Mabosi wenye magari kuweni makini na wafanyakazi wa ndani

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,857
1,538
Kama mnavyoona iyo ni Benz C500 toleo, ikiwa imepigwa na beki tatu baada ya kukiuka maagizo ya bosi wake, bosi alimwambia chukua gari uoshe na yeye akatekenya na kuingia lamini. Kama mnavyojua gari za kisasa hazinaga madogo jamaa alikamua mafuta ngoma ikachanganya na ikampelekea kushindwa kuimudu na kumtoa road na kutafuna garden ya watu.
IMG_20160307_114333.jpg
IMG_20160307_114104.jpg
IMG_20160307_114100.jpg
IMG_20160307_114022.jpg
IMG_20160307_113803.jpg
IMG_20160307_113812.jpg
IMG_20160307_113858.jpg
 
hii hata mie ilishanitokea, house girl wangu naye alijidai dereva akachukua funguo akawasha na kutia gia, kilichofuatiaaa...ni majanga...nilijenga nyumba ya watu nikatengeneza geti la watu na hasara juu ya gari...na yeye alizimia na kuteguka mguu...
 
Haya hutokea kwa kila mwenye gari kama si mtoto wako au beki tatu.
 
Bora katoka mzima ,ila usede ndio hivyo hasara

Kipato chake chote cha utumishi wake kitaishia kutengeneza gari ya boss wake, na kazi atakuwa hana, atarejea kwao kama alivyokuja, pole sana mtumishi
 
hii hata mie ilishanitokea, house girl wangu naye alijidai dereva akachukua funguo akawasha na kutia gia, kilichofuatiaaa...ni majanga...nilijenga nyumba ya watu nikatengeneza geti la watu na hasara juu ya gari...na yeye alizimia na kuteguka mguu...

Alipata wapi ujasiri wa kuingia kwenye gari yako, looks like hakutunza heshima yako boss, very bad!!
 
Unaanzaje kumpa funguo kijana wa kazi, eti endesha ukaoshe gari, huo ni uzembe. Utakuta hata leseni hana, wa kushitakiwa ni wewe!
 
Back
Top Bottom