Mabundi na Mapaka yamekuwa yakilia karibu na dirsha langu? Is there anything to worry about?

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,589
2,000
Enzi hizo nitokako akilia bundi au Ndege Fulani hivi simkumbuki au mbwa wakilia sana bila sababu za msingi tena kwa sauti kama ya yowe ilikuwa must MTU wa familia kufa.
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,589
2,000
Imani hizo Mimi sina. Ni Maombi kwa mbele. Soma Isaya 54:14-17. Na pia Mungu amekupa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka. Kanyaga wachawi.
 
Ngurubhe

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,840
2,000
Mim najua paka kuna mda huwa wakiwa kwenye heat period wanapiga sana kelele hadi wa-mate ndio huwa hali hio inaisha kuhusu bundi sjui
 
LuisMkinga

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
1,910
2,000
msh
Kuna mzungu mwanamke tulikuwa tumepanga naye nyumba Arusha. Sasa mapaka meusi yakawa yanalia sana usiku mpaka asubuhi kabisa karibu na mlango wa nyumba. Mimi tumbo moto kutokana na imani zetu hizi za kijinga. Mzungu akanishangaza siku moja aliporudi na chakula cha paka kutoka supamaketi huku akidai eti hao mapaka wana njaa na hawashibi huko wanakolishwa. Basi akawa anayawekea chakula usiku kabla ya kwenda kulala tena mbali kidogo karibu na geti. Kuanzia siku hiyo siku hayo mapaka sikuyasikia tena.

Haya mambo ni imani tu na mazingira ulimokulia. Ndiyo maana nasikia wazungu hata kuwaroga ni kazi kwa sababu hawamo katika wigo huo. Kuanzia siku hiyo nilijifunza kitu na kuachana na hofu hizi zisizo na sababu. Siku hizi wakilia kama nina kiporo nawapa, nasali as usual halafu naenda kuuchapa usingizi bila wasiwasi.
Mshenga wangu aliniambia kuna aina 999 za hofu.., alinitajia kama 30!
 
wasumu

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
2,008
2,000
piga mawe tu mie kabla goba ya dar haijaendelea mwaka2002 kulikuwa na mabund weng sana ....mie kila siku nikupiga tu mawe . nikuua tu . . ila sasa hv goba ni mjin du
 
CleverKING

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
8,508
2,000
Mmmmmh ........loading mshana jr njoo Baba
Acha kua na fikra za kijinga wewe,
huyo unayemuita ndio ameshakubrainwash? Kila kitu mnawaza ni uchawi na ushirikina tu ebo! Tuna safari ndefu sana na viumbe vyenye kuwaza mambo ya kufikirika na kishirikina kwenye kila jambo.
 
Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
23,571
2,000
ungesoma eilimu ya viumbe usingesumbuka ila kuna watu wanaitwa walokole pia wanaweza kukusaidia
 
SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
144,853
2,000
msh

Mshenga wangu aliniambia kuna aina 999 za hofu.., alinitajia kama 30!
Mkuu unaongelea Mshenga yupi? Huyu huyu wa kumrudisha Amina Chifupa na mazingaombwe ya kufufua wafu na kurejesha misukule au mwingine?

Kama ni huyo hata misukule anasema ipo aina 77 halafu akitoka hapo anapanda Hummer yake inayompeleka kwenye helkopita huyooo anapaa kwenda kwenye hekalu lake na kuacha huku nyuma misukule yake ikiwa haina hata nauli ya kupandia daladala. Akili kumkichwa my friend!
 
LuisMkinga

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
1,910
2,000
Mkuu unaongelea Mshenga yupi? Huyu huyu wa kumrudisha Amina Chifupa na mazingaombwe ya kufufua wafu na kurejesha misukule au mwingine?

