wapate pesa ya kununua maeneo kwa wanafamilia,

Sasa Eti wanakuja wahuni wanajifanya kuja kuvamia maeneo hayo na kuyauza

Eti kwa kigezo cha kutokuyaendeleza,

Nani alisema kama eneo halijaendelezwa kwa hiyo livamiwe na kuuzwa?

Na huko kuendeleza unakupimaje?

Mwingine amekuwa akilima Mazao ya msimu kila Mwaka mfano mahindi n.k utasemaje hajaendeleza?

Mbaya zaidi kuna maeneo mengine wamiliki walijenga hadi vibanda lakini wavamizi walivibomoa na kukata viwanja kisha kuuza,!

Serikali iko macho masaa 24 itasimama kwenye haki.
 
Kweli kabisa watu wanajipanga kuendeleza.
 
Kiasi kwamba wamiliki halali hawajengi sababu wavamizi wanajenga kibanda cha chumba kimoja basi kwa kutegeshea.

Na aliyeuziwa kiharamu anaogopa kujenga nyumba kubwa sababu ameshajua ameuziwa mali ya mtu mwingine na itarejeshwa kwa mwenye umiliki halali.

Serikali iingilie kati haraka haki itendeke wamiliki halali warejeshewe maeneo yao ili wayaendeleze haraka.
 
Moja kwa moja kwenye mada. Wamiliki wa viwanja vya mradi vilivyopimwa eneo la Mabwe pande, Kinondoni wamekuwa wakisumbuliwa sana na uvamizi uliokubuhu.

Usipoenda ndani ya miezi michache tu wakazi wa kule huvamia kiwanja chako na kuwauzia raia wema wasiojua. Hali hiyo inawaletea usumbufu na hasara wamiliki na pia wanunuzi wanaotapeliwa kila uchwao.

Rai manispaa ya Kinondoni irudishie bikoni zilizoondolewa na wavamizi na kuboresha miundombinu hii itasaidia kupunguza idadi ya wanaotapeliwa.
yaani kule ni balaaa, mimi mpaka sasa hvi nasumbuana nao polisi baada ya kuuza kiwanja changu !kwa hyo ni vurugu tupu!!inabidi kuwa makini sana
 
Back
Top Bottom