Maboresho ya uingizaji umeme kwenye mita za luku nchini

hendeboy

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
218
21
TANGAZO
MABORESHO YA UINGIZAJI UMEME KWENYE MITA ZA LUKU NCHINI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wanaotumia mita za LUKU, Shirika litafanya maboresho kwenye mfumo wa kuuza LUKU tarehe 01/09/2012.MTEJA WA TANESCO UNAYETUMIA MITA ZA LUKU ZINGATIA YAFUATAYO:
  1. Nunua umeme wa kwanza kuanzia tarehe 01/09/2012 kutoka ofisi za TANESCO au wakala wa LUKU. Baada ya hapo utaendelea kununua umeme kwa njia yoyote upendayo kama kawaida.
  2. Utakaponunua umeme kwenye ofisi za TANESCO au wakala wa LUKU utapatiwa namba mbili za maboresho pamoja na Vocha ya umeme .
  3. Mara upatapo namba hizo, tafadhali ziingize kwenye mita yako ukianzia na namba ya mabadilisho ya kwanza (Key Change Token 1), halafu bonyeza ‘ ’ au ‘#’, kisha ingiza namba ya pili (Key Change Token 2) halafu bonyeza ‘ ’ au ‘#’. Mwisho ingiza namba zilizoko kwenye Vocha ya LUKU.
  4. Tembelea ofisi za TANESCO ili kujua wakala wa LUKU unapopaswa kununua umeme na maelekezo zaidi. Pia orodha ya Mawakala immebandikwa kwenye ofisi zao.
Zingatia:Namba hizi (Key Changes) zitapatikana ofisi za TANESCO na wakala wa LUKU walioorozeshwa na TANESCO tu, haziwezi kupatikana kwa kununua umeme kwa njia za MPESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY, ZAP, MAXIMALIPO, NMB Mobile/ATM wala CRDB Mobile. Hivyo wateja wote wanashauriwa wanunue umeme kama inavyoelekezwa.Kwa tatizo lolote fika ofisi ya TANESCO iliyo karibu yako au piga022 219 44 00 au 0768985100.
 
Kwa staili hiyo vishoka na watumishi wengine wa TANESCO wasio waaminifu imekula kwao mazima.
 
Mlikuwa mtuambie haya maboresho yanafaida gani kwetu na kweli na si kutuambia kuna maboresho pasipo kutufafanulia
 
Faida na hasara zake ziwekwe wazi tafadhari msilete utapeli bana
 
Back
Top Bottom