Kama ni huyo hata misukule anasema ipo aina 77 halafu akitoka hapo anapanda Hummer yake inayompeleka kwenye helkopita huyooo anapaa kwenda kwenye hekalu lake na kuacha huku nyuma misukule yake ikiwa haina hata nauli ya kupandia daladala. Akili kumkichwa my friend!
hapana si yeye huyo.. ni mshenga aliyehusika mimi kufanikisha kuwa na mwenza wa maisha
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,609
2,000
Waungwana, mwezi uliopita Bundi alilia sana akiwa kwenye mti ulio karibu ya dirisha la chumbani kwangu.
Basi kwa Imani yangu ya Kikristo nikapotezea nikiamini kuwa Bundi naye kama ndge wengine ana haki ya kulia.
Sasa jana mapaka mawili nayo yamelia sana from the same spot... Sasa nikihusisha haya matukio mawili nimeanza kuingia na wasiwasi labda inawezekana kuna jambo la ziada kutoka wa hawa viumbe wawili?
Paka kulia usiku kuna aina 2 za paka kulia usiku kuna paka wanga aka paka watu na kuna paka viumbe wanyama sasa inategemea wamelia saa ngapi usiku ? kama ni usiku mapema basi hao watakuwa ni paka wanyama unaweza kutoka nje kuwapelekea chakula la kama kuanzia saa 8 au saa 9 usiku au saa 10 usitoke nje kuwapa chakula hao watakuwa sio paka bali ni wachawi wapo kazini unyamaze kimya wafanye kazi yao huko nje mpaka watakapo maliza kulia. Akilia bundi ujuwe kuna ishara kufa mtu ndani ya nyumba aliyolia au kufa mtu mtaani mwenu.Nijuavyo mimi. Akilai Jogoo saa 6 au saa 7 usiku basi anakuletea habari ya kifo cha mtu unapoishi ishi au katika familai yenu au katika ndugu zako kutatokea msiba. Akilia Mbwa wa mtaani mlio kama mbwa mwitu huyo mbwa akilia usiku kuna ishara ya hapo mtaani atakufa mtu.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,542
2,000
Pole sana mkuu. Yaonesha unaishi kwenye chumba kichafu sana na humo kuna mapanya. Bundi ni ndege mwenye uwezo wa kusikilizia harumfu ya muozo umbali wa km 5. Hivyo, akihisi kuna mzoga ndani ya nyumba huwaita wenzake waje kufikiri namna ya kuutoa huo mzoga ulipo hata ikibidi wagawane.
Paka naye, huweza kumsikia panya akitembea zaidi ya umbali wa mt 10 kwa shurubu zake. Hivyo, kwa kuwa umefunga mlango na dirish, anawasikia panya wanaotembea chumbani na anawatamani tu mkuu.
Dawa;
Fanya usafi ndani na mazingira yanayo kusumbua, hutaona wala kusikia tena hiyo kitu. Sio hivyo, utahama mtaaa
 
Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,670

Jamaniiiiiiiii :D:D:D
 
CleverKING

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
8,508
2,000
Paka kulia usiku kuna aina 2 za paka kulia usiku kuna paka wanga aka paka watu na kuna paka viumbe wanyama sasa inategemea wamelia saa ngapi usiku ? kama ni usiku mapema basi hao watakuwa ni paka wanyama unaweza kutoka nje kuwapelekea chakula la kama kuanzia saa 8 au saa 9 usiku au saa 10 usitoke nje kuwapa chakula hao watakuwa sio paka bali ni wachawi wapo kazini unyamaze kimya wafanye kazi yao huko nje mpaka watakapo maliza kulia. Akilia bundi ujuwe kuna ishara kufa mtu ndani ya nyumba aliyolia au kufa mtu mtaani mwenu.Nijuavyo mimi. Akilai Jogoo saa 6 au saa 7 usiku basi anakuletea habari ya kifo cha mtu unapoishi ishi au katika familai yenu au katika ndugu zako kutatokea msiba. Akilia Mbwa wa mtaani mlio kama mbwa mwitu huyo mbwa akilia usiku kuna ishara ya hapo mtaani atakufa mtu.
Kwahiyo hao viumbe wote uliowataja hapo juu ishara zao hua ni mbaya tuu za kufa mtu? Kwanini isiwe kwa mfano akilia Paka au Bundi ina maana hapo mtaani patatokea harusi? Mbona tunapenda kuamini vitu vibaya tu vitatutokea tunapoona dalili fulani kupitia hao viumbe? Au hua hakuna Jambo jema litakalotokea kwa kuangalia wayafanyayo hao viumbe??!!

Kwanini Bundi ashirikishwe na uchawi? Kwani sio kiumbe wa asili? Kwanini isiwe Sungura au Mwewe??!
 
hali mbaya

Member
Jan 7, 2014
79
95
Waungwana, mwezi uliopita Bundi alilia sana akiwa kwenye mti ulio karibu ya dirisha la chumbani kwangu.
Basi kwa Imani yangu ya Kikristo nikapotezea nikiamini kuwa Bundi naye kama ndge wengine ana haki ya kulia.
Sasa jana mapaka mawili nayo yamelia sana from the same spot... Sasa nikihusisha haya matukio mawili nimeanza kuingia na wasiwasi labda inawezekana kuna jambo la ziada kutoka wa hawa viumbe wawili?
Don't worry you will die soon.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom