Maboresho ya Posho ya Kuchunguza Maiti kwa Madaktari.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maboresho ya Posho ya Kuchunguza Maiti kwa Madaktari..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samora10, Jul 16, 2012.

 1. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Wakuu ni muda mrefu nimejaribu kufuatilia sakata la mgomo wa madaktari na serikali yetu.. Kiukweli sijafurahishwa na jinsi serikali inavyolishughulikia suala hili, Ni kama vile viongozi wetu wanaendesha nchi kidikteta na hapa sitataka kuanza kuongelea mkasa uliompata ndugu yetu Ulimboka na mengineyo mengi ila kuna mambo sio ya kufumbia macho asilani..

  Fikiria ndugu yako anakufa pale muhimbili halafu mtu anasimama pale bungeni na kuuambia uma eti wamepandisha posho ya kuchunguza maiti na eti huduma ziko sawa na wananchi wasiwe na wasiwasi wakati anajua kabisa kwamba hali sivyo anavyoongea.


  Turudi kwenye hoja ya msingi.. Tumesikia Serikali ikijisifia kupandisha POSHO YA KUCHUNGUZA MAITI toka 5000/= mpaka 100,000/= wakati posho ya daktari anayeacha familia yake nyumbani na kuhudumia wagonjwa masaa 24 akilipwa elfu 20!

  Najiuliza hivi hawa watawala hua wanafikiria nini? Yani walimaanisha nini kuongeza posho ya kuchunguza maiti na kuacha posho ya muhimu kabisa? Ndio kusema kwamba viongozi/wanasiasa wetu wanathamini maiti kuliko huyu anayeokoa maisha ya wagonjwa? Wanataka madaktari waanze kuua ili wapate posho nene za kuchunguza maiti?

  Naomba tutafakari hili..
   
 2. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  samora10 hiyo posho mmoja wa viongozi wa madaktari amewahi izungumzia kwamba kwa hapa nchini madaktari bingwa wa kufanya uchunguzi wa maiti hawazidi 10!
   
 3. F

  FAMILY LAW Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole kamanda, viongozi ndo hatuna,. wanaona ni bora maiti ichunguzwe utadhani watamfufua kuliko kumtibu mgonjwa apone..huku wenyewe wakikwea mapipa kwenda apollo.
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu ukiiangalia sana hii kitu unaweza fikiria mambo mengi sana.. ila tunaenda kubaya sana, hizi siasa zinazowekwa kwenye mambo ya msingi zitakuja kututokea puani siku moja
   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mkuu timbilimu hizo numbers ziliwekwa hapo makusudi ili wananchi waone kwamba kuna madai yameshughulikiwa.. sasa tunawadanganya wananchi ili iweje? hivi hawawezi kabisa kufanya chochote cha maana?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama posho hiyo imepandishwa ni kwa madaktari ambao idadi yao ni watano nchi nzima, ndio maana ulisikia raia wa Ethiopia waliofariki kwenye roli walisubiri daktari atoke Dar. Kama wapo madaktari hao kwanini hawakuwatumia wa Dodoma? Hizo ni FIX za watawala wenu waonekane wanajali sana maslahi ya Madaktari. Mbona hawapandishi maeneo mengine ambapo kuna madaktari wengi.
   
 7. N

  Nambombe Senior Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uwezi amini,utazani nchi inaongozwa na vichaa.Au viongozi wetu wamewekewa micro chip kwenye ubongo na super computer ina control bongo zao.
   
Loading...