Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,350
- 4,485
Tanga ni moja ya mkoa unaoongoza kwa mito yenye mamba nchini Tanzania, asilimia kubwa ya mito ya kule imejaa wanyama hao kufikia kuwa hatari mno kwa watumiaji. Ipo inajulikana kwa viumbe hawa kama vile Zigi, Pangani, Utomfu nakadhalika. Vilevile ipo isiyojulikana, haswa hii inayopatikana upande barabara iendayo Mombasa.
Nikiwa kama mzawa wa mkoa huo, nimeweza kubaini baadhi ya mito imekuwa chanzo cha vifo kwa wananchi na hata wengine kuwa na vilema vya kudumu. Kisa tu shida ya maji, ambapo mfumo wa maji safi upo mjini, haswa wilaya ya Tanga mjini na ile Tanga vijijini. Kwingine huko hutegemea mito, mabwawa na hata chemchem.
Kutokana na hilo maeneo ya kijiji ambapo ni asili yangu, nimeweza kushuhudia wananchi wakitumia mabwawa na chemchem kwa ajili ya kupata maji ya shughuli za nyumbani.
Baada ya muda fulani imekuwa ikijulikana mabwawa yale yana Mamba, tena wakubwa kwenye maeneo ambayo yapo mbali na mto.
Kila siku nimekuwa nikijiuliza hawa viumbe huwa wafika vipi huko, wanasafiri kufuata au ndo ule mpango wa kuvuna mamba na kuhamishia kwingine ndo unafanyika. Hebu wajuzi wa mambo nipeni ufahamu kwenye hili, niweze kujua.
Kama ni uhamishaji wa mamba kwenda sehemu zingine, inamaana wameona wanavijiji ndiyo milo ya hao wanyama? Maana unakuta eneo hapati chakula cha kutosha hata samaki si wengi.
Hivi hao wenye kutafuta maji kwa ajili ya majumbani hata wapo radhi kwenye bwawa wasioge au kufua karibu ilimradi kulinda usalama wa maji, mnawasaidia au kuwamaliza?
Kama kuna uwezekano wa Mamba kusafiri umbali mrefu kufuata maji ya kujificha pia tujuzane wajuzi, nataka nifahamu kuhusu hili. Ilimradi nisihukumu mamlaka husika, zenye tabia ya kuvuna mamba.
Wasalam!