Mabwawa ya Tanga kuwa na mamba

Hassan Mambosasa

Verified Member
Joined
Aug 2, 2014
Messages
2,166
Points
2,000

Hassan Mambosasa

Verified Member
Joined Aug 2, 2014
2,166 2,000
Tanga ni moja ya mkoa unaoongoza kwa mito yenye mamba nchini Tanzania, asilimia kubwa ya mito ya kule imejaa wanyama hao kufikia kuwa hatari mno kwa watumiaji. Ipo inajulikana kwa viumbe hawa kama vile Zigi, Pangani, Utomfu nakadhalika. Vilevile ipo isiyojulikana, haswa hii inayopatikana upande barabara iendayo Mombasa.

Nikiwa kama mzawa wa mkoa huo, nimeweza kubaini baadhi ya mito imekuwa chanzo cha vifo kwa wananchi na hata wengine kuwa na vilema vya kudumu. Kisa tu shida ya maji, ambapo mfumo wa maji safi upo mjini, haswa wilaya ya Tanga mjini na ile Tanga vijijini. Kwingine huko hutegemea mito, mabwawa na hata chemchem.

Kutokana na hilo maeneo ya kijiji ambapo ni asili yangu, nimeweza kushuhudia wananchi wakitumia mabwawa na chemchem kwa ajili ya kupata maji ya shughuli za nyumbani.

Baada ya muda fulani imekuwa ikijulikana mabwawa yale yana Mamba, tena wakubwa kwenye maeneo ambayo yapo mbali na mto.

Kila siku nimekuwa nikijiuliza hawa viumbe huwa wafika vipi huko, wanasafiri kufuata au ndo ule mpango wa kuvuna mamba na kuhamishia kwingine ndo unafanyika. Hebu wajuzi wa mambo nipeni ufahamu kwenye hili, niweze kujua.

Kama ni uhamishaji wa mamba kwenda sehemu zingine, inamaana wameona wanavijiji ndiyo milo ya hao wanyama? Maana unakuta eneo hapati chakula cha kutosha hata samaki si wengi.
Hivi hao wenye kutafuta maji kwa ajili ya majumbani hata wapo radhi kwenye bwawa wasioge au kufua karibu ilimradi kulinda usalama wa maji, mnawasaidia au kuwamaliza?

Kama kuna uwezekano wa Mamba kusafiri umbali mrefu kufuata maji ya kujificha pia tujuzane wajuzi, nataka nifahamu kuhusu hili. Ilimradi nisihukumu mamlaka husika, zenye tabia ya kuvuna mamba.

Wasalam!
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
4,959
Points
2,000

elvischirwa

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
4,959 2,000

Duh! Mamba wote hao hata picha ya kamjusi ka mamba imeshindikana! Kuna jambo hapo.
 
moudgulf

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2017
Messages
63,427
Points
2,000

moudgulf

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2017
63,427 2,000
Mkuu tatizo la mamba nadhani ni la kitaifa, pamoja na Tanga sidhani kama kuna mkoa ulioathrika zaidi na mamba kama Morogoro. Wilaya ya Kilosa kwenye mito iliyopo huko na wilaya ya Kilombero hasa mto wenye jina hilo na mto Ruaha ambao umepita mkoani humo kuna mamba wa kutisha.
Majimbo ya Morogoro kusini na kusini mashariki kando ya pori la akiba la Selous ni nyumbani kwa mamba. Kwenye majimbo hayo mawili hasa kata za Duthumi, Selembara na Kidunda mamba wamepeleka kilio kuliko Simba na nyoka wanaopatikana kwa wingi maeneo hayo. Bonde la Mto Ruvu pamoja mito washirika ya Duthumi, Mvuha, Mngazi na Mgetta ambayo yote inaelekeza maji yake mto Ruvu ni hatari sana kwa kiumbe huyo
FB_IMG_1539296456155.jpg
mamba kando ya mto Ruvu.
 
jebs2002

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2008
Messages
6,379
Points
2,000

jebs2002

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2008
6,379 2,000
Nimependa ulipoongelea mfumo wa maji safi kwa binadamu, kuwa na mamba wengi hasa kwenye mito siyo swala geni, Australia ina mfano wa kutosha kuhusu hili swala...
Swala ni kuwa control tu mamba, wana nyama nzuri sana kama ya kuku tu...
Ngozi, magamba na meno ya mamba yaweza kunufaisha jamii zilizopo karibu na hiyo mito iliyojaa mamba, hapo ndipo ubunifu wahitajika, swala tutafikiria hivyo?!
Mamba kusafiri muda mrefu kutafuta maji siyo swala geni, ni wanyama wanaohimili shida kuliko viumbe wengine, ila chonde chonde tu hili swala lisihusuhwe na imani potofu, hapo tutapoteza mwelekeo..
 
