kunena
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 506
- 717
LIVE: Katika kikao kinachoendelea muda huu kati ya wafanyabiashara wadogo wa madini na mkuu wa mkoa wa Arusha ndugu Mrisho Gambo wafanyabiashara hao wamempongeza bwana Gambo kwa kumleta mwekezaji wa Tanzanite One kampuni inayochimba madini ya Tanzanite mkoani Manyara.
Kero kubwa ya wafanyabiashara hao imekua ni kubanwa na kampuni hiyo kiasi kwamba maisha yamekua magumu kwani toka kampuni hiyo imeshika hatamu wamekua hawapati tena magonga na vumbi linalokua ni mabaki ya madini ambapo hapo nyuma yalikua yanawasaidia kujikimu kimaisha....
Mwekezaji Ndg Feisal ametoa majibu yenye kutia moyo wafanyabiashara hao na kusema kua watakaa na mbia mwenza kampuni ya STAMICO ili kuona namna gani wanaweza kuwasaidia wafanyabiashara hao kurudi katika hali zao za kawaida kiuchumi.
Pamoja na hayo wafanyabiashara hao wamemshukuru sana mkuu wa mkoa kwa uchapakazi wake na namna anavyojitahidi kutatua changamoto za makundi mbalimbali mkoani Arusha....
Mkuu wa mkoa Ndg Mrisho Gambo
Pembeni ya Mh Gambo ni Mkurugenzi wa Tanzanite One bwana Feisal
Mkuu wa mkoa wa Arusha akiteta jambo na Mh Fabian Daqqaro mkuu wa wilaya ya Arusha mjini
Kamishna wa madini kanda ya kati akitoa majibu kwa wafanyabiashara
Wafanyabiashara wa madini wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mh Gambo kwa umakini