Hassan Mambosasa

Verified Member
Joined
Aug 2, 2014
Messages
2,166
Points
2,000

Hassan Mambosasa

Verified Member
Joined Aug 2, 2014
2,166 2,000
Mkuu tatizo la mamba nadhani ni la kitaifa, pamoja na Tanga sidhani kama kuna mkoa ulioathrika zaidi na mamba kama Morogoro. Wilaya ya Kilosa kwenye mito iliyopo huko na wilaya ya Kilombero hasa mto wenye jina hilo na mto Ruaha ambao umepita mkoani humo kuna mamba wa kutisha.
Majimbo ya Morogoro kusini na kusini mashariki kando ya pori la akiba la Selous ni nyumbani kwa mamba. Kwenye majimbo hayo mawili hasa kata za Duthumi, Selembara na Kidunda mamba wamepeleka kilio kuliko Simba na nyoka wanaopatikana kwa wingi maeneo hayo. Bonde la Mto Ruvu pamoja mito washirika ya Duthumi, Mvuha, Mngazi na Mgetta ambayo yote inaelekeza maji yake mto Ruvu ni hatari sana kwa kiumbe huyoView attachment 927046 mamba kando ya mto Ruvu.
Mkuu kinachonitis shaka ni bwawa ghafla tu lina mamba siku zote halina. Huwa wanafika vipi?
 
Hassan Mambosasa

Verified Member
Joined
Aug 2, 2014
Messages
2,166
Points
2,000

Hassan Mambosasa

Verified Member
Joined Aug 2, 2014
2,166 2,000
Nimependa ulipoongelea mfumo wa maji safi kwa binadamu, kuwa na mamba wengi hasa kwenye mito siyo swala geni, Australia ina maana mfano wa kutosha kuhusu hili swala...
Swala ni kuwa control tu mamba, wana nyama nzuri sana kama ya kuku tu...
Ngozi, magamba na meno ya mamba yaweza kunufaisha jamii zilizopo karibu na hiyo mito iliyojaa mamba, hapo ndipo ubunifu wahitajika, swala tutafikiria hivyo?!
Mamba kusafiri muda mrefu kutafuta maji siyo swala geni, ni wanyama wanaohimili shida kuliko viumbe wengine, ila chonde chonde tu hili swala lisihusuhwe na imani potofu, hapo tutapoteza mwelekeo..
Sawa mkuu
 
Hassan Mambosasa

Verified Member
Joined
Aug 2, 2014
Messages
2,166
Points
2,000

Hassan Mambosasa

Verified Member
Joined Aug 2, 2014
2,166 2,000
Utomfu = MKURUMUZI
Mbali na Mkurumuzi, mto uliyoleta misiba mingi Tanga mmojawapo ni huu.. Ingawa ndiyo mto ambao mfumo mzima wa majisafi jiji zima la Tanga huanzia hapo, bado maeneo ambayo hayajafikiwa na mifumo huo huko vijijini nje ya jiji. Mfano Muheza, mwaka huu wamekufa watu 17 kisa Mamba
IMG-20181110-WA0007.jpeg
 
Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
35,047
Points
2,000

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
35,047 2,000
Kwa Mfano Kange au maweni kama sijakosea kuna bwawa lina mamba wa kutosha tu ila hawa walibebwa na maji wakati wa mafuriko. Walikua wanafugwa kiwanda cha Rhyno mvua ilipokua kubwa kuta za bwawa lao hapo kiwandani zikapasuka na mamba wakabebwa mpaka huko maweni ambako sasa wameanza kuwa kero na wanakijiji wameshatoa taarifa kwa maliasili ila hamna hatua zinazochukuliwa na ukitegemea hilo eneo mamba walilopo ni eneo linalotumika kwa shughuli za kilimo na ni njia pia ya wanafunzi wakiwa wanaenda mashuleni.
Mkuu kinachonitis shaka ni bwawa ghafla tu lina mamba siku zote halina. Huwa wanafika vipi?
 
Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
35,047
Points
2,000

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
35,047 2,000
Huu mto gani?
Mbali na Mkurumuzi, mto uliyoleta misiba mingi Tanga mmojawapo ni huu.. Ingawa ndiyo mto ambao mfumo mzima wa majisafi jiji zima la Tanga huanzia hapo, bado maeneo ambayo hayajafikiwa na mifumo huo huko vijijini nje ya jiji. Mfano Muheza, mwaka huu wamekufa watu 17 kisa Mamba View attachment 931724
 
Forum statistics

Threads 1,343,529
Members 515,077
Posts 32,787,751
Top